Mwanzo 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 8 (Swahili) Genesis 8 (English)

Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua; Mwanzo 8:1

God remembered Noah, all the animals, and all the cattle that were with him in the ark; and God made a wind to pass over the earth. The waters subsided.

chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa; Mwanzo 8:2

The deep's fountains and the sky's windows were also stopped, and the rain from the sky was restrained.

maji yakadumu kuondoka katika nchi; na mwisho wa siku mia na hamsini maji yakapunguka. Mwanzo 8:3

The waters receded from off the earth continually. After the end of one hundred fifty days the waters decreased.

Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati. Mwanzo 8:4

The ark rested in the seventh month, on the seventeenth day of the month, on Ararat's mountains.

Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana. Mwanzo 8:5

The waters receded continually until the tenth month. In the tenth month, on the first day of the month, the tops of the mountains were seen.

Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; Mwanzo 8:6

It happened at the end of forty days, that Noah opened the window of the ark which he had made,

akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. Mwanzo 8:7

and he sent forth a raven. It went back and forth, until the waters were dried up from off the earth.

Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; Mwanzo 8:8

He sent forth a dove from him, to see if the waters were abated from off the surface of the ground,

bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani. Mwanzo 8:9

but the dove found no place to rest her foot, and she returned to him into the ark; for the waters were on the surface of the whole earth. He put forth his hand, and took her, and brought her to him into the ark.

Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili, Mwanzo 8:10

He stayed yet another seven days; and again he sent forth the dove out of the ark.

njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. Mwanzo 8:11

The dove came back to him at evening, and, behold, in her mouth was an olive leaf plucked off. So Noah knew that the waters were abated from off the earth.

Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe. Mwanzo 8:12

He stayed yet another seven days, and sent forth the dove; and she didn't return to him any more.

Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka. Mwanzo 8:13

It happened in the six hundred first year, in the first month, the first day of the month, the waters were dried up from off the earth. Noah removed the covering of the ark, and looked. He saw that the surface of the ground was dried.

Na mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa kavu. Mwanzo 8:14

In the second month, on the twenty-seventh day of the month, the earth was dry.

Mungu akamwambia Nuhu, akisema, Mwanzo 8:15

God spoke to Noah, saying,

Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. Mwanzo 8:16

"Go forth from the ark, you, and your wife, and your sons, and your sons' wives with you.

Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi. Mwanzo 8:17

Bring forth with you every living thing that is with you of all flesh, including birds, cattle, and every creeping thing that creeps on the earth; that they may breed abundantly in the earth, and be fruitful, and multiply on the earth."

Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; Mwanzo 8:18

Noah went forth, with his sons, his wife, and his sons' wives with him.

kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina. Mwanzo 8:19

Every animal, every creeping thing, and every bird, whatever moves on the earth, after their families, went forth out of the ark.

Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Mwanzo 8:20

Noah built an altar to Yahweh, and took of every clean animal, and of every clean bird, and offered burnt offerings on the altar.

Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. Mwanzo 8:21

Yahweh smelled the sweet savor. Yahweh said in his heart, "I will not again curse the ground any more for man's sake, because the imagination of man's heart is evil from his youth; neither will I ever again strike everything living, as I have done.

Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.

Mwanzo 8:22

While the earth remains, seed time and harvest, and cold and heat, and summer and winter, and day and night shall not cease."