Mwanzo 43 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 43 (Swahili) Genesis 43 (English)

Njaa ikawa nzito katika nchi. Mwanzo 43:1

The famine was severe in the land.

Ikawa walipokwisha kula nafaka waliyoileta kutoka Misri, baba yao akawaambia, Rudini huko, mkatununulie chakula kidogo. Mwanzo 43:2

It happened, when they had eaten up the grain which they had brought out of Egypt, their father said to them, "Go again, buy us a little more food."

Yuda akamwambia akisema, Yule mtu alituagizia sana akisema, Hamtaniona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi. Mwanzo 43:3

Judah spoke to him, saying, "The man solemnly warned us, saying, 'You shall not see my face, unless your brother is with you.'

Ukimpeleka ndugu yetu pamoja nasi, tutashuka na kukununulia chakula. Mwanzo 43:4

If you will send our brother with us, we will go down and buy you food,

Ila usipompeleka, hatushuki, maana mtu yule alituambia, Hamtaniona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa pamoja nanyi. Mwanzo 43:5

but if you will not send him, we will not go down, for the man said to us, 'You shall not see my face, unless your brother is with you.'"

Israeli akasema, Mbona mmenitendea vibaya hata mkamwarifu mtu yule ya kwamba mna ndugu mwingine? Mwanzo 43:6

Israel said, "Why did you treat me so badly, telling the man that you had another brother?"

Wakasema, Mtu yule alituhoji sana habari zetu na za jamaa yetu, akisema, Baba yenu angali hai? Mnaye ndugu mwingine? Nasi tukamjibu sawasawa na maswali hayo. Je! Tuliweza kujua ya kwamba atasema, Shukeni pamoja na ndugu yenu? Mwanzo 43:7

They said, "The man asked directly concerning ourselves, and concerning our relatives, saying, 'Is your father still alive? Have you another brother?' We just answered his questions. Is there any way we could know that he would say, 'Bring your brother down?'"

Yuda akamwambia Israeli babaye, Mpeleke kijana pamoja nami, tuondoke, tuende zetu, ili tupate kuishi, wala tusife, sisi na wewe na watoto wetu. Mwanzo 43:8

Judah said to Israel, his father, "Send the boy with me, and we will arise and go, so that we may live, and not die, both we, and you, and also our little ones.

Mimi nitakuwa mdhamini wake, umtake mkononi mwangu. Nisipomleta tena kwako, na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye hatia mbele yako daima; Mwanzo 43:9

I will be collateral for him. From my hand will you require him. If I don't bring him to you, and set him before you, then let me bear the blame forever,

maana kama hatungalikawia, hakika tungaliisha kurudi mara ya pili. Mwanzo 43:10

for unless we had lingered, surely we would have returned a second time by now."

Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi. Mwanzo 43:11

Their father, Israel, said to them, "If it be so now, do this. Take from the choice fruits of the land in your bags, and carry down a present for the man, a little balm, a little honey, spices and myrrh, nuts, and almonds;

Mkatwae fedha maradufu mikononi mwenu, na fedha zile zilizorudishwa kinywani mwa magunia yenu zirudisheni mikononi mwenu; labda zilisahauliwa. Mwanzo 43:12

and take double money in your hand, with the money that was returned in the mouth of your sacks carry again in your hand. Perhaps it was an oversight.

Mtwaeni na ndugu yenu, mwondoke na kurudi kwa mtu yule. Mwanzo 43:13

Take also your brother, and arise, go again to the man.

Mungu Mwenyezi na awape rehema usoni pa mtu yule ili awafungulie ndugu yenu huyo mwingine, na Benyamini. Nami nikifiwa na watoto wangu, nimefiwa. Mwanzo 43:14

May God Almighty give you mercy before the man, that he may release to you your other brother and Benjamin. If I am bereaved of my children, I am bereaved."

Basi hao watu wakatwaa zawadi ile, wakatwaa na fedha maradufu mikononi mwao, na Benyamini; wakaondoka, wakashuka mpaka Misri, wakasimama mbele ya Yusufu. Mwanzo 43:15

The men took that present, and they took double money in their hand, and Benjamin; and rose up, went down to Egypt, and stood before Joseph.

Naye Yusufu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, Uwalete watu hawa nyumbani, ukachinje na kuandalia, maana watu hawa watakula pamoja nami adhuhuri. Mwanzo 43:16

When Joseph saw Benjamin with them, he said to the steward of his house, "Bring the men into the house, and butcher an animal, and make ready; for the men will dine with me at noon."

Yule mtu akafanya kama Yusufu alivyomwambia Naye akawaleta watu hao nyumbani mwa Yusufu. Mwanzo 43:17

The man did as Joseph commanded, and the man brought the men to Joseph's house.

