Mwanzo Mlango 46 Genesis

Mwanzo 46:1 Genesis 46:1

Akasafiri Israeli, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye.

Mwanzo 46:2 Genesis 46:2

Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa.

Mwanzo 46:3 Genesis 46:3

Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko.

Mwanzo 46:4 Genesis 46:4

Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako.

Mwanzo 46:5 Genesis 46:5

Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.

Mwanzo 46:6 Genesis 46:6

Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye.

Mwanzo 46:7 Genesis 46:7

Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri.

Mwanzo 46:8 Genesis 46:8

Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli walioingia Misri, Yakobo na wanawe: Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo.

Mwanzo 46:9 Genesis 46:9

Na wana wa Reubeni; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.

Mwanzo 46:10 Genesis 46:10

Na wana wa Simeoni; Yemueli na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli, mwana wa mwanamke Mkanaani.

Mwanzo 46:11 Genesis 46:11

Na wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.

Mwanzo 46:12 Genesis 46:12

Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli.

Mwanzo 46:13 Genesis 46:13

Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni.

Mwanzo 46:14 Genesis 46:14

Na wana wa Zabuloni; Seredi, na Eloni, na Yaleeli.

Mwanzo 46:15 Genesis 46:15

Hao ndio wana wa Lea, aliomzalia Yakobo katika Padan-aramu, na Dina, binti yake. Nafsi zote za wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.

Mwanzo 46:16 Genesis 46:16

Na wana wa Gadi; Sefoni, na Hagi, na Shuni, na Esboni, na Eri, na Arodi, na Areli.

Mwanzo 46:17 Genesis 46:17

Na wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na Sera, umbu lao. Na wana wa Beria ni Heberi, na Malkieli.

Mwanzo 46:18 Genesis 46:18

Hao ndio wana wa Zilpa, ambaye Labani alimpa Lea, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao, nafsi kumi na sita.

Mwanzo 46:19 Genesis 46:19

Wana wa Raheli, mkewe Yakobo Yusufu na Benyamini.

Mwanzo 46:20 Genesis 46:20

Walizaliwa kwake Yusufu katika nchi ya Misri, Manase na Efraimu, aliomzalia Asenathi binti Potifera, kuhani wa Oni.

Mwanzo 46:21 Genesis 46:21

Na wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Ashbeli, na Gera, na Naamani, na Ehi, na Roshi, na Mupimu, na Hupimu, na Ardi.

Mwanzo 46:22 Genesis 46:22

Hao ndio wana wa Raheli, aliomzalia Yakobo, nafsi zote walikuwa kumi na wanne.

Mwanzo 46:23 Genesis 46:23

Na wana wa Dani; Hushimu.

Mwanzo 46:24 Genesis 46:24

Na wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yaseri, na Shilemu.

Mwanzo 46:25 Genesis 46:25

Hao ndio wana wa Bilha, ambaye Labani alimpa Raheli, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao; nafsi zote walikuwa saba.

Mwanzo 46:26 Genesis 46:26

Nafsi zote waliokuja pamoja na Yakobo mpaka Misri waliotoka viunoni mwake, bila wake za wanawe Yakobo, nafsi zote walikuwa sitini na sita.

Mwanzo 46:27 Genesis 46:27

Na wana wa Yusufu aliozaliwa katika Misri walikuwa nafsi wawili. Nafsi zote za nyumba ya Yakobo walioingia Misri walikuwa sabini.

Mwanzo 46:28 Genesis 46:28

Yakobo akampeleka Yuda mbele yake kwa Yusufu, ili amwongoze njia mpaka Gosheni. Wakaja mpaka nchi ya Gosheni.

Mwanzo 46:29 Genesis 46:29

Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kizima.

Mwanzo 46:30 Genesis 46:30

Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai.

Mwanzo 46:31 Genesis 46:31

Yusufu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, Nitapanda mimi nimpashe Farao habari; nitamwambia, Ndugu zangu, na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia.

Mwanzo 46:32 Genesis 46:32

Na watu hao ni wachungaji, maana wamekuwa watu wa kuchunga wanyama, nao wameleta kondoo zao, na ng'ombe zao, na yote waliyo nayo.

Mwanzo 46:33 Genesis 46:33

Itakuwa Farao atakapowaita, na kuwauliza, Kazi yenu ni nini?

Mwanzo 46:34 Genesis 46:34

Semeni, Watumwa wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu; mpate kukaa katika nchi ya Gosheni; maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri.