Mwanzo 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 21 (Swahili) Genesis 21 (English)

Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema. Mwanzo 21:1

Yahweh visited Sarah as he had said, and Yahweh did to Sarah as he had spoken.

Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. Mwanzo 21:2

Sarah conceived, and bore Abraham a son in his old age, at the set time of which God had spoken to him.

Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia. Mwanzo 21:3

Abraham called his son who was born to him, whom Sarah bare to him, Isaac.{Isaac means "He laughs."}

Ibrahimu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru. Mwanzo 21:4

Abraham circumcised his son, Isaac, when he was eight days old, as God had commanded him.

Naye Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka. Mwanzo 21:5

Abraham was one hundred years old when his son, Isaac, was born to him.

Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami. Mwanzo 21:6

Sarah said, "God has made me laugh. Everyone who hears will laugh with me."

Akasema, N'nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake. Mwanzo 21:7

She said, "Who would have said to Abraham, that Sarah would nurse children? For I have borne him a son in his old age."

Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya. Mwanzo 21:8

The child grew, and was weaned. Abraham made a great feast on the day that Isaac was weaned.

Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Mwanzo 21:9

Sarah saw the son of Hagar the Egyptian, whom she had borne to Abraham, mocking.

Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. Mwanzo 21:10

Therefore she said to Abraham, "Cast out this handmaid and her son! For the son of this handmaid will not be heir with my son, even with Isaac."

Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. Mwanzo 21:11

The thing was very grievous in Abraham's sight on account of his son.

Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. Mwanzo 21:12

God said to Abraham, "Don't let it be grievous in your sight because of the boy, and because of your handmaid. In all that Sarah says to you, listen to her voice. For from Isaac will your seed be called.

Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako. Mwanzo 21:13

Also of the son of the handmaid will I make a nation, because he is your seed."

Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. Mwanzo 21:14

Abraham rose up early in the morning, and took bread and a bottle of water, and gave it to Hagar, putting it on her shoulder, and gave her the child, and sent her away. She departed, and wandered in the wilderness of Beersheba.

Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. Mwanzo 21:15

The water in the bottle was spent, and she cast the child under one of the shrubs.

Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia. Mwanzo 21:16

She went and sat down opposite him, a good way off, about a bow shot away. For she said, "Don't let me see the death of the child." She sat over against him, and lifted up her voice, and wept.

Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Mwanzo 21:17

God heard the voice of the boy. The angel of God called to Hagar out of the sky, and said to her, "What ails you, Hagar? Don't be afraid. For God has heard the voice of the boy where he is.

Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. Mwanzo 21:18

Get up, lift up the boy, and hold him in your hand. For I will make him a great nation."

Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana. Mwanzo 21:19

God opened her eyes, and she saw a well of water. She went, filled the bottle with water, and gave the boy drink.

Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde. Mwanzo 21:20

God was with the boy, and he grew. He lived in the wilderness, and became, as he grew up, an archer.

Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri. Mwanzo 21:21

He lived in the wilderness of Paran. His mother took a wife for him out of the land of Egypt.

Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Ibrahimu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda. Mwanzo 21:22

It happened at that time, that Abimelech and Phicol the captain of his host spoke to Abraham, saying, "God is with you in all that you do.

Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake. Mwanzo 21:23

Now therefore swear to me here by God that you will not deal falsely with me, nor with my son, nor with my son's son. But according to the kindness that I have done to you, you shall do to me, and to the land in which you have lived as a foreigner."

Ibrahimu akasema, Nitaapa. Mwanzo 21:24

Abraham said, "I will swear."

Kisha Ibrahimu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumwa wa Abimeleki wamekinyang'anya. Mwanzo 21:25

Abraham complained to Abimelech because of a water well, which Abimelech's servants had violently taken away.

Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu. Mwanzo 21:26

Abimelech said, "I don't know who has done this thing. Neither did you tell me, neither did I hear of it, until today."

Ibrahimu akatwaa kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano. Mwanzo 21:27

Abraham took sheep and oxen, and gave them to Abimelech. Those two made a covenant.

Ibrahimu akaweka wana kondoo wa kike saba peke yao. Mwanzo 21:28

Abraham set seven ewe lambs of the flock by themselves.

Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini? Mwanzo 21:29

Abimelech said to Abraham, "What do these seven ewe lambs which you have set by themselves mean?"

Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki. Mwanzo 21:30

He said, "You shall take these seven ewe lambs from my hand, that it may be a witness to me, that I have dug this well."

Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili. Mwanzo 21:31

Therefore he called that place Beersheba,{Beersheba can mean "well of the oath" or "well of seven."} because they both swore there.

Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti. Mwanzo 21:32

So they made a covenant at Beersheba. Abimelech rose up with Phicol, the captain of his host, and they returned into the land of the Philistines.

Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la Bwana Mungu wa milele. Mwanzo 21:33

Abraham planted a tamarisk tree in Beersheba, and called there on the name of Yahweh, the Everlasting God.

Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi. Mwanzo 21:34

Abraham lived as a foreigner in the land of the Philistines many days.