Mwanzo 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 2 (Swahili) Genesis 2 (English)

Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Mwanzo 2:1

The heavens and the earth were finished, and all the host of them.

Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mwanzo 2:2

On the seventh day God finished his work which he had made; and he rested on the seventh day from all his work which he had made.

Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. Mwanzo 2:3

God blessed the seventh day, and made it holy, because he rested in it from all his work which he had created and made.

Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi Mwanzo 2:4

This is the history of the generations of the heavens and of the earth when they were created, in the day that Yahweh God made earth and the heavens.

hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; Mwanzo 2:5

No plant of the field was yet in the earth, and no herb of the field had yet sprung up; for Yahweh God had not caused it to rain on the earth. There was not a man to till the ground,

ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi. Mwanzo 2:6

but a mist went up from the earth, and watered the whole surface of the ground.

Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Mwanzo 2:7

Yahweh God formed man from the dust of the ground, and breathed into his nostrils the breath of life; and man became a living soul.

Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya. Mwanzo 2:8

Yahweh God planted a garden eastward, in Eden, and there he put the man whom he had formed.

Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mwanzo 2:9

Out of the ground Yahweh God made every tree to grow that is pleasant to the sight, and good for food; the tree of life also in the midst of the garden, and the tree of the knowledge of good and evil.

Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne. Mwanzo 2:10

A river went out of Eden to water the garden; and from there it was parted, and became four heads.

Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu; Mwanzo 2:11

The name of the first is Pishon: this is the one which flows through the whole land of Havilah, where there is gold;

na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham. Mwanzo 2:12

and the gold of that land is good. There is aromatic resin and the onyx stone.

Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi. Mwanzo 2:13

The name of the second river is Gihon: the same river that flows through the whole land of Cush.

Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati. Mwanzo 2:14

The name of the third river is Hiddekel: this is the one which flows in front of Assyria. The fourth river is the Euphrates.

Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Mwanzo 2:15

Yahweh God took the man, and put him into the garden of Eden to dress it and to keep it.

Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, Mwanzo 2:16

Yahweh God commanded the man, saying, "Of every tree of the garden you may freely eat:

walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. Mwanzo 2:17

but of the tree of the knowledge of good and evil, you shall not eat of it: for in the day that you eat of it you will surely die."

Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Mwanzo 2:18

Yahweh God said, "It is not good that the man should be alone; I will make him a helper suitable for him."

Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake. Mwanzo 2:19

Out of the ground Yahweh God formed every animal of the field, and every bird of the sky, and brought them to the man to see what he would call them. Whatever the man called every living creature, that was its name.

Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye. Mwanzo 2:20

The man gave names to all cattle, and to the birds of the sky, and to every animal of the field; but for man there was not found a helper suitable for him.

Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, Mwanzo 2:21

Yahweh God caused a deep sleep to fall on the man, and he slept; and he took one of his ribs, and closed up the flesh in its place.

na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Mwanzo 2:22

He made the rib, which Yahweh God had taken from the man, into a woman, and brought her to the man.

Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Mwanzo 2:23

The man said, "This is now bone of my bones, and flesh of my flesh. She will be called Woman, because she was taken out of Man."

Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Mwanzo 2:24

Therefore a man will leave his father and his mother, and will join with his wife, and they will be one flesh.

Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya. Mwanzo 2:25

They were both naked, the man and his wife, and were not ashamed.