Mwanzo 34 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 34 (Swahili) Genesis 34 (English)

Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi. Mwanzo 34:1

Dinah, the daughter of Leah, whom she bore to Jacob, went out to see the daughters of the land.

Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri. Mwanzo 34:2

Shechem the son of Hamor the Hivite, the prince of the land, saw her. He took her, lay with her, and humbled her.

Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri. Mwanzo 34:3

His soul joined to Dinah, the daughter of Jacob, and he loved the young lady, and spoke kindly to the young lady.

Shekemu akamwambia Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu. Mwanzo 34:4

Shechem spoke to his father, Hamor, saying, "Get me this young lady as a wife."

Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja. Mwanzo 34:5

Now Jacob heard that he had defiled Dinah, his daughter; and his sons were with his cattle in the field. Jacob held his peace until they came.

Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye. Mwanzo 34:6

Hamor the father of Shechem went out to Jacob to talk with him.

Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka. Mwanzo 34:7

The sons of Jacob came in from the field when they heard it. The men were grieved, and they were very angry, because he had done folly in Israel in lying with Jacob's daughter; which thing ought not to be done.

Hamori akasema nao, akinena, Roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe. Mwanzo 34:8

Hamor talked with them, saying, "The soul of my son, Shechem, longs for your daughter. Please give her to him as a wife.

Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu. Mwanzo 34:9

Make marriages with us. Give your daughters to us, and take our daughters for yourselves.

Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo. Mwanzo 34:10

You shall dwell with us: and the land will be before you. Live and trade in it, and get possessions in it."

Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa. Mwanzo 34:11

Shechem said to her father and to her brothers, "Let me find favor in your eyes, and whatever you will tell me I will give.

Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu. Mwanzo 34:12

Ask me a great amount for a dowry, and I will give whatever you ask of me, but give me the young lady as a wife."

Wana wa Yakobo wakawajibu Shekemu na Hamori babaye, kwa hila, maana amemharibu Dina, umbu lao, Mwanzo 34:13

The sons of Jacob answered Shechem and Hamor his father with deceit, and spoke, because he had defiled Dinah their sister,

wakawaambia, Hatuwezi kufanya neno hili, tumpe umbu letu mtu asiyetahiriwa; ingekuwa aibu kwetu. Mwanzo 34:14

and said to them, "We can't do this thing, to give our sister to one who is uncircumcised; for that is a reproach to us.

Lakini kwa sharti hii tu tutapatana nanyi; mkiwa kama sisi, akitahiriwa kila mwanamume wenu, Mwanzo 34:15

Only on this condition will we consent to you. If you will be as we are, that every male of you be circumcised;

ndipo tutawapa ninyi binti yetu, na sisi tutatwaa binti zenu tutakaa pamoja nanyi, nasi tutakuwa watu wamoja. Mwanzo 34:16

then will we give our daughters to you, and we will take your daughters to us, and we will dwell with you, and we will become one people.

Lakini kama hamtusikii na kutahiriwa, basi tutamtwaa umbu letu, nasi tutakwenda zetu. Mwanzo 34:17

But if you will not listen to us, to be circumcised, then we will take our sister,{Hebrew has, literally, "daughter"} and we will be gone."

Maneno yao yakawa mema machoni pa Hamori, na machoni pa Shekemu, mwana wa Hamori. Mwanzo 34:18

Their words pleased Hamor, and Shechem, Hamor's son.

Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani mwa babaye. Mwanzo 34:19

The young man didn't wait to do this thing, because he had delight in Jacob's daughter, and he was honored above all the house of his father.

Hamori, na Shekemu mwanawe, wakaja langoni pa mji wao, wakasema na watu wa mji wao, wakinena, Mwanzo 34:20

Hamor and Shechem, his son, came to the gate of their city, and talked with the men of their city, saying,

Watu hawa wana amani nasi, basi na wakae katika nchi, na kufanya biashara humo; kwa maana nchi ni kubwa, yawatosha; na tuwatwae binti zao kuwa wake zetu, na binti zetu tuwape wao. Mwanzo 34:21

"These men are peaceful with us. Therefore let them live in the land and trade in it. For, behold, the land is large enough for them. Let us take their daughters to us for wives, and let us give them our daughters.

Lakini kwa sharti hiyo moja tu watapatana nasi wakae wote kwetu, tuwe watu wamoja, kama tukitahiriwa kila mwanamume, kama hawa walivyotahiriwa. Mwanzo 34:22

Only on this condition will the men consent to us to dwell with us, to become one people, if every male among us be circumcised, as they are circumcised.

Je! Kondoo zao, na mali zao, na wanyama wao wote hawatakuwa mali zetu? Basi na tupatane nao tu, nao watakaa kwetu. Mwanzo 34:23

Won't their cattle and their substance and all their animals be ours? Only let us give our consent to them, and they will dwell with us."

Wakawasikia Hamori na Shekemu mwanawe, wote watokao katika lango la mji wake. Wakatahiriwa kila mwanamume, wote watokao katika lango la mji wake. Mwanzo 34:24

All who went out of the gate of his city listened to Hamor, and to Shechem his son; and every male was circumcised, all who went out of the gate of his city.

Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua waume wote. Mwanzo 34:25

It happened on the third day, when they were sore, that two of Jacob's sons, Simeon and Levi, Dinah's brothers, each took his sword, came upon the unsuspecting city, and killed all the males.

Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka. Mwanzo 34:26

They killed Hamor and Shechem, his son, with the edge of the sword, and took Dinah out of Shechem's house, and went away.

Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao. Mwanzo 34:27

Jacob's sons came on the dead, and plundered the city, because they had defiled their sister.

Wakachukua kondoo zao, na ng'ombe zao, na punda zao, na vitu vilivyokuwamo mjini, navyo vilivyokuwako kondeni. Mwanzo 34:28

They took their flocks, their herds, their donkeys, that which was in the city, that which was in the field;

Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka. Mwanzo 34:29

and all their wealth. They took captive all their little ones and their wives, and took as plunder everything that was in the house.

Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu. Mwanzo 34:30

Jacob said to Simeon and Levi, "You have troubled me, to make me odious to the inhabitants of the land, among the Canaanites and the Perizzites. I am few in number. They will gather themselves together against me and strike me, and I will be destroyed, I and my house."

Nao wakasema, Je! Ni vema amtendee umbu letu kama kahaba?

Mwanzo 34:31

They said, "Should he deal with our sister as with a prostitute?"