Mwanzo 47 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 47 (Swahili) Genesis 47 (English)

Ndipo Yusufu akaja akamwarifu Farao, akasema, Baba yangu, na ndugu zangu, na kondoo zao, na ng'ombe zao, na yote waliyo nayo, wamekuja kutoka nchi ya Kanaani, nao wako katika nchi ya Gosheni. Mwanzo 47:1

Then Joseph went in and told Pharaoh, and said, "My father and my brothers, with their flocks, their herds, and all that they own, have come out of the land of Canaan; and, behold, they are in the land of Goshen."

Akatwaa watu watano miongoni mwa nduguze, akawasimamisha mbele ya Farao. Mwanzo 47:2

From among his brothers he took five men, and presented them to Pharaoh.

Farao akawauliza hao nduguze, Kazi yenu ni nini? Wakamwambia Farao, Watumwa wako tu wachunga wanyama, sisi, na baba zetu. Mwanzo 47:3

Pharaoh said to his brothers, "What is your occupation?" They said to Pharaoh, "Your servants are shepherds, both we, and our fathers."

Wakamwambia Farao, Tumekuja kukaa ugenini katika nchi hii, kwa sababu wanyama wa watumwa wako hawana malisho, maana njaa ni nzito sana katika nchi ya Kanaani. Basi, twakusihi, uturuhusu sisi watumwa wako tukae katika nchi ya Gosheni. Mwanzo 47:4

They said to Pharaoh, "We have come to live as foreigners in the land, for there is no pasture for your servants' flocks. For the famine is severe in the land of Canaan. Now therefore, please let your servants dwell in the land of Goshen."

Farao akamwambia Yusufu, akisema, Baba yako na ndugu zako wamekujia; Mwanzo 47:5

Pharaoh spoke to Joseph, saying, "Your father and your brothers have come to you.

nchi ya Misri iko mbele yako, palipo pema pa nchi uwakalishe baba yako na ndugu zako; na wakae katika nchi ya Gosheni. Tena ukijua ya kuwa wako watu hodari miongoni mwao, uwaweke wawe wakuu wa wanyama wangu. Mwanzo 47:6

The land of Egypt is before you. Make your father and your brothers dwell in the best of the land. Let them dwell in the land of Goshen. If you know any able men among them, then put them in charge of my cattle."

Yusufu akamleta Yakobo babaye ndani akamweka mbele ya Farao Yakobo akambariki Farao. Mwanzo 47:7

Joseph brought in Jacob, his father, and set him before Pharaoh, and Jacob blessed Pharaoh.

Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi? Mwanzo 47:8

Pharaoh said to Jacob, "How many are the days of the years of your life?"

Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao. Mwanzo 47:9

Jacob said to Pharaoh, "The days of the years of my pilgrimage are one hundred thirty years. Few and evil have been the days of the years of my life, and they have not attained to the days of the years of the life of my fathers in the days of their pilgrimage."

Yakobo akambariki Farao, akatoka mbele ya Farao. Mwanzo 47:10

Jacob blessed Pharaoh, and went out from the presence of Pharaoh.

Yusufu akawakalisha babaye na nduguze, na kuwapa milki katika nchi ya Misri, katika mahali pazuri pa nchi, katika nchi ya Ramesesi, kama Farao alivyoamuru. Mwanzo 47:11

Joseph placed his father and his brothers, and gave them a possession in the land of Egypt, in the best of the land, in the land of Rameses, as Pharaoh had commanded.

Naye Yusufu akawalisha babaye na nduguze na nyumba yote ya babaye, kwa kadiri ya hesabu ya watoto wao. Mwanzo 47:12

Joseph nourished his father, his brothers, and all of his father's household, with bread, according to their families.

Wala hapakuwa na chakula katika nchi yote, kwa kuwa njaa ilikuwa nzito sana, hata nchi ya Misri, na nchi ya Kanaani zikataabika, kwa sababu ya njaa. Mwanzo 47:13

There was no bread in all the land; for the famine was very severe, so that the land of Egypt and the land of Canaan fainted by reason of the famine.

Yusufu akakusanya fedha zote zilizoonekana katika nchi ya Misri na katika nchi ya Kanaani, kwa nafaka waliyoinunua. Yusufu akazileta zile fedha nyumbani mwa Farao. Mwanzo 47:14

Joseph gathered up all the money that was found in the land of Egypt, and in the land of Canaan, for the grain which they bought: and Joseph brought the money into Pharaoh's house.

Fedha zote zilipokwisha katika nchi ya Misri na katika nchi ya Kanaani, Wamisri wote walimjia Yusufu, wakisema, Tupe sisi chakula, kwa nini tufe mbele ya macho yako? Maana fedha zetu zimekwisha. Mwanzo 47:15

When the money was all spent in the land of Egypt, and in the land of Canaan, all the Egyptians came to Joseph, and said, "Give us bread, for why should we die in your presence? For our money fails."

