1 Mambo ya Nyakati Mlango 15 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 15:1

Basi Daudi akajifanyia nyumba katika mji wa Daudi; akapaweka tayari mahali kwa ajili ya sanduku la Mungu, akalipigia hema.

1 Mambo ya Nyakati 15:2

Ndipo Daudi akasema, Haimpasi mtu awaye yote kulichukua sanduku la Mungu, isipokuwa Walawi peke yao; kwa kuwa hao ndio aliowachagua Bwana, ili walichukue sanduku la Mungu, na kumtumikia daima.

1 Mambo ya Nyakati 15:3

Basi Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu, ili kulipandisha sanduku la Bwana, mpaka mahali pake alipoliwekea tayari.

1 Mambo ya Nyakati 15:4

Daudi akawakutanisha wana wa Haruni, na Walawi;

1 Mambo ya Nyakati 15:5

wa wana wa Kohathi; Urieli mkuu wao, na nduguze mia na ishirini;

1 Mambo ya Nyakati 15:6

wa wana wa Merari; Asaya mkuu wao, na nduguze mia mbili na ishirini;

1 Mambo ya Nyakati 15:7

wa wana wa Gershoni; Yoeli mkuu wao, na nduguze mia na thelathini;

1 Mambo ya Nyakati 15:8

wa wana wa Elsafani; Shemaya mkuu wao, na nduguze mia mbili;

1 Mambo ya Nyakati 15:9

wa wana wa Hebroni; Elieli mkuu wao, na nduguze themanini;

1 Mambo ya Nyakati 15:10

wa wana wa Uzieli; Aminadabu mkuu wao, na nduguze mia na kumi na wawili.

1 Mambo ya Nyakati 15:11

Tena, Daudi akawaita Sadoki na Abiathari makuhani, na hao Walawi, Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli, na Aminadabu,

1 Mambo ya Nyakati 15:12

akawaambia, Ninyi ni vichwa vya mbari za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu, ili mlipandishe sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale nilipoliwekea tayari.

1 Mambo ya Nyakati 15:13

Kwani kwa sababu ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, Bwana, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta sawasawa na sheria.

1 Mambo ya Nyakati 15:14

Basi makuhani na Walawi wakajitakasa, ili wapate kulipandisha sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli.

1 Mambo ya Nyakati 15:15

Na wana wa Walawi wakalichukua sanduku la Mungu mabegani mwao kwa miti yake, kama vile Musa alivyoamuru, sawasawa na neno la Bwana.

1 Mambo ya Nyakati 15:16

Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha.

1 Mambo ya Nyakati 15:17

Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi;

1 Mambo ya Nyakati 15:18

na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, mabawabu.

1 Mambo ya Nyakati 15:19

Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;

1 Mambo ya Nyakati 15:20

na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya sauti ya Alamothi;

1 Mambo ya Nyakati 15:21

na Matithiya, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, na Azazia, wenye vinubi vya sauti ya Sheminithi,

1 Mambo ya Nyakati 15:22

waongoze. Na Kenania, mkuu wa Walawi, alikuwa juu ya uchukuzi; yeye aliusimamia uchukuzi, kwa sababu alikuwa mstadi.

1 Mambo ya Nyakati 15:23

Na Berekia na Elkana walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku.

1 Mambo ya Nyakati 15:24

Na Shebania, na Yoshafati, na Nethaneli, na Amasai, na Zekaria, na Benaya, na Eliezeri, makuhani, wakapiga baragumu mbele ya sanduku la Mungu; na Obed-edomu na Yehia walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku.

1 Mambo ya Nyakati 15:25

Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na maakida wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la agano la Bwana kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;

1 Mambo ya Nyakati 15:26

hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la agano la Bwana, wakachinja ng'ombe saba, na kondoo waume saba.

1 Mambo ya Nyakati 15:27

Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.

1 Mambo ya Nyakati 15:28

Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi.

1 Mambo ya Nyakati 15:29

Hata ikawa, sanduku la agano la Bwana lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake.