Mwanzo 42 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 42 (Swahili) Genesis 42 (English)

Basi Yakobo akaona ya kuwa kuna nafaka katika Misri, Yakobo akawaambia wanawe, Kwa nini mnatazamana? Mwanzo 42:1

Now Jacob saw that there was grain in Egypt, and Jacob said to his sons, "Why do you look at one another?"

Akasema, Angalia, nimesikia ya kuwa kuna nafaka Misri; shukeni huko mkatununulie chakula, tupate kuishi wala tusife. Mwanzo 42:2

He said, "Behold, I have heard that there is grain in Egypt. Go down there, and buy for us from there, so that we may live, and not die."

Basi ndugu kumi wa Yusufu wakashuka Misri ili wanunue nafaka. Mwanzo 42:3

Joseph's ten brothers went down to buy grain from Egypt.

Walakini Benyamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumpeleka pamoja na ndugu zake, maana alisema, Mabaya yasimpate. Mwanzo 42:4

But Jacob didn't send Benjamin, Joseph's brother, with his brothers; for he said, "Lest perhaps harm happen to him."

Wana wa Israeli wakaja wanunue chakula miongoni mwao waliokuja, kwa kuwa kulikuwa na njaa katika nchi ya Kanaani. Mwanzo 42:5

The sons of Israel came to buy among those who came, for the famine was in the land of Canaan.

Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake. Mwanzo 42:6

Joseph was the governor over the land. It was he who sold to all the people of the land. Joseph's brothers came, and bowed themselves down to him with their faces to the earth.

Yusufu akawaona nduguze, akawatambua, lakini alijifanya kama mgeni kwao. Akasema nao kwa maneno makali, akawaambia, Mmetoka wapi ninyi? Wakasema. Tumetoka nchi ya Kanaani, ili tununue chakula. Mwanzo 42:7

Joseph saw his brothers, and he recognized them, but acted like a stranger to them, and spoke roughly with them. He said to them, "Where did you come from?" They said, "From the land of Canaan to buy food."

Yusufu akawatambua nduguze, bali wao hawakumtambua yeye. Mwanzo 42:8

Joseph recognized his brothers, but they didn't recognize him.

Yusufu akazikumbuka zile ndoto alizowaotea. Akawaambia, Wapelelezi ninyi, mmekuja ili mwuone utupu wa nchi. Mwanzo 42:9

Joseph remembered the dreams which he dreamed about them, and said to them, "You are spies! You have come to see the nakedness of the land."

Wakamwambia, Hasha, bwana, watumwa wako tumekuja ili tununue chakula. Mwanzo 42:10

They said to him, "No, my lord, but your servants have come to buy food.

Sisi sote ni wana wa mtu mmoja tu watu wa kweli sisi; watumwa wako si wapelelezi. Mwanzo 42:11

We are all one man's sons; we are honest men. Your servants are not spies."

Akawaambia, Sivyo, mmekuja ili mwuone utupu wa nchi. Mwanzo 42:12

He said to them, "No, but you have come to see the nakedness of the land."

Wakamwambia, Sisi watumwa wako tu ndugu kumi na wawili, wana wa mtu mmoja katika nchi ya Kanaani; na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo, na mmoja hayuko. Mwanzo 42:13

They said, "We, your servants, are twelve brothers, the sons of one man in the land of Canaan; and, behold, the youngest is this day with our father, and one is no more."

Yusufu akawaambia, Ndivyo nilivyowaambia, nikisema, Wapelelezi ninyi. Mwanzo 42:14

Joseph said to them, "It is like I told you, saying, 'You are spies.'

Mtabainika kwa njia hii; aishivyo Farao, hamtoki hapa, asipokuja huku huyo ndugu yenu mdogo. Mwanzo 42:15

Hereby you shall be tested. By the life of Pharaoh you shall not go forth from here, unless your youngest brother come here.

Mpelekeni mmoja wenu, aende akamlete ndugu yenu, na ninyi mtafungwa, hata maneno yenu yahakikishwe, kama mna kweli ninyi; ikiwa sivyo, aishivyo Farao, ninyi ni wapelelezi. Mwanzo 42:16

Send one of you, and let him get your brother, and you shall be bound, that your words may be tested, whether there is truth in you, or else by the life of Pharaoh surely you are spies."

Akawatia wote gerezani siku tatu. Mwanzo 42:17

He put them all together into custody three days.

Yusufu akawaambia siku ya tatu, Fanyeni hivi, mkaishi, maana mimi namcha Mungu. Mwanzo 42:18

Joseph said to them the third day, "Do this, and live, for I fear God.

Kama ni wa kweli ninyi ndugu yenu mmoja na afungwe gerezani, nanyi nendeni mkachukue nafaka kwa njaa ya nyumba zenu, Mwanzo 42:19

If you are honest men, then let one of your brothers be bound in your prison-house; but you go, carry grain for the famine of your houses.

mkamlete ndugu yenu mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala hamtakufa. Ndivyo walivyofanya. Mwanzo 42:20

Bring your youngest brother to me; so will your words be verified, and you won't die." They did so.

Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosa ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia kwa hiyo shida hii imetupata. Mwanzo 42:21

They said one to another, "We are most assuredly guilty concerning our brother, in that we saw the distress of his soul, when he begged us, and we wouldn't listen. Therefore this distress has come on us."

Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, msimkose kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo damu yake inatakwa tena. Mwanzo 42:22

Reuben answered them, saying, "Didn't I tell you, saying, 'Don't sin against the child,' and you wouldn't listen? Therefore also, behold, his blood is required."

Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alikuwapo mkalimani kati yao. Mwanzo 42:23

They didn't know that Joseph understood them; for there was an interpreter between them.

Akajitenga nao akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao. Mwanzo 42:24

He turned himself about from them, and wept, and he returned to them, and spoke to them, and took Simeon from among them, and bound him before their eyes.

Yusufu akaamuru kuvijaza vyombo vyao nafaka, na kumrudishia kila mtu fedha yake katika gunia lake, na kuwapa chakula cha njiani. Mwanzo 42:25

Then Joseph commanded to fill their bags with grain, and to restore every man's money into his sack, and to give them food for the way. So it done to them.

Navyo ndivyo walivyofanyiwa. Wakaweka nafaka yao juu ya punda zao, wakatoka huko. Mwanzo 42:26

They loaded their donkeys with their grain, and departed from there.

Mmoja wao alipofungua gunia lake ili ampe punda wake chakula katika nyumba ya wageni, aliiona fedha yake; kumbe! Iko kinywani mwa gunia lake. Mwanzo 42:27

As one of them opened his sack to give his donkey food in the lodging-place, he saw his money. Behold, it was in the mouth of his sack.

Akawaambia nduguze, Fedha yangu imerudishwa, angalia, imo humo guniani mwangu. Mioyo yao ikazimia, wakageukiana wakitetemeka, wakasema, N'nini hii Mungu aliyotutendea? Mwanzo 42:28

He said to his brothers, "My money is restored! Behold, it is even in my sack." Their hearts failed them, and they turned trembling one to another, saying, "What is this that God has done to us?"

Wakaja kwa Yakobo, baba yao, katika nchi ya Kanaani, wakampasha habari za yote yaliyowapata, wakisema, Mwanzo 42:29

They came to Jacob their father to the land of Canaan, and told him all that had happened to them, saying,

Mtu yule aliye bwana wa nchi alisema nasi kwa maneno makali, akatufanya tu wapelelezi wa nchi. Mwanzo 42:30

"The man, the lord of the land, spoke roughly with us, and took us for spies of the country.

Tukamwambia, Tu watu wa kweli sisi, wala si wapelelezi. Mwanzo 42:31

We said to him, 'We are honest men. We are no spies.

Sisi tu ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu. Mmoja hayuko, na mdogo wetu yuko pamoja na baba yetu leo katika nchi ya Kanaani. Mwanzo 42:32

We are twelve brothers, sons of our father; one is no more, and the youngest is this day with our father in the land of Canaan.'

Yule mtu, bwana wa nchi, akatuambia, Kwa njia hii nitawajua kama ninyi ni watu wa kweli; ndugu yenu mmoja mwacheni huku kwangu, kachukueni nafaka kwa njaa ya nyumba zenu, mwende zenu. Mwanzo 42:33

The man, the lord of the land, said to us, 'Hereby will I know that you are honest men. Leave one of your brothers with me, and take grain for the famine of your houses, and go your way.

Mkaniletee ndugu yenu mdogo; ndipo nitakapojua kama ninyi si wapelelezi, bali ni watu wa kweli; basi nitawarudishia ndugu yenu, nanyi mtafanya biashara katika nchi hii. Mwanzo 42:34

Bring your youngest brother to me. Then I will know that you are not spies, but that you are honest men. So I will deliver your brother to you, and you shall trade in the land.'"

Ikawa walipomimina magunia yao, kumbe! Bahasha ya fedha ya kila mtu imo katika gunia lake. Nao walipoziona bahasha za fedha zao, wao na baba yao waliogopa. Mwanzo 42:35

It happened as they emptied their sacks, that behold, every man's bundle of money was in his sack. When they and their father saw their bundles of money, they were afraid.

Yakobo baba yao akawaambia, Mmeniondolea watoto wangu; Yusufu hayuko, wala Simeoni hayuko, na Benyamini mnataka kumchukua naye; mambo hayo yote yamenipata mimi. Mwanzo 42:36

Jacob, their father, said to them, "You have bereaved me of my children! Joseph is no more, Simeon is no more, and you want to take Benjamin away. All these things are against me."

Reubeni akamwambia babaye, akasema, Uwaue wanangu wawili nisipomrudisha kwako; mtie katika mikono yangu, nami nitamrudisha kwako. Mwanzo 42:37

Reuben spoke to his father, saying, "Kill my two sons, if I don't bring him to you. Deliver him into my hand, and I will bring him to you again."

Akasema, Mwanangu hatashuka pamoja nanyi, maana nduguye amekufa, naye amesalia peke yake; mabaya yakimpata katika njia mtakayoiendea ndipo mtakaposhusha mvi zangu kwa sikitiko mpaka kaburini.

Mwanzo 42:38

He said, "My son shall not go down with you; for his brother is dead, and he only is left. If harm happens to him by the way in which you go, then you will bring down my gray hairs with sorrow to Sheol."