Mwanzo 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 1 (Swahili) Genesis 1 (English)

Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Mwanzo 1:1

In the beginning God{After "God," the Hebrew has the two letters "Aleph Tav" (the first and last letters of the Hebrew alphabet) as a grammatical marker.} created the heavens and the earth.

Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mwanzo 1:2

Now the earth was formless and empty. Darkness was on the surface of the deep. God's Spirit was hovering over the surface of the waters.

Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mwanzo 1:3

God said, "Let there be light," and there was light.

Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mwanzo 1:4

God saw the light, and saw that it was good. God divided the light from the darkness.

Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. Mwanzo 1:5

God called the light Day, and the darkness he called Night. There was evening and there was morning, one day.

Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mwanzo 1:6

God said, "Let there be an expanse in the midst of the waters, and let it divide the waters from the waters."

Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mwanzo 1:7

God made the expanse, and divided the waters which were under the expanse from the waters which were above the expanse, and it was so.

Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili. Mwanzo 1:8

God called the expanse sky. There was evening and there was morning, a second day.

Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. Mwanzo 1:9

God said, "Let the waters under the sky be gathered together to one place, and let the dry land appear," and it was so.

Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mwanzo 1:10

God called the dry land Earth, and the gathering together of the waters he called Seas. God saw that it was good.

Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Mwanzo 1:11

God said, "Let the earth put forth grass, herbs yielding seed, and fruit trees bearing fruit after their kind, with its seed in it, on the earth," and it was so.

Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mwanzo 1:12

The earth brought forth grass, herbs yielding seed after their kind, and trees bearing fruit, with its seed in it, after their kind: and God saw that it was good.

Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu. Mwanzo 1:13

There was evening and there was morning, a third day.

Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; Mwanzo 1:14

God said, "Let there be lights in the expanse of sky to divide the day from the night; and let them be for signs, and for seasons, and for days and years;

tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. Mwanzo 1:15

and let them be for lights in the expanse of sky to give light on the earth," and it was so.

Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mwanzo 1:16

God made the two great lights: the greater light to rule the day, and the lesser light to rule the night. He also made the stars.

Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi Mwanzo 1:17

God set them in the expanse of sky to give light to the earth,

na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mwanzo 1:18

and to rule over the day and over the night, and to divide the light from the darkness. God saw that it was good.

Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne. Mwanzo 1:19

There was evening and there was morning, a fourth day.

Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Mwanzo 1:20

God said, "Let the waters swarm with swarms of living creatures, and let birds fly above the earth in the open expanse of sky."

Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mwanzo 1:21

God created the large sea creatures, and every living creature that moves, with which the waters swarmed, after their kind, and every winged bird after its kind. God saw that it was good.

Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. Mwanzo 1:22

God blessed them, saying, "Be fruitful, and multiply, and fill the waters in the seas, and let birds multiply on the earth."

Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano. Mwanzo 1:23

There was evening and there was morning, a fifth day.

Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mwanzo 1:24

God said, "Let the earth bring forth living creatures after their kind, cattle, creeping things, and animals of the earth after their kind," and it was so.

Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mwanzo 1:25

God made the animals of the earth after their kind, and the cattle after their kind, and everything that creeps on the ground after its kind. God saw that it was good.

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mwanzo 1:26

God said, "Let us make man in our image, after our likeness: and let them have dominion over the fish of the sea, and over the birds of the sky, and over the cattle, and over all the earth, and over every creeping thing that creeps on the earth."

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mwanzo 1:27

God created man in his own image. In God's image he created him; male and female he created them.

Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mwanzo 1:28

God blessed them. God said to them, "Be fruitful, multiply, fill the earth, and subdue it. Have dominion over the fish of the sea, over the birds of the sky, and over every living thing that moves on the earth."

Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; Mwanzo 1:29

God said, "Behold, I have given you every herb yielding seed, which is on the surface of all the earth, and every tree, which bears fruit yielding seed. It will be your food.

na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mwanzo 1:30

To every animal of the earth, and to every bird of the sky, and to everything that creeps on the earth, in which there is life, I have given every green herb for food." And it was so.

Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita. Mwanzo 1:31

God saw everything that he had made, and, behold, it was very good. There was evening and there was morning, the sixth day.