1 Mambo ya Nyakati Mlango 24 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 24:1

Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

1 Mambo ya Nyakati 24:2

Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani.

1 Mambo ya Nyakati 24:3

Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya usimamizi wao.

1 Mambo ya Nyakati 24:4

Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao; na wa wana wa Ithamari, sawasawa na mbari za baba zao, wanane.

1 Mambo ya Nyakati 24:5

Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.

1 Mambo ya Nyakati 24:6

Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.

1 Mambo ya Nyakati 24:7

Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya;

1 Mambo ya Nyakati 24:8

ya tatu Harimu, ya nne Seorimu;

1 Mambo ya Nyakati 24:9

ya tano Malkia, ya sita Miyamini;

1 Mambo ya Nyakati 24:10

ya saba Hakosi, ya nane Abia;

1 Mambo ya Nyakati 24:11

ya kenda Yeshua, ya kumi Shekania;

1 Mambo ya Nyakati 24:12

ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu;

1 Mambo ya Nyakati 24:13

ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu;

1 Mambo ya Nyakati 24:14

ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri;

1 Mambo ya Nyakati 24:15

ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi;

1 Mambo ya Nyakati 24:16

ya kumi na kenda Pethahia, ya ishirini Ezekieli;

1 Mambo ya Nyakati 24:17

ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli;

1 Mambo ya Nyakati 24:18

ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.

1 Mambo ya Nyakati 24:19

Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, waingie nyumbani mwa Bwana kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.

1 Mambo ya Nyakati 24:20

Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya.

1 Mambo ya Nyakati 24:21

Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao.

1 Mambo ya Nyakati 24:22

Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi.

1 Mambo ya Nyakati 24:23

Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne.

1 Mambo ya Nyakati 24:24

Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri.

1 Mambo ya Nyakati 24:25

Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria.

1 Mambo ya Nyakati 24:26

Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno.

1 Mambo ya Nyakati 24:27

Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri.

1 Mambo ya Nyakati 24:28

Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana.

1 Mambo ya Nyakati 24:29

Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli.

1 Mambo ya Nyakati 24:30

Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata mbari za baba zao.

1 Mambo ya Nyakati 24:31

Hao nao wakatupiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa mbari za baba za makuhani na za Walawi; mbari za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.