Mwanzo 25 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 25 (Swahili) Genesis 25 (English)

Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura. Mwanzo 25:1

Abraham took another wife, and her name was Keturah.

Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua. Mwanzo 25:2

She bore him Zimran, Jokshan, Medan, Midian, Ishbak, and Shuah.

Yokshani akamzaa Sheba, na Dedani; na wana wa Dedani walikuwa Waashuri na Waletushi, na Waleumi. Mwanzo 25:3

Jokshan became the father of Sheba, and Dedan. The sons of Dedan were Asshurim, Letushim, and Leummim.

Na wana wa Midiani walikuwa, Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote walikuwa ni wana wa Ketura. Mwanzo 25:4

The sons of Midian: Ephah, Epher, Hanoch, Abida, and Eldaah. All these were the children of Keturah.

Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo. Mwanzo 25:5

Abraham gave all that he had to Isaac,

Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu. Mwanzo 25:6

but to the sons of the concubines who Abraham had, Abraham gave gifts. He sent them away from Isaac his son, while he yet lived, eastward, to the east country.

Hizi ndizo siku za miaka ya maisha ya Ibrahimu alizoishi, miaka mia, na sabini na mitano. Mwanzo 25:7

These are the days of the years of Abraham's life which he lived: one hundred seventy-five years.

Ibrahimu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake. Mwanzo 25:8

Abraham gave up the spirit, and died in a good old age, an old man, and full of years, and was gathered to his people.

Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni bin Sohari Mhiti, lielekealo Mamre. Mwanzo 25:9

Isaac and Ishmael, his sons, buried him in the cave of Machpelah, in the field of Ephron, the son of Zohar the Hittite, which is before Mamre,

Katika lile shamba alilolinunua Ibrahimu kwa wazawa Hethi, huko ndiko alikozikwa Ibrahimu na Sara mkewe. Mwanzo 25:10

the field which Abraham purchased of the children of Heth. There was Abraham buried, with Sarah his wife.

Ikawa, baada ya kufa kwake Ibrahimu, Mungu akambariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akakaa karibu ya Beer-lahai-roi. Mwanzo 25:11

It happened after the death of Abraham, that God blessed Isaac, his son. Isaac lived by Beer Lahai Roi.

Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli, mwana wa Ibrahimu, ambaye Hajiri, Mmisri, mjakazi wa Sara, alimzalia Ibrahimu. Mwanzo 25:12

Now this is the history of the generations of Ishmael, Abraham's son, whom Hagar the Egyptian, Sarah's handmaid, bore to Abraham.

Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu, Mwanzo 25:13

These are the names of the sons of Ishmael, by their names, according to the order of their birth: the firstborn of Ishmael, Nebaioth, then Kedar, Adbeel, Mibsam,

na Mishma, na Duma, na Masa, Mwanzo 25:14

Mishma, Dumah, Massa,

na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema. Mwanzo 25:15

Hadad, Tema, Jetur, Naphish, and Kedemah.

Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao. Mwanzo 25:16

These are the sons of Ishmael, and these are their names, by their villages, and by their encampments: twelve princes, according to their nations.

Na hii ndiyo miaka ya maisha ya Ishmaeli, miaka mia na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake. Mwanzo 25:17

These are the years of the life of Ishmael: one hundred thirty-seven years. He gave up the spirit and died, and was gathered to his people.

Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote. Mwanzo 25:18

They lived from Havilah to Shur that is before Egypt, as you go toward Assyria. He lived opposite all his relatives.

Na hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka. Mwanzo 25:19

This is the history of the generations of Isaac, Abraham's son. Abraham became the father of Isaac.

Isaka akawa mwenye miaka arobaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake. Mwanzo 25:20

Isaac was forty years old when he took Rebekah, the daughter of Bethuel the Syrian of Paddan Aram, the sister of Laban the Syrian, to be his wife.

Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba. Mwanzo 25:21

Isaac entreated Yahweh for his wife, because she was barren. Yahweh was entreated by him, and Rebekah his wife conceived.

Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana. Mwanzo 25:22

The children struggled together within her. She said, "If it be so, why do I live?" She went to inquire of Yahweh.

Bwana akamwambia,Mataifa mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo. Mwanzo 25:23

Yahweh said to her, Two nations are in your womb, Two peoples will be separated from your body. The one people will be stronger than the other people. The elder will serve the younger.

Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake. Mwanzo 25:24

When her days to be delivered were fulfilled, behold, there were twins in her womb.

Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. Mwanzo 25:25

The first came out red all over, like a hairy garment. They named him Esau.

Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa. Mwanzo 25:26

After that, his brother came out, and his hand had hold on Esau's heel. He was named Jacob. Isaac was sixty years old when she bore them.

Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani. Mwanzo 25:27

The boys grew. Esau was a skillful hunter, a man of the field. Jacob was a quiet man, living in tents.

Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo. Mwanzo 25:28

Now Isaac loved Esau, because he ate his venison. Rebekah loved Jacob.

Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. Mwanzo 25:29

Jacob boiled stew. Esau came in from the field, and he was famished.

Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu. Mwanzo 25:30

Esau said to Jacob, "Please feed me with that same red stew, for I am famished." Therefore his name was called Edom.

Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza. Mwanzo 25:31

Jacob said, "First, sell me your birthright."

Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? Mwanzo 25:32

Esau said, "Behold, I am about to die. What good is the birthright to me?"

Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Mwanzo 25:33

Jacob said, "Swear to me first." He swore to him. He sold his birthright to Jacob.

Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Mwanzo 25:34

Jacob gave Esau bread and stew of lentils. He ate and drank, rose up, and went his way. So Esau despised his birthright.