Mwanzo 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 5 (Swahili) Genesis 5 (English)

Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; Mwanzo 5:1

This is the book of the generations of Adam. In the day that God created man, he made him in God's likeness.

mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. Mwanzo 5:2

He created them male and female, and blessed them, and called their name Adam,{"Adam" and "Man" are spelled with the exact same consonants in Hebrew, so this can be correctly translated either way.} in the day when they were created.

Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. Mwanzo 5:3

Adam lived one hundred thirty years, and became the father of a son in his own likeness, after his image, and named him Seth.

Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:4

The days of Adam after he became the father of Seth were eight hundred years, and he became the father of sons and daughters.

Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa. Mwanzo 5:5

All the days that Adam lived were nine hundred thirty years, then he died.

Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi. Mwanzo 5:6

Seth lived one hundred five years, and became the father of Enosh.

Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:7

Seth lived after he became the father of Enosh eight hundred seven years, and became the father of sons and daughters.

Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa. Mwanzo 5:8

All the days of Seth were nine hundred twelve years, then he died.

Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani. Mwanzo 5:9

Enosh lived ninety years, and became the father of Kenan.

Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:10

Enosh lived after he became the father of Kenan, eight hundred fifteen years, and became the father of sons and daughters.

Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa. Mwanzo 5:11

All the days of Enosh were nine hundred five years, then he died.

Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. Mwanzo 5:12

Kenan lived seventy years, and became the father of Mahalalel.

Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:13

Kenan lived after he became the father of Mahalalel eight hundred forty years, and became the father of sons and daughters

Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa. Mwanzo 5:14

and all the days of Kenan were nine hundred ten years, then he died.

Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. Mwanzo 5:15

Mahalalel lived sixty-five years, and became the father of Jared.

Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:16

Mahalalel lived after he became the father of Jared eight hundred thirty years, and became the father of sons and daughters.

Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa. Mwanzo 5:17

All the days of Mahalalel were eight hundred ninety-five years, then he died.

Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. Mwanzo 5:18

Jared lived one hundred sixty-two years, and became the father of Enoch.

Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:19

Jared lived after he became the father of Enoch eight hundred years, and became the father of sons and daughters.

Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa. Mwanzo 5:20

All the days of Jared were nine hundred sixty-two years, then he died.

Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Mwanzo 5:21

Enoch lived sixty-five years, and became the father of Methuselah.

Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:22

Enoch walked with God after he became the father of Methuselah three hundred years, and became the father of sons and daughters.

Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Mwanzo 5:23

all the days of Enoch were three hundred sixty-five years.

Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. Mwanzo 5:24

Enoch walked with God, and he was not, for God took him.

Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki. Mwanzo 5:25

Methuselah lived one hundred eighty-seven years, and became the father of Lamech.

Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:26

Methuselah lived after he became the father of Lamech seven hundred eighty-two years, and became the father of sons and daughters.

Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa. Mwanzo 5:27

All the days of Methuselah were nine hundred sixty-nine years, then he died.

Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana. Mwanzo 5:28

Lamech lived one hundred eighty-two years, and became the father of a son,

Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana. Mwanzo 5:29

and he named him Noah, saying, "This same will comfort us in our work and in the toil of our hands, because of the ground which Yahweh has cursed."

Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake. Mwanzo 5:30

Lamech lived after he became the father of Noah five hundred ninety-five years, and became the father of sons and daughters.

Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa. Mwanzo 5:31

All the days of Lamech were seven hundred seventy-seven years, then he died.

Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi. Mwanzo 5:32

Noah was five hundred years old, and Noah became the father of Shem, Ham, and Japheth.