Mwanzo Mlango 36 Genesis

Mwanzo 36:1 Genesis 36:1

Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu.

Mwanzo 36:2 Genesis 36:2

Esau alitwaa binti za Kanaani, kuwa wakeze; Ada, binti Eloni, Mhiti, na Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi;

Mwanzo 36:3 Genesis 36:3

na Basemathi, binti Ishmaeli, nduguye Nebayothi.

Mwanzo 36:4 Genesis 36:4

Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli.

Mwanzo 36:5 Genesis 36:5

Oholibama alizaa Yeushi, na Yalamu, na Kora. Hao ndio wana wa Esau aliozaliwa katika nchi ya Kanaani.

Mwanzo 36:6 Genesis 36:6

Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye.

Mwanzo 36:7 Genesis 36:7

Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao.

Mwanzo 36:8 Genesis 36:8

Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.

Mwanzo 36:9 Genesis 36:9

Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri.

Mwanzo 36:10 Genesis 36:10

Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reuli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau.

Mwanzo 36:11 Genesis 36:11

Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi.

Mwanzo 36:12 Genesis 36:12

Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau.

Mwanzo 36:13 Genesis 36:13

Na hawa ni wana wa Reueli, Nahathi, na Zera, na Shama na Miza. Hao walikuwa wana wa Basemathi, mkewe Esau.

Mwanzo 36:14 Genesis 36:14

Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora.

Mwanzo 36:15 Genesis 36:15

Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi,

Mwanzo 36:16 Genesis 36:16

jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio majumbe, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada.

Mwanzo 36:17 Genesis 36:17

Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau.

Mwanzo 36:18 Genesis 36:18

Na hawa ni wana wa Oholibama, mkewe Esau; jumbe Yeushi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau.

Mwanzo 36:19 Genesis 36:19

Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu.

Mwanzo 36:20 Genesis 36:20

Hawa ni wana wa Seiri, Mhori, wenyeji wa nchi ile; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana,

Mwanzo 36:21 Genesis 36:21

na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu.

Mwanzo 36:22 Genesis 36:22

Na wana wa Lotani, ni Hori, na Hemamu; na umbu lake Lotani ni Timna.

Mwanzo 36:23 Genesis 36:23

Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu.

Mwanzo 36:24 Genesis 36:24

Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye.

Mwanzo 36:25 Genesis 36:25

Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana.

Mwanzo 36:26 Genesis 36:26

Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.

Mwanzo 36:27 Genesis 36:27

Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani.

Mwanzo 36:28 Genesis 36:28

Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani.

Mwanzo 36:29 Genesis 36:29

Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana,

Mwanzo 36:30 Genesis 36:30

jumbe Dishoni, jumbe Eseri jumbe Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, kwa habari za majumbe yao, katika nchi ya Seiri.

Mwanzo 36:31 Genesis 36:31

Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli.

Mwanzo 36:32 Genesis 36:32

Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba.

Mwanzo 36:33 Genesis 36:33

Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake.

Mwanzo 36:34 Genesis 36:34

Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake.

Mwanzo 36:35 Genesis 36:35

Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi.

Mwanzo 36:36 Genesis 36:36

Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake.

Mwanzo 36:37 Genesis 36:37

Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake.

Mwanzo 36:38 Genesis 36:38

Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake.

Mwanzo 36:39 Genesis 36:39

Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.

Mwanzo 36:40 Genesis 36:40

Na hayo ndiyo majina ya majumbe waliotoka kwa Esau, kufuata jamaa zao, na mahali pao, kwa majina yao. Jumbe Timna, jumbe Alva, jumbe Yethethi,

Mwanzo 36:41 Genesis 36:41

jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni,

Mwanzo 36:42 Genesis 36:42

jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari,

Mwanzo 36:43 Genesis 36:43

jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kufuata makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu.