Mwanzo 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 7 (Swahili) Genesis 7 (English)

Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. Mwanzo 7:1

Yahweh said to Noah, "Come with all of your household into the ark, for I have seen your righteousness before me in this generation.

Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. Mwanzo 7:2

You shall take seven pairs of every clean animal with you, the male and his female. Of the animals that are not clean, take two, the male and his female.

Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote. Mwanzo 7:3

Also of the birds of the sky, seven and seven, male and female, to keep seed alive on the surface of all the earth.

Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali. Mwanzo 7:4

In seven days, I will cause it to rain on the earth for forty days and forty nights. Every living thing that I have made, I will destroy from the surface of the ground."

Nuhu akafanya kama vile Bwana alivyomwamuru. Mwanzo 7:5

Noah did everything that Yahweh commanded him.

Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi. Mwanzo 7:6

Noah was six hundred years old when the flood of waters came on the earth.

Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika. Mwanzo 7:7

Noah went into the ark with his sons, his wife, and his sons' wives, because of the waters of the flood.

Na katika wanyama walio safi, na wanyama wasio safi, na ndege, navyo vyote vitambaavyo juu ya nchi, Mwanzo 7:8

Clean animals, animals that are not clean, birds, and everything that creeps on the ground

wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, mume na mke, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu. Mwanzo 7:9

went by pairs to Noah into the ark, male and female, as God commanded Noah.

Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi. Mwanzo 7:10

It happened after the seven days, that the waters of the flood came on the earth.

Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka. Mwanzo 7:11

In the six hundredth year of Noah's life, in the second month, on the seventeenth day of the month, on the same day all the fountains of the great deep were burst open, and the sky's windows were opened.

Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku. Mwanzo 7:12

The rain was on the earth forty days and forty nights.

Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye; Mwanzo 7:13

In the same day Noah, and Shem, Ham, and Japheth, the sons of Noah, and Noah's wife, and the three wives of his sons with them, entered into the ark;

wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yo yote. Mwanzo 7:14

they, and every animal after its kind, all the cattle after their kind, every creeping thing that creeps on the earth after its kind, and every bird after its kind, every bird of every sort.

Waliingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake. Mwanzo 7:15

They went to Noah into the ark, by pairs of all flesh with the breath of life in them.

Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; Bwana akamfungia. Mwanzo 7:16

Those who went in, went in male and female of all flesh, as God commanded him; and Yahweh shut him in.

Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini; nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi. Mwanzo 7:17

The flood was forty days on the earth. The waters increased, and lifted up the ark, and it was lifted up above the earth.

Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji. Mwanzo 7:18

The waters prevailed, and increased greatly on the earth; and the ark floated on the surface of the waters.

Maji yakapata nguvu sana sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa. Mwanzo 7:19

The waters prevailed exceedingly on the earth. All the high mountains that were under the whole sky were covered.

Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. Mwanzo 7:20

The waters prevailed fifteen cubits upward, and the mountains were covered.

Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; Mwanzo 7:21

All flesh died that moved on the earth, including birds, cattle, animals, every creeping thing that creeps on the earth, and every man.

kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. Mwanzo 7:22

All in whose nostrils was the breath of the spirit of life, of all that was on the dry land, died.

Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina. Mwanzo 7:23

Every living thing was destroyed that was on the surface of the ground, including man, cattle, creeping things, and birds of the sky. They were destroyed from the earth. Only Noah was left, and those who were with him in the ark.

Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini. Mwanzo 7:24

The waters prevailed on the earth one hundred fifty days.