Yusufu akasema, Toeni wanyama wenu, nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu, kama fedha zenu zimekwisha. Mwanzo 47:16

Joseph said, "Give your cattle; and I will give you food for your cattle, if money fails."

Wakaleta wanyama wao kwa Yusufu; Yusufu akawapa chakula badala ya farasi, na badala ya kondoo, na badala ya ng'ombe, na badala ya punda, naye akawalisha chakula badala ya wanyama wao wote mwaka ule. Mwanzo 47:17

They brought their cattle to Joseph, and Joseph gave them bread in exchange for the horses, and for the flocks, and for the herds, and for the donkeys: and he fed them with bread in exchange for all their cattle for that year.

Na mwaka ule ulipokwisha wakamjia mwaka wa pili, wakamwambia, Hatumfichi bwana wetu ya kwamba fedha zetu zimekwisha, na makundi ya wanyama ni mali ya bwana wetu, hakikusalia kitu mbele ya bwana wetu, ila miili yetu na nchi zetu. Mwanzo 47:18

When that year was ended, they came to him the second year, and said to him, "We will not hide from my lord how our money is all spent, and the herds of cattle are my lord's. There is nothing left in the sight of my lord, but our bodies, and our lands.

Kwa nini tufe mbele ya macho yako, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu kwa chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumwa wa Farao; kisha utupe mbegu, tuishi wala tusife, wala nchi yetu isipotee. Mwanzo 47:19

Why should we die before your eyes, both we and our land? Buy us and our land for bread, and we and our land will be servants to Pharaoh. Give us seed, that we may live, and not die, and that the land won't be desolate."

Basi Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri; maana Wamisri waliuza kila mtu shamba lake; kwa sababu njaa ilikuwa imewazidi sana, nchi ikawa mali yake Farao. Mwanzo 47:20

So Joseph bought all the land of Egypt for Pharaoh, for the Egyptians sold every man his field, because the famine was severe on them, and the land became Pharaoh's.

Akawahamisha hao watu, akawaweka katika miji, tangu upande huu wa Misri hata upande huu. Mwanzo 47:21

As for the people, he moved them to the cities from one end of the border of Egypt even to the other end of it.

Ila nchi ya makuhani hakuinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao. Mwanzo 47:22

Only he didn't buy the land of the priests, for the priests had a portion from Pharaoh, and ate their portion which Pharaoh gave them. That is why they didn't sell their land.

Yusufu akawaambia watu, Angalieni, nimewanunua leo, ninyi, na nchi yenu, kuwa mali ya Farao; basi mbegu zenu ni hizi, zipandeni katika nchi. Mwanzo 47:23

Then Joseph said to the people, "Behold, I have bought you and your land today for Pharaoh. Behold, here is seed for you, and you shall sow the land.

Itakuwa wakati wa mavuno mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu wenyewe, kuwa mbegu za nchi, na chakula chenu, na chakula chao waliomo nyumbani mwenu, na chakula cha watoto wenu. Mwanzo 47:24

It will happen at the harvests, that you shall give a fifth to Pharaoh, and four parts will be your own, for seed of the field, for your food, for them of your households, and for food for your little ones."

Wakasema, Umetulinda hai, na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao. Mwanzo 47:25

They said, "You have saved our lives! Let us find favor in the sight of my lord, and we will be Pharaoh's servants."

Yusufu akaifanya sheria kwa habari ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao. Mwanzo 47:26

Joseph made it a statute concerning the land of Egypt to this day, that Pharaoh should have the fifth. Only the land of the priests alone didn't become Pharaoh's.

Israeli akakaa katika nchi ya Misri, katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali humo, wakaongezeka na kuzidi sana. Mwanzo 47:27

Israel lived in the land of Egypt, in the land of Goshen; and they got themselves possessions therein, and were fruitful, and multiplied exceedingly.

Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, basi siku za miaka ya maisha yake Yakobo ilikuwa miaka mia moja na arobaini na saba. Mwanzo 47:28

Jacob lived in the land of Egypt seventeen years. So the days of Jacob, the years of his life, were one hundred forty-seven years.

Siku za kufa kwake Israeli zikakaribia; akamwita mwanawe Yusufu, akamwambia, Kama nimeona kibali machoni pako, weka mkono wako chini ya paja langu, ukanifanyie rehema na kweli; nakusihi usinizike katika Misri. Mwanzo 47:29

The time drew near that Israel must die, and he called his son Joseph, and said to him, "If now I have found favor in your sight, please put your hand under my thigh, and deal kindly and truly with me. Please don't bury me in Egypt,

Lakini nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. Akasema, Nitafanya kama ulivyosema. Mwanzo 47:30

but when I sleep with my fathers, you shall carry me out of Egypt, and bury me in their burying place." He said, "I will do as you have said."

Akanena, Niapie. Naye akamwapia. Israeli akajiinamisha kwenye mchago wa kitanda.

Mwanzo 47:31

He said, "Swear to me," and he swore to him. Israel bowed himself on the bed's head.