Mwanzo 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 4 (Swahili) Genesis 4 (English)

Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. Mwanzo 4:1

The man knew Eve his wife. She conceived, and gave birth to Cain, and said, "I have gotten a man with Yahweh's help."

Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Mwanzo 4:2

Again she gave birth, to Cain's brother Abel. Abel was a keeper of sheep, but Cain was a tiller of the ground.

Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Mwanzo 4:3

As time passed, it happened that Cain brought an offering to Yahweh from the fruit of the ground.

Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; Mwanzo 4:4

Abel also brought some of the firstborn of his flock and of the fat of it. Yahweh respected Abel and his offering,

bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. Mwanzo 4:5

but he didn't respect Cain and his offering. Cain was very angry, and the expression on his face fell.

Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Mwanzo 4:6

Yahweh said to Cain, "Why are you angry? Why has the expression of your face fallen?

Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Mwanzo 4:7

If you do well, will it not be lifted up? If you don't do well, sin crouches at the door. Its desire is for you, but you are to rule over it."

Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua. Mwanzo 4:8

Cain said to Abel, his brother, "Let's go into the field." It happened, when they were in the field, that Cain rose up against Abel, his brother, and killed him.

Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Mwanzo 4:9

Yahweh said to Cain, "Where is Abel, your brother?" He said, "I don't know. Am I my brother's keeper?"

Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Mwanzo 4:10

Yahweh said, "What have you done? The voice of your brother's blood cries to me from the ground.

Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; Mwanzo 4:11

Now you are cursed because of the ground, which has opened its mouth to receive your brother's blood from your hand.

utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. Mwanzo 4:12

From now on, when you till the ground, it won't yield its strength to you. You shall be a fugitive and a wanderer in the earth."

Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Mwanzo 4:13

Cain said to Yahweh, "My punishment is greater than I can bear.

Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. Mwanzo 4:14

Behold, you have driven me out this day from the surface of the ground. I will be hidden from your face, and I will be a fugitive and a wanderer in the earth. It will happen that whoever finds me will kill me."

Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. Mwanzo 4:15

Yahweh said to him, "Therefore whoever slays Cain, vengeance will be taken on him sevenfold." Yahweh appointed a sign for Cain, lest any finding him should strike him.

Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. Mwanzo 4:16

Cain went out from Yahweh's presence, and dwelt in the land of Nod, on the east of Eden.

Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe. Mwanzo 4:17

Cain knew his wife. She conceived, and gave birth to Enoch. He built a city, and called the name of the city, after the name of his son, Enoch.

Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki. Mwanzo 4:18

To Enoch was born Irad. Irad became the father of Mehujael. Mehujael became the father of Methushael. Methushael became the father of Lamech.

Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila. Mwanzo 4:19

Lamech took two wives: the name of the one was Adah, and the name of the other Zillah.

Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. Mwanzo 4:20

Adah gave birth to Jabal, who was the father of those who dwell in tents and have cattle.

Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi. Mwanzo 4:21

His brother's name was Jubal, who was the father of all who handle the harp and pipe.

Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama. Mwanzo 4:22

Zillah also gave birth to Tubal Cain, the forger of every cutting instrument of brass and iron. Tubal Cain's sister was Naamah.

Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua; Mwanzo 4:23

Lamech said to his wives, "Adah and Zillah, Hear my voice, You wives of Lamech, listen to my speech, For I have slain a man for wounding me, A young man for bruising me.

Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba. Mwanzo 4:24

If Cain will be avenged seven times, Truly Lamech seventy-seven times."

Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. Mwanzo 4:25

Adam knew his wife again. She gave birth to a son, and named him Seth. For, she said, "God has appointed me another child instead of Abel, for Cain killed him."

Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana. Mwanzo 4:26

There was also born a son to Seth, and he named him Enosh. Then men began to call on Yahweh's name.