Mwanzo 40 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 40 (Swahili) Genesis 40 (English)

Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri. Mwanzo 40:1

It happened after these things, that the butler of the king of Egypt and his baker offended their lord, the king of Egypt.

Farao akawaghadhibikia maakida wake wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji. Mwanzo 40:2

Pharaoh was angry with his two officers, the chief cupbearer and the chief baker.

Akawatia katika lindo nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani, mahali alipofungwa Yusufu. Mwanzo 40:3

He put them in custody in the house of the captain of the guard, into the prison, the place where Joseph was bound.

Mkuu wa askari akamwekea Yusufu watu hao, naye akawahudumu, nao wakakaa siku kadha wa kadha katika kifungo. Mwanzo 40:4

The captain of the guard assigned them to Joseph, and he took care of them. They stayed in prison many days.

Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. Mwanzo 40:5

They both dreamed a dream, each man his dream, in one night, each man according to the interpretation of his dream, the cupbearer and the baker of the king of Egypt, who were bound in the prison.

Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika. Mwanzo 40:6

Joseph came in to them in the morning, and saw them, and saw that they were sad.

Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? Mwanzo 40:7

He asked Pharaoh's officers who were with him in custody in his master's house, saying, "Why do you look so sad today?"

Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie. Mwanzo 40:8

They said to him, "We have dreamed a dream, and there is no one who can interpret it." Joseph said to them, "Don't interpretations belong to God? Please tell it to me."

Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu. Mwanzo 40:9

The chief cupbearer told his dream to Joseph, and said to him, "In my dream, behold, a vine was in front of me,

Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva. Mwanzo 40:10

and in the vine were three branches. It was as though it budded, its blossoms shot forth, and the clusters of it brought forth ripe grapes.

Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake. Mwanzo 40:11

Pharaoh's cup was in my hand; and I took the grapes, and pressed them into Pharaoh's cup, and I gave the cup into Pharaoh's hand."

Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu. Mwanzo 40:12

Joseph said to him, "This is the interpretation of it: the three branches are three days.

Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake. Mwanzo 40:13

Within three more days, Pharaoh will lift up your head, and restore you to your office. You will give Pharaoh's cup into his hand, the way you did when you were his cupbearer.

Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii. Mwanzo 40:14

But remember me when it will be well with you, and show kindness, please, to me, and make mention of me to Pharaoh, and bring me out of this house.

Kwa sababu hakika naliibiwa kutoka nchi ya Waebrania, wala hapa sikutenda neno lo lote hata wanitie gerezani. Mwanzo 40:15

For indeed, I was stolen away out of the land of the Hebrews, and here also have I done nothing that they should put me into the dungeon."

Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu. Mwanzo 40:16

When the chief baker saw that the interpretation was good, he said to Joseph, "I also was in my dream, and, behold, three baskets of white bread were on my head.

Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu. Mwanzo 40:17

In the uppermost basket there was all kinds of baked food for Pharaoh, and the birds ate them out of the basket on my head."

Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu. Mwanzo 40:18

Joseph answered, "This is the interpretation of it. The three baskets are three days.

Baada ya siku tatu Farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako. Mwanzo 40:19

Within three more days, Pharaoh will lift up your head from off you, and will hang you on a tree; and the birds will eat your flesh from off you."

Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake. Mwanzo 40:20

It happened the third day, which was Pharaoh's birthday, that he made a feast for all his servants, and he lifted up the head of the chief cupbearer and the head of the chief baker among his servants.

Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, naye akampa Farao kikombe mkononi mwake. Mwanzo 40:21

He restored the chief cupbearer to his position again, and he gave the cup into Pharaoh's hand;

Bali akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyowafasiria. Mwanzo 40:22

but he hanged the chief baker, as Joseph had interpreted to them.

Lakini huyo mkuu wa wanyweshaji hakumkumbuka Yusufu, alimsahau.

Mwanzo 40:23

Yet the chief cupbearer didn't remember Joseph, but forgot him.