Mwanzo 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 10 (Swahili) Genesis 10 (English)

Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. Mwanzo 10:1

Now this is the history of the generations of the sons of Noah and of Shem, Ham, and Japheth. Sons were born to them after the flood.

Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Mwanzo 10:2

The sons of Japheth: Gomer, Magog, Madai, Javan, Tubal, Meshech, and Tiras.

Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Mwanzo 10:3

The sons of Gomer: Ashkenaz, Riphath, and Togarmah.

Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. Mwanzo 10:4

The sons of Javan: Elishah, Tarshish, Kittim, and Dodanim.

Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao. Mwanzo 10:5

Of these were the isles of the nations divided in their lands, everyone after his language, after their families, in their nations.

Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Mwanzo 10:6

The sons of Ham: Cush, Mizraim, Put, and Canaan.

Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani. Mwanzo 10:7

The sons of Cush: Seba, Havilah, Sabtah, Raamah, and Sabteca. The sons of Raamah: Sheba and Dedan.

Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Mwanzo 10:8

Cush became the father of Nimrod: he began to be a mighty one in the earth.

Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana. Mwanzo 10:9

He was a mighty hunter before Yahweh. Therefore it is said, "Like Nimrod, a mighty hunter before Yahweh."

Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari. Mwanzo 10:10

The beginning of his kingdom was Babel, Erech, Accad, and Calneh, in the land of Shinar.

Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala; Mwanzo 10:11

Out of that land he went forth into Assyria, and built Nineveh, Rehoboth Ir, Calah,

na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa. Mwanzo 10:12

and Resen between Nineveh and Calah (the same is the great city).

Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, Mwanzo 10:13

Mizraim became the father of Ludim, Anamim, Lehabim, Naphtuhim,

na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori. Mwanzo 10:14

Pathrusim, Casluhim (which the Philistines descended from), and Caphtorim.

Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, Mwanzo 10:15

Canaan became the father of Sidon (his firstborn), Heth,

na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi, Mwanzo 10:16

the Jebusite, the Amorite, the Girgashite,

na Mhivi, na Mwarki, na Msini, Mwanzo 10:17

the Hivite, the Arkite, the Sinite,

na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana. Mwanzo 10:18

the Arvadite, the Zemarite, and the Hamathite. Afterward the families of the Canaanites were spread abroad.

Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha. Mwanzo 10:19

The border of the Canaanites was from Sidon, as you go toward Gerar, to Gaza; as you go toward Sodom, Gomorrah, Admah, and Zeboiim, to Lasha.

Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. Mwanzo 10:20

These are the sons of Ham, after their families, after their languages, in their lands, in their nations.

Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana. Mwanzo 10:21

To Shem, the father of all the children of Eber, the elder brother of Japheth, to him also were children born.

Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu. Mwanzo 10:22

The sons of Shem: Elam, Asshur, Arpachshad, Lud, and Aram.

Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Mwanzo 10:23

The sons of Aram: Uz, Hul, Gether, and Mash.

Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi. Mwanzo 10:24

Arpachshad became the father of Shelah. Shelah became the father of Eber.

Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani. Mwanzo 10:25

To Eber were born two sons. The name of the one was Peleg, for in his days was the earth divided. His brother's name was Joktan.

Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera, Mwanzo 10:26

Joktan became the father of Almodad, Sheleph, Hazarmaveth, Jerah,

na Hadoramu, na Uzali, na Dikla, Mwanzo 10:27

Hadoram, Uzal, Diklah,

na Obali, na Abimaeli, na Seba, Mwanzo 10:28

Obal, Abimael, Sheba,

na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Mwanzo 10:29

Ophir, Havilah, and Jobab. All these were the sons of Joktan.

Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki. Mwanzo 10:30

Their dwelling was from Mesha, as you go toward Sephar, the mountain of the east.

Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. Mwanzo 10:31

These are the sons of Shem, after their families, after their languages, in their lands, after their nations.

Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika. Mwanzo 10:32

These are the families of the sons of Noah, after their generations, in their nations. Of these were the nations divided in the earth after the flood.