1 Mambo ya Nyakati Mlango 16 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 16:1

Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.

1 Mambo ya Nyakati 16:2

Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana.

1 Mambo ya Nyakati 16:3

Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.

1 Mambo ya Nyakati 16:4

Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli;

1 Mambo ya Nyakati 16:5

Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;

1 Mambo ya Nyakati 16:6

nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la agano la Mungu.

1 Mambo ya Nyakati 16:7

Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana, kwa mkono wa Asafu na nduguze.

1 Mambo ya Nyakati 16:8

Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake.

1 Mambo ya Nyakati 16:9

Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; Zitafakarini ajabu zake zote.

1 Mambo ya Nyakati 16:10

Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.

1 Mambo ya Nyakati 16:11

Mtakeni Bwana na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.

1 Mambo ya Nyakati 16:12

Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;

1 Mambo ya Nyakati 16:13

Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake, Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

1 Mambo ya Nyakati 16:14

Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake.

1 Mambo ya Nyakati 16:15

Likumbukeni agano lake milele, Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.

1 Mambo ya Nyakati 16:16

Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka;

1 Mambo ya Nyakati 16:17

Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri, Na Israeli liwe agano la milele.

1 Mambo ya Nyakati 16:18

Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa;

1 Mambo ya Nyakati 16:19

Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa; Naam, watu wachache na wageni ndani yake.

1 Mambo ya Nyakati 16:20

Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.

1 Mambo ya Nyakati 16:21

Hakumwacha mtu awaonee; Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao;

1 Mambo ya Nyakati 16:22

Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.

1 Mambo ya Nyakati 16:23

Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.

1 Mambo ya Nyakati 16:24

Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.

1 Mambo ya Nyakati 16:25

Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.

1 Mambo ya Nyakati 16:26

Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.

1 Mambo ya Nyakati 16:27

Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake.

1 Mambo ya Nyakati 16:28

Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu.

1 Mambo ya Nyakati 16:29

Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu;

1 Mambo ya Nyakati 16:30

Tetemekeni mbele zake, nchi yote.

1 Mambo ya Nyakati 16:31

Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, Bwana ametamalaki;

1 Mambo ya Nyakati 16:32

Bahari na ivume na vyote viijazavyo; Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;

1 Mambo ya Nyakati 16:33

Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha,

1 Mambo ya Nyakati 16:34

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

1 Mambo ya Nyakati 16:35

Nanyi mkaseme, Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.

1 Mambo ya Nyakati 16:36

Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi Bwana.

1 Mambo ya Nyakati 16:37

Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la agano la Bwana, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake.

1 Mambo ya Nyakati 16:38

Naye Obed-edomu, pamoja na ndugu zao, sitini na wanane; Obed-edomu na mwana wa Yeduthuni, na Hosa, wawe mabawabu;

1 Mambo ya Nyakati 16:39

na Sadoki kuhani, na nduguze makuhani, mbele ya maskani ya Bwana katika mahali pa juu palipokuwa huko Gibeoni,

1 Mambo ya Nyakati 16:40

ili kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika torati ya Bwana, aliyowaamuru Israeli;

1 Mambo ya Nyakati 16:41

na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Bwana, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;

1 Mambo ya Nyakati 16:42

na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni.

1 Mambo ya Nyakati 16:43

Kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake; naye Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake.