Mwanzo 28 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 28 (Swahili) Genesis 28 (English)

Basi Isaka akamwita Yakobo, akambariki, akamwagiza akamwambia, Usitwae mke wa binti za Kanaani. Mwanzo 28:1

Isaac called Jacob, blessed him, and commanded him, "You shall not take a wife of the daughters of Canaan.

Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako. Mwanzo 28:2

Arise, go to Paddan Aram, to the house of Bethuel your mother's father. Take a wife from there from the daughters of Laban, your mother's brother.

Na Mungu Mwenyezi, akubariki, akuzidishe, na kukuongeza, ili uwe mkutano wa makabila. Mwanzo 28:3

May God Almighty bless you, and make you fruitful, and multiply you, that you may be a company of peoples,

Akupe mbaraka wa Ibrahimu, wewe na uzao wako pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, Mungu aliyompa Ibrahimu. Mwanzo 28:4

and give you the blessing of Abraham, to you, and to your seed with you, that you may inherit the land where you travel, which God gave to Abraham."

Basi Isaka akampeleka Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau. Mwanzo 28:5

Isaac sent Jacob away. He went to Paddan Aram to Laban, son of Bethuel the Syrian, Rebekah's brother, Jacob's and Esau's mother.

Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usitwae mke wa binti za Kanaani, Mwanzo 28:6

Now Esau saw that Isaac had blessed Jacob and sent him away to Paddan Aram, to take him a wife from there, and that as he blessed him he gave him a charge, saying, "You shall not take a wife of the daughters of Canaan,"

na ya kuwa Yakobo amewatii babaye na mamaye, akaenda Padan-aramu. Mwanzo 28:7

and that Jacob obeyed his father and his mother, and was gone to Paddan Aram.

Esau akaona ya kuwa binti za Kanaani hawakumpendeza Isaka, baba yake. Mwanzo 28:8

Esau saw that the daughters of Canaan didn't please Isaac, his father.

Basi Esau akaenda kwa Ishmaeli akamtwaa Mahalathi, binti Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, ndugu wa Nebayothi, kuwa mkewe pamoja na wakeze aliokuwa nao. Mwanzo 28:9

Esau went to Ishmael, and took, besides the wives that he had, Mahalath the daughter of Ishmael, Abraham's son, the sister of Nebaioth, to be his wife.

Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Mwanzo 28:10

Jacob went out from Beersheba, and went toward Haran.

Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Mwanzo 28:11

He came to a certain place, and stayed there all night, because the sun had set. He took one of the stones of the place, and put it under his head, and lay down in that place to sleep.

Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Mwanzo 28:12

He dreamed. Behold, a stairway set up on the earth, and the top of it reached to heaven. Behold, the angels of God ascending and descending on it.

Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Mwanzo 28:13

Behold, Yahweh stood above it, and said, "I am Yahweh, the God of Abraham your father, and the God of Isaac. The land whereon you lie, to you will I give it, and to your seed.

Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Mwanzo 28:14

Your seed will be as the dust of the earth, and you will spread abroad to the west, and to the east, and to the north, and to the south. In you and in your seed will all the families of the earth be blessed.

Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. Mwanzo 28:15

Behold, I am with you, and will keep you, wherever you go, and will bring you again into this land. For I will not leave you, until I have done that which I have spoken of to you."

Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Mwanzo 28:16

Jacob awakened out of his sleep, and he said, "Surely Yahweh is in this place, and I didn't know it."

Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. Mwanzo 28:17

He was afraid, and said, "How dreadful is this place! This is none other than God's house, and this is the gate of heaven."

Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Mwanzo 28:18

Jacob rose up early in the morning, and took the stone that he had put under his head, and set it up for a pillar, and poured oil on the top of it.

Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. Mwanzo 28:19

He called the name of that place Bethel, but the name of the city was Luz at the first.

Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; Mwanzo 28:20

Jacob vowed a vow, saying, "If God will be with me, and will keep me in this way that I go, and will give me bread to eat, and clothing to put on,

nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Mwanzo 28:21

so that I come again to my father's house in peace, and Yahweh will be my God,

Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

Mwanzo 28:22

then this stone, which I have set up for a pillar, will be God's house. Of all that you will give me I will surely give the tenth to you."