Mwanzo 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 11 (Swahili) Genesis 11 (English)

Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Mwanzo 11:1

The whole earth was of one language and of one speech.

Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. Mwanzo 11:2

It happened, as they traveled east, that they found a plain in the land of Shinar; and they lived there.

Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Mwanzo 11:3

They said one to another, "Come, let's make brick, and burn them thoroughly." They had brick for stone, and they used tar for mortar.

Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Mwanzo 11:4

They said, "Come, let's build us a city, and a tower, whose top reaches to the sky, and let's make us a name; lest we be scattered abroad on the surface of the whole earth."

Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. Mwanzo 11:5

Yahweh came down to see the city and the tower, which the children of men built.

Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Mwanzo 11:6

Yahweh said, "Behold, they are one people, and they have all one language; and this is what they begin to do. Now nothing will be withheld from them, which they intend to do.

Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. Mwanzo 11:7

Come, let's go down, and there confuse their language, that they may not understand one another's speech."

Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. Mwanzo 11:8

So Yahweh scattered them abroad from there on the surface of all the earth. They stopped building the city.

Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote. Mwanzo 11:9

Therefore the name of it was called Babel, because Yahweh confused the language of all the earth, there. From there, Yahweh scattered them abroad on the surface of all the earth.

Hivi ndivyo vizazi vya Shemu; Shemu alikuwa mtu wa miaka mia akamzaa Arfaksadi miaka miwili baada ya gharika. Mwanzo 11:10

This is the history of the generations of Shem. Shem was one hundred years old, and became the father of Arpachshad two years after the flood.

Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 11:11

Shem lived after he became the father of Arpachshad five hundred years, and became the father of sons and daughters.

Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela. Mwanzo 11:12

Arpachshad lived thirty-five years, and became the father of Shelah.

Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 11:13

Arpachshad lived after he became the father of Shelah four hundred three years, and became the father of sons and daughters.

Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. Mwanzo 11:14

Shelah lived thirty years, and became the father of Eber:

Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 11:15

and Shelah lived after he became the father of Eber four hundred three years, and became the father of sons and daughters.

Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. Mwanzo 11:16

Eber lived thirty-four years, and became the father of Peleg.

Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 11:17

Eber lived after he became the father of Peleg four hundred thirty years, and became the father of sons and daughters.

Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu. Mwanzo 11:18

Peleg lived thirty years, and became the father of Reu.

Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na kenda, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 11:19

Peleg lived after he became the father of Reu two hundred nine years, and became the father of sons and daughters.

Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. Mwanzo 11:20

Reu lived thirty-two years, and became the father of Serug.

Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 11:21

Reu lived after he became the father of Serug two hundred seven years, and became the father of sons and daughters.

Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori. Mwanzo 11:22

Serug lived thirty years, and became the father of Nahor.

Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 11:23

Serug lived after he became the father of Nahor two hundred years, and became the father of sons and daughters.

Nahori akaishi miaka ishirini na kenda, akamzaa Tera. Mwanzo 11:24

Nahor lived twenty-nine years, and became the father of Terah.

Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia na kumi na kenda, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 11:25

Nahor lived after he became the father of Terah one hundred nineteen years, and became the father of sons and daughters.

Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Mwanzo 11:26

Terah lived seventy years, and became the father of Abram, Nahor, and Haran.

Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. Mwanzo 11:27

Now this is the history of the generations of Terah. Terah became the father of Abram, Nahor, and Haran. Haran became the father of Lot.

Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. Mwanzo 11:28

Haran died before his father Terah in the land of his birth, in Ur of the Chaldees.

Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. Mwanzo 11:29

Abram and Nahor took wives. The name of Abram's wife was Sarai, and the name of Nahor's wife, Milcah, the daughter of Haran who was also the father of Iscah.

Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. Mwanzo 11:30

Sarai was barren. She had no child.

Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. Mwanzo 11:31

Terah took Abram his son, Lot the son of Haran, his son's son, and Sarai his daughter-in-law, his son Abram's wife. They went forth from Ur of the Chaldees, to go into the land of Canaan. They came to Haran, and lived there.

Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani. Mwanzo 11:32

The days of Terah were two hundred five years. Terah died in Haran.