Mwanzo 26 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 26 (Swahili) Genesis 26 (English)

Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari. Mwanzo 26:1

There was a famine in the land, besides the first famine that was in the days of Abraham. Isaac went to Abimelech king of the Philistines, to Gerar.

Bwana akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia. Mwanzo 26:2

Yahweh appeared to him, and said, "Don't go down into Egypt. Dwell in the land which I will tell you of.

Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. Mwanzo 26:3

Sojourn in this land, and I will be with you, and will bless you. For to you, and to your seed, I will give all these lands, and I will establish the oath which I swore to Abraham your father.

Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. Mwanzo 26:4

I will multiply your seed as the stars of the sky, and will give to your seed all these lands. In your seed will all the nations of the earth be blessed,

Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu. Mwanzo 26:5

because Abraham obeyed my voice, and kept my charge, my commandments, my statutes, and my laws."

Isaka akakaa katika Gerari. Mwanzo 26:6

Isaac lived in Gerar.

Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso. Mwanzo 26:7

The men of the place asked him about his wife. He said, "She is my sister," for he was afraid to say, "My wife," lest, he thought, the men of the place might kill me for Rebekah, because she was beautiful to look on.

Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anacheza-cheza na Rebeka mkewe. Mwanzo 26:8

It happened, when he had been there a long time, that Abimelech king of the Philistines looked out at a window, and saw, and, behold, Isaac was caressing Rebekah, his wife.

Abimeleki akamwita Isaka, akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni ndugu yangu huyu? Isaka akamwambia, Kwa sababu nalisema, Nisife kwa ajili yake. Mwanzo 26:9

Abimelech called Isaac, and said, "Behold, surely she is your wife. Why did you say, 'She is my sister?'" Isaac said to him, "Because I said, 'Lest I die because of her.'"

Abimeleki akasema, Ni nini hii uliyotutendea? Labda mtu mmojawapo angalilala na mkeo bila kufikiri, nawe ungalitutia hatiani. Mwanzo 26:10

Abimelech said, "What is this you have done to us? One of the people might easily have lain with your wife, and you would have brought guilt on us!"

Basi Abimeleki akawaamuru watu wote, akisema, Amgusaye mtu huyu au mkewe lazima atauawa. Mwanzo 26:11

Abimelech charged all the people, saying, "He who touches this man or his wife will surely be put to death."

Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki. Mwanzo 26:12

Isaac sowed in that land, and reaped in the same year one hundred times what he planted. Yahweh blessed him.

Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana. Mwanzo 26:13

The man grew great, and grew more and more until he became very great.

Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu. Mwanzo 26:14

He had possessions of flocks, possessions of herds, and a great household. The Philistines envied him.

Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza kifusi. Mwanzo 26:15

Now all the wells which his father's servants had dug in the days of Abraham his father, the Philistines had stopped, and filled with earth.

Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi. Mwanzo 26:16

Abimelech said to Isaac, "Go from us, for you are much mightier than we."

Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko. Mwanzo 26:17

Isaac departed from there, encamped in the valley of Gerar, and lived there.

Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. Mwanzo 26:18

Isaac dug again the wells of water, which they had dug in the days of Abraham his father. For the Philistines had stopped them after the death of Abraham. He called their names after the names by which his father had called them.

Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. Mwanzo 26:19

Isaac's servants dug in the valley, and found there a well of springing water.

Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye. Mwanzo 26:20

The herdsmen of Gerar argued with Isaac's herdsmen, saying, "The water is ours." He called the name of the well Esek, because they contended with him.

Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. Mwanzo 26:21

They dug another well, and they argued over that, also. He called the name of it Sitnah.

Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi. Mwanzo 26:22

He left that place, and dug another well. They didn't argue over that one. He called it Rehoboth. He said, "For now Yahweh has made room for us, and we will be fruitful in the land."

Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba. Mwanzo 26:23

He went up from there to Beersheba.

Bwana akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu. Mwanzo 26:24

Yahweh appeared to him the same night, and said, "I am the God of Abraham your father. Don't be afraid, for I am with you, and will bless you, and multiply your seed for my servant Abraham's sake."

Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko. Mwanzo 26:25

He built an altar there, and called on the name of Yahweh, and pitched his tent there. There Isaac's servants dug a well.

Ndipo Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli, jemadari wa jeshi lake. Mwanzo 26:26

Then Abimelech went to him from Gerar, and Ahuzzath his friend, and Phicol the captain of his host.

Isaka akawauliza, Mbona mwanijia, nanyi mmenichukia, mkanifukuza kwenu? Mwanzo 26:27

Isaac said to them, "Why have you come to me, since you hate me, and have sent me away from you?"

Wakasema, Hakika tuliona ya kwamba Bwana alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane, sisi na wewe, na kufanya mapatano nawe Mwanzo 26:28

They said, "We saw plainly that Yahweh was with you. We said, 'Let there now be an oath between us, even between us and you, and let us make a covenant with you,

ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe, wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u mbarikiwa wa Bwana. Mwanzo 26:29

that you will do us no harm, as we have not touched you, and as we have done to you nothing but good, and have sent you away in peace.' You are now the blessed of Yahweh."

Basi akawafanyia karamu, nao wakala, wakanywa. Mwanzo 26:30

He made them a feast, and they ate and drink.

Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani. Mwanzo 26:31

They rose up some time in the morning, and swore one to another. Isaac sent them away, and they departed from him in peace.

Ikawa siku ileile, watumwa wa Isaka wakaja wakampasha habari za kile kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, Tumeona maji. Mwanzo 26:32

It happened the same day, that Isaac's servants came, and told him concerning the well which they had dug, and said to him, "We have found water."

Naye akakiita jina lake Shiba; kwa hiyo jina la mji huo ni Beer-sheba, hata leo. Mwanzo 26:33

He called it Shibah.{Shibah means "oath" or "seven."} Therefore the name of the city is Beersheba{Beersheba means "well of the oath" or "well of the seven"} to this day.

Esau alipokuwa mwenye miaka arobaini, akamwoa Yudithi, binti Beeri, Mhiti, na Basemathi, binti Eloni, Mhiti. Mwanzo 26:34

When Esau was forty years old, he took as wife Judith, the daughter of Beeri the Hittite, and Basemath, the daughter of Elon the Hittite.

Roho zao Isaka na Rebeka zikajaa uchungu kwa ajili yao.

Mwanzo 26:35

They grieved Isaac and Rebekah's spirits.