1
Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;
But God remembered Noah and all the animals and livestock that were with him in the ark. And God sent a wind over the earth, and the waters began to subside.
2
chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa;
The springs of the deep and the floodgates of the heavens were closed, and the rain from the sky was restrained.
3
maji yakadumu kuondoka katika nchi; na mwisho wa siku mia na hamsini maji yakapunguka.
The waters receded steadily from the earth, and after 150 days the waters had gone down.
4
Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati.
On the seventeenth day of the seventh month, the ark came to rest on the mountains of Ararat.
5
Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
And the waters continued to recede until the tenth month, and on the first day of the tenth month the tops of the mountains became visible.
6
Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya;
After forty days Noah opened the window he had made in the ark
7
akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi.
and sent out a raven. It kept flying back and forth until the waters had dried up from the earth.
8
Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi;
Then Noah sent out a dove to see if the waters had receded from the surface of the ground.
9
bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.
But the dove found no place to rest her foot, and she returned to him in the ark, because the waters were still covering the surface of all the earth. So he reached out his hand and brought her back inside the ark.
10
Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili,
Noah waited seven more days and again sent out the dove from the ark.
11
njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
And behold, the dove returned to him in the evening with a freshly plucked olive leaf in her beak. So Noah knew that the waters had receded from the earth.
12
Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.
And Noah waited seven more days and sent out the dove again, but this time she did not return to him.
13
Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka.
In Noah’s six hundred and first year, on the first day of the first month, the waters had dried up from the earth. So Noah removed the covering from the ark and saw that the surface of the ground was dry.
14
Na mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa kavu.
By the twenty-seventh day of the second month, the earth was fully dry.
15
Mungu akamwambia Nuhu, akisema,
Then God said to Noah,
16
Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe.
“Come out of the ark, you and your wife, along with your sons and their wives.
17
Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
Bring out all the living creatures that are with you—birds, livestock, and everything that crawls upon the ground—so that they can spread out over the earth and be fruitful and multiply upon it.”
18
Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye;
So Noah came out, along with his sons and his wife and his sons’ wives.
19
kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina.
Every living creature, every creeping thing, and every bird—everything that moves upon the earth—came out of the ark, kind by kind.
20
Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Then Noah built an altar to the LORD. And taking from every kind of clean animal and clean bird, he offered burnt offerings on the altar.
21
Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.
When the LORD smelled the pleasing aroma, He said in His heart, “Never again will I curse the ground because of man, even though every inclination of his heart is evil from his youth. And never again will I destroy all living creatures as I have done.
22
Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma. </p>
As long as the earth endures, seedtime and harvest, cold and heat, summer and winter, day and night shall never cease.”