Mwanzo 30 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 30 (Swahili) Genesis 30 (English)

Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi. Mwanzo 30:1

When Rachel saw that she bore Jacob no children, Rachel envied her sister. She said to Jacob, "Give me children, or else I will die."

Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba? Mwanzo 30:2

Jacob's anger was kindled against Rachel, and he said, "Am I in God's place, who has withheld from you the fruit of the womb?"

Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae juu ya magoti yangu, nami nipate uzao kwa yeye. Mwanzo 30:3

She said, "Behold, my maid Bilhah. Go in to her, that she may bear on my knees, and I also may obtain children by her."

Basi akampa Bilha mjakazi wake kuwa mkewe. Yakobo akaingia kwake. Mwanzo 30:4

She gave him Bilhah her handmaid as wife, and Jacob went in to her.

Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana. Mwanzo 30:5

Bilhah conceived, and bore Jacob a son.

Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani. Mwanzo 30:6

Rachel said, "God has judged me, and has also heard my voice, and has given me a son." Therefore called she his name Dan.

Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. Mwanzo 30:7

Bilhah, Rachel's handmaid, conceived again, and bore Jacob a second son.

Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali. Mwanzo 30:8

Rachel said, "With mighty wrestlings have I wrestled with my sister, and have prevailed." She named him Naphtali.

Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe. Mwanzo 30:9

When Leah saw that she had finished bearing, she took Zilpah, her handmaid, and gave her to Jacob as a wife.

Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana. Mwanzo 30:10

Zilpah, Leah's handmaid, bore Jacob a son.

Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi. Mwanzo 30:11

Leah said, "How fortunate!" She named him Gad.

Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili. Mwanzo 30:12

Zilpah, Leah's handmaid, bore Jacob a second son.

Lea akasema, Ni heri mimi, maana wanawake wataniita heri. Akamwita jina lake Asheri. Mwanzo 30:13

Leah said, "Happy am I, for the daughters will call me happy." She named him Asher.

Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao. Mwanzo 30:14

Reuben went in the days of wheat harvest, and found mandrakes in the field, and brought them to his mother, Leah. Then Rachel said to Leah, "Please give me some of your son's mandrakes."

Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang'anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao. Mwanzo 30:15

She said to her, "Is it a small matter that you have taken away my husband? Would you take away my son's mandrakes, also?" Rachel said, "Therefore he will lie with you tonight for your son's mandrakes."

Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa tunguja za mwanangu; akalala kwake usiku ule. Mwanzo 30:16

Jacob came from the field in the evening, and Leah went out to meet him, and said, "You must come in to me; for I have surely hired you with my son's mandrakes." He lay with her that night.

Mungu akamsikia Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano. Mwanzo 30:17

God listened to Leah, and she conceived, and bore Jacob a fifth son.

Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari. Mwanzo 30:18

Leah said, "God has given me my hire, because I gave my handmaid to my husband." She named him Issachar.

Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita. Mwanzo 30:19

Leah conceived again, and bore a sixth son to Jacob.

Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni. Mwanzo 30:20

Leah said, "God has endowed me with a good dowry. Now my husband will live with me, because I have borne him six sons." She named him Zebulun.

Baadaye akazaa binti, akamwita jina lake Dina. Mwanzo 30:21

Afterwards, she bore a daughter, and named her Dinah.

Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo. Mwanzo 30:22

God remembered Rachel, and God listened to her, and opened her womb.

Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu. Mwanzo 30:23

She conceived, bore a son, and said, "God has taken away my reproach."

Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine. Mwanzo 30:24

She named him Joseph,{Joseph means "may he add."} saying, "May Yahweh add another son to me."

Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu. Mwanzo 30:25

It happened, when Rachel had borne Joseph, that Jacob said to Laban, "Send me away, that I may go to my own place, and to my country.

Nipe wake zangu na watoto wangu, niliokutumikia, niende zangu, maana umejua utumishi wangu niliokutumikia. Mwanzo 30:26

Give me my wives and my children for whom I have served you, and let me go: for you know my service with which I have served you."

Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba Bwana amenibariki kwa ajili yako. Mwanzo 30:27

Laban said to him, "If now I have found favor in your eyes, stay here, for I have divined that Yahweh has blessed me for your sake."

Akasema, Sema mshahara wako utakao, nami nitatoa. Mwanzo 30:28

He said, "Appoint me your wages, and I will give it."

Akamwambia, Umejua jinsi nilivyokutumikia, na jinsi wanyama wako walivyokuwa kwangu. Mwanzo 30:29

He said to him, "You know how I have served you, and how your cattle have fared with me.

Maana mali yako ilikuwa haba kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, Bwana akakubariki kila nilikokwenda. Basi sasa, nitaangalia lini mambo ya nyumba yangu mwenyewe? Mwanzo 30:30

For it was little which you had before I came, and it has increased to a multitude. Yahweh has blessed you wherever I turned. Now when will I provide for my own house also?"

Akamwuliza, Nikupe nini? Yakobo akasema, Usinipe kitu; ukinifanyia neno hili, nitalisha wanyama wako tena na kuwalinda. Mwanzo 30:31

He said, "What shall I give you?" Jacob said, "You shall not give me anything. If you will do this thing for me, I will again feed your flock and keep it.

Nitapita katika wanyama wako wote leo, na kutoa huko kila mnyama aliye na madoadoa na marakaraka, na kila mnyama mweusi katika hao kondoo, na aliye na marakaraka na madoadoa katika mbuzi; nao watakuwa mshahara wangu. Mwanzo 30:32

I will pass through all your flock today, removing from there every speckled and spotted one, and every black one among the sheep, and the spotted and speckled among the goats. This will be my hire.

Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa. Mwanzo 30:33

So my righteousness will answer for me hereafter, when you come concerning my hire that is before you. Everyone that is not speckled and spotted among the goats, and black among the sheep, that might be with me, will be counted stolen."

Labani akasema, Tazama, na iwe hivi kama usemavyo. Mwanzo 30:34

Laban said, "Behold, I desire it to be according to your word."

Basi akatoa siku ile mbuzi waume walio na milia na madoadoa, na mbuzi wake walio na madoadoa na marakaraka, kila aliye na doa jeupe, na kondoo wote waliokuwa weusi, akawatia mikononi mwa wanawe. Mwanzo 30:35

That day, he removed the male goats that were streaked and spotted, and all the female goats that were speckled and spotted, every one that had white in it, and all the black ones among the sheep, and gave them into the hand of his sons.

Akajitenga na Yakobo mwendo wa siku tatu; naye Yakobo akachunga wanyama wa Labani waliosalia. Mwanzo 30:36

He set three days' journey between himself and Jacob, and Jacob fed the rest of Laban's flocks.

Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito. Mwanzo 30:37

Jacob took to himself rods of fresh poplar, almond, plane tree, peeled white streaks in them, and made the white appear which was in the rods.

Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa. Mwanzo 30:38

He set the rods which he had peeled opposite the flocks in the gutters in the watering-troughs where the flocks came to drink. They conceived when they came to drink.

Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka. Mwanzo 30:39

The flocks conceived before the rods, and the flocks brought forth streaked, speckled, and spotted.

Na Yakobo akawatenga wana-kondoo, akazielekeza nyuso za makundi zielekee wale waliokuwa na milia, na kila aliyekuwa mweusi katika wanyama wa Labani. Akaweka kando wanyama wake mwenyewe, wala hakuwachanganya pamoja na wanyama wa Labani. Mwanzo 30:40

Jacob separated the lambs, and set the faces of the flocks toward the streaked and all the black in the flock of Laban: and he put his own droves apart, and didn't put them into Laban's flock.

Ikawa kila walipopata mimba wanyama wenye nguvu, Yakobo akaziweka zile fito mbele ya macho ya hao wanyama katika mabirika ili kwamba wachukue mimba kati ya zile fito, Mwanzo 30:41

It happened, whenever the stronger of the flock conceived, that Jacob laid the rods before the eyes of the flock in the gutters, that they might conceive among the rods;

lakini wanyama walipodhoofika hakuziweka zile fito. Basi wale dhaifu walikuwa wa Labani, na wenye nguvu walikuwa wa Yakobo. Mwanzo 30:42

but when the flock were feeble, he didn't put them in. So the feebler were Laban's, and the stronger Jacob's.

Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda. Mwanzo 30:43

The man increased exceedingly, and had large flocks, maid-servants and men-servants, and camels and donkeys.