Lakini watu hao wakaogopa kwa sababu wameletwa nyumbani mwa Yusufu, wakasema, Kwa sababu ya fedha zile zilizorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tumeletwa humu; apate kutushitaki, na kutuangukia, atutwae sisi kuwa watumwa, na punda zetu. Mwanzo 43:18

The men were afraid, because they were brought to Joseph's house; and they said, "Because of the money that was returned in our sacks at the first time are we brought in; that he may seek occasion against us, and fall on us, and take us for bondservants, along with our donkeys."

Wakamkaribia yule msimamizi wa nyumba ya Yusufu, wakasema naye mlangoni pa nyumba. Mwanzo 43:19

They came near to the steward of Joseph's house, and they spoke to him at the door of the house,

Wakamwambia, Tazama, bwana, kweli tulishuka mara ya kwanza ili tununue chakula. Mwanzo 43:20

and said, "Oh, my lord, we came indeed down at the first time to buy food:

Ikawa, tulipofika nyumba ya wageni, tukafungua magunia yetu, kumbe! Fedha za kila mtu zilikuwako kinywani mwa gunia lake, fedha zetu kwa uzani wake kamili; nasi tumezileta tena mikononi mwetu. Mwanzo 43:21

and it happened, when we came to the lodging-place, that we opened our sacks, and, behold, every man's money was in the mouth of his sack, our money in full weight. We have brought it again in our hand.

Nasi tumeleta fedha nyingine mikononi mwetu ili tununue chakula; hatujui ni nani aliyezitia fedha zetu katika magunia yetu. Mwanzo 43:22

We have brought down other money in our hand to buy food. We don't know who put our money in our sacks."

Akawaambia, Amani iwe kwenu, msiogope; Mungu wenu, naye ni Mungu wa baba yenu, amewapa akiba katika magunia yenu; fedha zenu ziliniwasilia. Kisha akawatolea Simeoni. Mwanzo 43:23

He said, "Peace be to you. Don't be afraid. Your God, and the God of your father, has given you treasure in your sacks. I received your money." He brought Simeon out to them.

Mtu yule akawaleta wale watu nyumbani mwa Yusufu, akawapa maji, wakatawadha miguu, akawapa punda zao chakula. Mwanzo 43:24

The man brought the men into Joseph's house, and gave them water, and they washed their feet. He gave their donkeys fodder.

Wakaiweka tayari ile zawadi hata atakapokuja Yusufu adhuhuri, maana wamesikia ya kwamba watakula chakula huko. Mwanzo 43:25

They made ready the present for Joseph's coming at noon, for they heard that they should eat bread there.

Alipokuja Yusufu nyumbani, wakamletea ile zawadi iliyokuwa mikononi mwao nyumbani mwake, wakamwinamia mpaka nchi. Mwanzo 43:26

When Joseph came home, they brought him the present which was in their hand into the house, and bowed down themselves to him to the earth.

Akawaulizia hali yao, akasema, Je! Baba yenu, yule mzee mliyemnena, hajambo? Angali hai? Mwanzo 43:27

He asked them of their welfare, and said, "Is your father well, the old man of whom you spoke? Is he yet alive?"

Wakasema, Mtumwa wako baba yetu hajambo, angali hai; wakainama, wakasujudu. Mwanzo 43:28

They said, "Your servant, our father, is well. He is still alive." They bowed the head, and did homage.

Akainua macho yake, akamwona Benyamini, nduguye, mwana wa mamake, akasema, Huyu ndiye ndugu yenu mdogo, mliyeniambia habari zake? Akasema, Mungu akufadhili, mwanangu. Mwanzo 43:29

He lifted up his eyes, and saw Benjamin, his brother, his mother's son, and said, "Is this your youngest brother, of whom you spoke to me?" He said, "God be gracious to you, my son."

Yusufu akafanya haraka, kwa sababu moyo wake ulimwonea shauku nduguye, akatafuta pa kulia, akaingia chumbani mwake, akalia humo. Mwanzo 43:30

Joseph made haste; for his heart yearned over his brother: and he sought a place to weep; and he entered into his room, and wept there.

Akanawa uso, akatoka, akajizuia, akasema, Leteni chakula. Mwanzo 43:31

He washed his face, and came out. He controlled himself, and said, "Serve the meal."

Wakamwandalia yeye peke yake, na wao peke yao, na wale Wamisri waliokula pamoja naye peke yao; maana Wamisri hawawezi kula pamoja na Waebrania, kwa kuwa ni chukizo kwa Wamisri. Mwanzo 43:32

They served him by himself, and them by themselves, and the Egyptians, that ate with him, by themselves, because the Egyptians don't eat bread with the Hebrews, for that is an abomination to the Egyptians.

Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao. Mwanzo 43:33

They sat before him, the firstborn according to his birthright, and the youngest according to his youth, and the men marveled one with another.

Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafanya furaha pamoja naye. Mwanzo 43:34

He sent portions to them from before him, but Benjamin's portion was five times as much as any of theirs. They drank, and were merry with him.