Mwanzo 49 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 49 (Swahili) Genesis 49 (English)

Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. Mwanzo 49:1

Jacob called to his sons, and said: "Gather yourselves together, that I may tell you that which will happen to you in the days to come.

Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu. Mwanzo 49:2

Assemble yourselves, and hear, you sons of Jacob; Listen to Israel, your father.

Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Mwanzo 49:3

"Reuben, you are my firstborn, my might, and the beginning of my strength; The pre-eminence of dignity, and the pre-eminence of power.

Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu. Mwanzo 49:4

Boiling over as water, you shall not have the pre-eminence; Because you went up to your father's bed; Then defiled it. He went up to my couch.

Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri. Mwanzo 49:5

"Simeon and Levi are brothers; Weapons of violence are their swords.

Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe; Mwanzo 49:6

My soul, don't come into their council; My glory, don't be united to their assembly; For in their anger they killed a man, In their self-will they hamstrung an ox.

Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli. Mwanzo 49:7

Cursed be their anger, for it was fierce; And their wrath, for it was cruel. I will divide them in Jacob, Scatter them in Israel.

Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Mwanzo 49:8

"Judah, your brothers will praise you: Your hand will be on the neck of your enemies; Your father's sons will bow down before you.

Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? Mwanzo 49:9

Judah is a lion's cub. From the prey, my son, you have gone up. He stooped down, he crouched as a lion, As a lioness. Who will rouse him up?

Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. Mwanzo 49:10

The scepter will not depart from Judah, Nor the ruler's staff from between his feet, Until he comes to whom it belongs. To him will the obedience of the peoples be.

Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu. Mwanzo 49:11

Binding his foal to the vine, His donkey's colt to the choice vine; He has washed his garments in wine, His robes in the blood of grapes:

Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. Mwanzo 49:12

His eyes will be red with wine, His teeth white with milk.

Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni. Mwanzo 49:13

"Zebulun will dwell at the haven of the sea. He will be for a haven of ships. His border will be on Sidon.

Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo; Mwanzo 49:14

"Issachar is a strong donkey, Lying down between the saddlebags.

Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu. Mwanzo 49:15

He saw a resting-place, that it was good, The land, that it was pleasant; He bows his shoulder to the burden, And becomes a servant doing forced labor.

Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli; Mwanzo 49:16

"Dan will judge his people, As one of the tribes of Israel.

Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali. Mwanzo 49:17

Dan will be a serpent in the way, An adder in the path, That bites the horse's heels, So that his rider falls backward.

Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana. Mwanzo 49:18

I have waited for your salvation, Yahweh.

Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino. Mwanzo 49:19

"Gad, a troop will press on him; But he will press on their heel.

Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme. Mwanzo 49:20

Out of Asher his bread will be fat, He will yield royal dainties.

Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri. Mwanzo 49:21

"Naphtali is a doe set free, Who bears beautiful fawns.

Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani. Mwanzo 49:22

"Joseph is a fruitful vine, A fruitful vine by a spring; His branches run over the wall.

Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Mwanzo 49:23

The archers have sorely grieved him, Shot at him, and persecute him:

Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli, Mwanzo 49:24

But his bow abode in strength, The arms of his hands were made strong, By the hands of the Mighty One of Jacob, (From there is the shepherd, the stone of Israel),

Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba. Mwanzo 49:25

Even by the God of your father, who will help you, By the Almighty, who will bless you, With blessings of heaven above, Blessings of the deep that lies below, Blessings of the breasts, and of the womb.

Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake. Mwanzo 49:26

The blessings of your father Have prevailed above the blessings of the ancient mountains, Above the bounty of the age-old hills. They will be on the head of Joseph, On the crown of the head of him who is separated from his brothers.

Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka. Mwanzo 49:27

"Benjamin is a ravenous wolf. In the morning he will devour the prey. At evening he will divide the spoil."

Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki. Mwanzo 49:28

All these are the twelve tribes of Israel, and this is what their father spoke to them and blessed them. He blessed everyone according to his blessing.

Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti; Mwanzo 49:29

He charged them, and said to them, "I am to be gathered to my people. Bury me with my fathers in the cave that is in the field of Ephron the Hittite,

katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia. Mwanzo 49:30

in the cave that is in the field of Machpelah, which is before Mamre, in the land of Canaan, which Abraham bought with the field from Ephron the Hittite as a burial place.

Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; Mwanzo 49:31

There they buried Abraham and Sarah, his wife. There they buried Isaac and Rebekah, his wife, and there I buried Leah:

shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi. Mwanzo 49:32

the field and the cave that is therein, which was purchased from the children of Heth."

Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.

Mwanzo 49:33

When Jacob made an end of charging his sons, he gathered up his feet into the bed, and yielded up the spirit, and was gathered to his people.