Mwanzo Mlango 35 Genesis

Mwanzo 35:1 Genesis 35:1

Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako.

Mwanzo 35:2 Genesis 35:2

Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu.

Mwanzo 35:3 Genesis 35:3

Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea.

Mwanzo 35:4 Genesis 35:4

Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.

Mwanzo 35:5 Genesis 35:5

Wakashika njia, hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo.

Mwanzo 35:6 Genesis 35:6

Basi Yakobo akafika Luzu, ulio katika nchi ya Kanaani, ndio Betheli, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye.

Mwanzo 35:7 Genesis 35:7

Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake.

Mwanzo 35:8 Genesis 35:8

Akafa Debora mlezi wa Rebeka, akazikwa chini ya Betheli, chini ya mwaloni; na jina lake likaitwa Alon-bakuthi.

Mwanzo 35:9 Genesis 35:9

Mungu akamtokea Yakobo tena, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.

Mwanzo 35:10 Genesis 35:10

Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.

Mwanzo 35:11 Genesis 35:11

Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.

Mwanzo 35:12 Genesis 35:12

Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.

Mwanzo 35:13 Genesis 35:13

Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.

Mwanzo 35:14 Genesis 35:14

Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake.

Mwanzo 35:15 Genesis 35:15

Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.

Mwanzo 35:16 Genesis 35:16

Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.

Mwanzo 35:17 Genesis 35:17

Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine.

Mwanzo 35:18 Genesis 35:18

Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.

Mwanzo 35:19 Genesis 35:19

Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.

Mwanzo 35:20 Genesis 35:20

Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.

Mwanzo 35:21 Genesis 35:21

Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili wa mnara wa Ederi.

Mwanzo 35:22 Genesis 35:22

Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.

Mwanzo 35:23 Genesis 35:23

Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.

Mwanzo 35:24 Genesis 35:24

Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini.

Mwanzo 35:25 Genesis 35:25

Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali.

Mwanzo 35:26 Genesis 35:26

Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.

Mwanzo 35:27 Genesis 35:27

Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Ibrahimu na Isaka.

Mwanzo 35:28 Genesis 35:28

Siku za Isaka zilikuwa miaka mia na themanini.

Mwanzo 35:29 Genesis 35:29

Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika