Mwanzo 31 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 31 (Swahili) Genesis 31 (English)

Basi Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema, Yakobo amechukua mali yote ya baba yetu; na kwa mali ya baba yetu amepata fahari hii yote. Mwanzo 31:1

He heard the words of Laban's sons, saying, "Jacob has taken away all that was our father's. From that which was our father's, has he gotten all this wealth."

Yakobo akaona uso wa Labani, ya kuwa hakumtazama vema kama jana na juzi. Mwanzo 31:2

Jacob saw the expression on Laban's face, and, behold, it was not toward him as before.

Bwana akamwambia Yakobo, Urudi mpaka nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami nitakuwa pamoja nawe. Mwanzo 31:3

Yahweh said to Jacob, "Return to the land of your fathers, and to your relatives, and I will be with you."

Yakobo akatuma watu, akawaita Raheli na Lea waje nyikani kwenye wanyama wake. Akawaambia, Mwanzo 31:4

Jacob sent and called Rachel and Leah to the field to his flock,

Naona uso wa baba yenu, kwamba hanitazami vema kama jana na juzi. Lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami. Mwanzo 31:5

and said to them, "I see the expression on your father's face, that it is not toward me as before; but the God of my father has been with me.

Nanyi mmejua ya kwamba kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu. Mwanzo 31:6

You know that I have served your father with all of my strength.

Na baba yenu amenidanganya, akabadili mshahara wangu mara kumi; lakini Mungu hakumwacha kunidhuru. Mwanzo 31:7

Your father has deceived me, and changed my wages ten times, but God didn't allow him to hurt me.

Aliposema, Walio na madoadoa watakuwa mshahara wako, wanyama wote wakazaa madoadoa. Aliposema, Walio na milia watakuwa mshahara wako, ndipo wanyama wote wakazaa wenye milia. Mwanzo 31:8

If he said this, 'The speckled will be your wages,' then all the flock bore speckled. If he said this, 'The streaked will be your wages,' then all the flock bore streaked.

Hivi Mungu akamnyang'anya mali yake baba yenu, na kunipa mimi. Mwanzo 31:9

Thus God has taken away the cattle of your father, and given them to me.

Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba, naliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka. Mwanzo 31:10

It happened at the time that the flock conceive, that I lifted up my eyes, and saw in a dream, and behold, the male goats which leaped on the flock were streaked, speckled, and grizzled.

Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Mwanzo 31:11

The angel of God said to me in the dream, 'Jacob,' and I said, 'Here I am.'

Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. Mwanzo 31:12

He said, 'Now lift up your eyes, and behold, all the male goats which leap on the flock are streaked, speckled, and grizzled, for I have seen all that Laban does to you.

Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa. Mwanzo 31:13

I am the God of Bethel, where you anointed a pillar, where you vowed a vow to me. Now arise, get out from this land, and return to the land of your birth."

Raheli na Lea wakajibu, wakamwambia, Je! Imetubakia sehemu au urithi katika nyumba ya baba yetu? Mwanzo 31:14

Rachel and Leah answered him, "Is there yet any portion or inheritance for us in our father's house?

Hakutufanya kama wageni, maana ametuuza, naye amekula fedha zetu kabisa? Mwanzo 31:15

Aren't we accounted by him as foreigners? For he has sold us, and has also quite devoured our money.

Maana mali yote ambayo Mungu amemnyang'anya baba yetu, mali hiyo ndiyo yetu na ya wana wetu. Basi yo yote Mungu aliyokuambia, uyafanye. Mwanzo 31:16

For all the riches which God has taken away from our father, that is ours and our children's. Now then, whatever God has said to you, do."

Ndipo Yakobo akaondoka, akapandisha wanawe na wakeze juu ya ngamia. Mwanzo 31:17

Then Jacob rose up, and set his sons and his wives on the camels,

Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani. Mwanzo 31:18

and he carried away all his cattle, and all his substance which he had gathered, the cattle of his getting, which he had gathered in Paddan Aram, to go to Isaac his father to the land of Canaan.

Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye. Mwanzo 31:19

Now Laban had gone to shear his sheep: and Rachel stole the teraphim{teraphim were household idols that may have been associated with inheritance rights to the household property.} that were her father's.

Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia. Mwanzo 31:20

Jacob deceived Laban the Syrian, in that he didn't tell him that he was running away.

Basi akakimbia yeye na yote aliyokuwa nayo; akaondoka akauvuka mto, akaelekeza uso wake kwenda mlima wa Gileadi. Mwanzo 31:21

So he fled with all that he had. He rose up, passed over the River, and set his face toward the mountain of Gilead.

Hata siku ya tatu Labani akaambiwa ya kwamba Yakobo amekimbia, Mwanzo 31:22

Laban was told on the third day that Jacob had fled.

akatwaa ndugu zake pamoja naye, akamfuata mwendo wa siku saba. Akampata katika mlima wa Gileadi. Mwanzo 31:23

He took his relatives with him, and pursued after him seven days' journey. He overtook him in the mountain of Gilead.

Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari. Mwanzo 31:24

God came to Laban, the Syrian, in a dream of the night, and said to him, "Take heed to yourself that you don't speak to Jacob either good or bad."

Labani akamfikia Yakobo, na Yakobo alikuwa amepiga hema zake katika mlima, na Labani na ndugu zake wakapiga hema zao katika mlima wa Gileadi. Mwanzo 31:25

Laban caught up with Jacob. Now Jacob had pitched his tent in the mountain, and Laban with his relatives encamped in the mountain of Gilead.

Labani akamwambia Yakobo, Umefanya nini? Umenihadaa, ukawachukua binti zangu kama mateka waliotwaliwa kwa upanga. Mwanzo 31:26

Laban said to Jacob, "What have you done, that you have deceived me, and carried away my daughters like captives of the sword?

Mbona umekimbia kwa siri ukanihadaa, wala hukuniambia, nipate kuagana nawe uende zako kwa furaha, na nyimbo, na ngoma, na kinubi? Mwanzo 31:27

Why did you flee secretly, and deceive me, and didn't tell me, that I might have sent you away with mirth and with songs, with tambourine and with harp;

Wala hukuniacha niwabusu wanangu, na binti zangu; basi umetenda upumbavu. Mwanzo 31:28

and didn't allow me to kiss my sons and my daughters? Now have you done foolishly.

Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari. Mwanzo 31:29

It is in the power of my hand to hurt you, but the God of your father spoke to me last night, saying, 'Take heed to yourself that you don't speak to Jacob either good or bad.'

Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu? Mwanzo 31:30

Now, you want to be gone, because you sore longed after your father's house, but why have you stolen my gods?"

Yakobo akajibu, akamwambia Labani, Kwa sababu naliogopa, nikasema, Usije ukaninyang'anya binti zako kwa nguvu. Mwanzo 31:31

Jacob answered Laban, "Because I was afraid, for I said, 'Lest you should take your daughters from me by force.'

Awaye yote utakayemwona kuwa nayo miungu yako, yeye asiishi. Mbele ya ndugu zetu ukitambue kilicho chako kwangu, ukakichukue. Maana Yakobo hakujua ya kwamba Raheli ameiiba. Mwanzo 31:32

With whoever you find your gods, he shall not live. Before our relatives, discern what is yours with me, and take it." For Jacob didn't know that Rachel had stolen them.

Labani akaingia katika hema ya Yakobo, na hema ya Lea, na hema ya vijakazi wawili, wala hakuiona. Akatoka katika hema ya Lea, akaingia katika hema ya Raheli. Mwanzo 31:33

Laban went into Jacob's tent, into Leah's tent, and into the tent of the two maid-servants; but he didn't find them. He went out of Leah's tent, and entered into Rachel's tent.

Basi Raheli alikuwa amevitwaa vile vinyago ameviweka katika matandiko ya ngamia, na kuvikalia. Labani akapapasa hema yote wala hakuviona. Mwanzo 31:34

Now Rachel had taken the teraphim, put them in the camel's saddle, and sat on them. Laban felt about all the tent, but didn't find them.

Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago. Mwanzo 31:35

She said to her father, "Don't let my lord be angry that I can't rise up before you; for the manner of women is on me." He searched, but didn't find the teraphim.

Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N'nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii? Mwanzo 31:36

Jacob was angry, and argued with Laban. Jacob answered Laban, "What is my trespass? What is my sin, that you have hotly pursued after me?

Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu. Mwanzo 31:37

Now that you have felt around in all my stuff, what have you found of all your household stuff? Set it here before my relatives and your relatives, that they may judge between us two.

Miaka hii ishirini nimekaa kwako; kondoo zako wala mbuzi zako wake hawakuharibu mimba wala waume katika wanyama wako sikuwala. Mwanzo 31:38

These twenty years have I been with you. Your ewes and your female goats have not cast their young, and I haven't eaten the rams of your flocks.

Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku. Mwanzo 31:39

That which was torn of animals, I didn't bring to you. I bore the loss of it. Of my hand you required it, whether stolen by day or stolen by night.

Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu. Mwanzo 31:40

Thus I was; in the day the drought consumed me, and the frost by night; and my sleep fled from my eyes.

Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi. Mwanzo 31:41

These twenty years have I been in your house. I served you fourteen years for your two daughters, and six years for your flock, and you have changed my wages ten times.

Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu. Mwanzo 31:42

Unless the God of my father, the God of Abraham, and the fear of Isaac, had been with me, surely now you would have sent me away empty. God has seen my affliction and the labor of my hands, and rebuked you last night."

Labani akajibu, akamwambia Yakobo, Hao binti ni binti zangu, na wana ni wanangu, na wanyama ni wanyama wangu, na yote uyaonayo ni yangu; nami naweza kuwatendea nini leo binti zangu na wana wao waliowalea? Mwanzo 31:43

Laban answered Jacob, "The daughters are my daughters, the children are my children, the flocks are my flocks, and all that you see is mine: and what can I do this day to these my daughters, or to their children whom they have borne?

Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe. Mwanzo 31:44

Now come, let us make a covenant, you and I; and let it be for a witness between me and you."

Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo. Mwanzo 31:45

Jacob took a stone, and set it up for a pillar.

Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu. Mwanzo 31:46

Jacob said to his relatives, "Gather stones." They took stones, and made a heap. They ate there by the heap.

Labani aliiita Yegarsahadutha, lakini Yakobo aliiita Galedi. Mwanzo 31:47

Laban called it Jegar Sahadutha,{"Jegar Sahadutha" means "Witness Heap" in Aramaic.} but Jacob called it Galeed.{"Galeed" means "Witness Heap" in Hebrew.}

Labani akasema, Chungu hii ni shahidi kati ya mimi na wewe hivi leo. Kwa hiyo likaitwa jina lake Galedi, Mwanzo 31:48

Laban said, "This heap is witness between me and you this day." Therefore it was named Galeed

na Mispa, maana alisema, Mungu avizie kati ya mimi na wewe, wakati tusipoonana. Mwanzo 31:49

and Mizpah, for he said, "Yahweh watch between me and you, when we are absent one from another.

Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe. Mwanzo 31:50

If you will afflict my daughters, and if you will take wives besides my daughters, no man is with us; behold, God is witness between me and you."

Labani akamwambia Yakobo, Tazama chungu hii utazame na nguzo niliyoitia kati ya mimi na wewe. Mwanzo 31:51

Laban said to Jacob, "See this heap, and see the pillar, which I have set between me and you.

Chungu hii na iwe shahidi, na nguzo hii na iwe shahidi, ya kuwa mimi sitapita chungu hii kuja kwako, wala wewe hutapita chungu hii na nguzo hii uje kwangu, kwa madhara. Mwanzo 31:52

May this heap be a witness, and the pillar be a witness, that I will not pass over this heap to you, and that you will not pass over this heap and this pillar to me, for harm.

Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu. Mwanzo 31:53

The God of Abraham, and the God of Nahor, the God of their father, judge between us." Then Jacob swore by the fear of his father, Isaac.

Yakobo akachinja sadaka katika mlima, akawaita ndugu zake waje wale chakula, nao wakala chakula, wakakaa usiku kucha mlimani. Mwanzo 31:54

Jacob offered a sacrifice in the mountain, and called his relatives to eat bread. They ate bread, and stayed all night in the mountain.

Labani akaondoka asubuhi na mapema, akawabusu wanawe na binti zake, akawabariki; kisha Labani akaenda zake, akarudi kwao. Mwanzo 31:55

Early in the morning, Laban rose up, and kissed his sons and his daughters, and blessed them. Laban departed and returned to his place.