Mwanzo Mlango 39 Genesis

Mwanzo 39:1 Genesis 39:1

Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko.

Mwanzo 39:2 Genesis 39:2

Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.

Mwanzo 39:3 Genesis 39:3

Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.

Mwanzo 39:4 Genesis 39:4

Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.

Mwanzo 39:5 Genesis 39:5

Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.

Mwanzo 39:6 Genesis 39:6

Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.

Mwanzo 39:7 Genesis 39:7

Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.

Mwanzo 39:8 Genesis 39:8

Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.

Mwanzo 39:9 Genesis 39:9

Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?

Mwanzo 39:10 Genesis 39:10

Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.

Mwanzo 39:11 Genesis 39:11

Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;

Mwanzo 39:12 Genesis 39:12

huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.

Mwanzo 39:13 Genesis 39:13

Ikawa alipoona ya kwamba amemwachilia nguo yake mkononi mwake, naye amekimbia nje,

Mwanzo 39:14 Genesis 39:14

akawaita watu wa nyumbani mwake, akasema nao, akinena, Angalieni, ametuletea mtu Mwebrania atufanyie dhihaka. Ameingia kwangu, ili alale nami, nikalia kwa sauti kuu.

Mwanzo 39:15 Genesis 39:15

Ikawa, aliposikia ya kuwa nimepaza sauti yangu na kulia, aliiacha nguo yake kwangu, akakimbia, akatoka nje.

Mwanzo 39:16 Genesis 39:16

Basi akaiweka ile nguo kwake hata bwana wake aje nyumbani.

Mwanzo 39:17 Genesis 39:17

Naye akamwambia kama maneno hayo, akisema, Yule mtumwa Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kwangu anidhihaki.

Mwanzo 39:18 Genesis 39:18

Ikawa nilipopaza sauti yangu, nikalia, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje.

Mwanzo 39:19 Genesis 39:19

Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo kama haya, hasira yake ikawaka.

Mwanzo 39:20 Genesis 39:20

Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa wafungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani.

Mwanzo 39:21 Genesis 39:21

Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.

Mwanzo 39:22 Genesis 39:22

Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya.

Mwanzo 39:23 Genesis 39:23

Wala mkuu wa gereza hakuangalia neno lililoko mkononi mwa Yusufu; kwa kuwa Bwana alikuwa pamoja naye. Bwana akayafanikisha yote aliyoyafanya.