Mwanzo 27 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 27 (Swahili) Genesis 27 (English)

Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa. Mwanzo 27:1

It happened, that when Isaac was old, and his eyes were dim, so that he could not see, he called Esau his elder son, and said to him, "My son?" He said to him, "Here I am."

Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu. Mwanzo 27:2

He said, "See now, I am old. I don't know the day of my death.

Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; Mwanzo 27:3

Now therefore, please take your weapons, your quiver and your bow, and go out to the field, and take me venison.

ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa. Mwanzo 27:4

Make me savory food, such as I love, and bring it to me, that I may eat, and that my soul may bless you before I die."

Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete. Mwanzo 27:5

Rebekah heard when Isaac spoke to Esau his son. Esau went to the field to hunt for venison, and to bring it.

Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia, nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako, akinena, Mwanzo 27:6

Rebekah spoke to Jacob her son, saying, "Behold, I heard your father speak to Esau your brother, saying,

Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili nile, na kukubariki mbele za Bwana kabla ya kufa kwangu. Mwanzo 27:7

'Bring me venison, and make me savory food, that I may eat, and bless you before Yahweh before my death.'

Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama nitakavyokuagiza. Mwanzo 27:8

Now therefore, my son, obey my voice according to that which I command you.

Enenda sasa kundini ukanitwalie wana-mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo. Mwanzo 27:9

Go now to the flock, and get me from there two good kids of the goats. I will make them savory food for your father, such as he loves.

Kisha utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya kufa kwake. Mwanzo 27:10

You shall bring it to your father, that he may eat, so that he may bless you before his death."

Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini. Mwanzo 27:11

Jacob said to Rebekah his mother, "Behold, Esau my brother is a hairy man, and I am a smooth man.

Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si mbaraka. Mwanzo 27:12

What if my father touches me? I will seem to him as a deceiver, and I would bring a curse on myself, and not a blessing."

Mamaye akamwambia, Laana yako na iwe juu yangu, mwanangu, usikie sauti yangu tu, enenda ukaniletee wana-mbuzi. Mwanzo 27:13

His mother said to him, "Let your curse be on me, my son. Only obey my voice, and go get them for me."

Akaenda, akawatwaa, akamletea mamaye. Mamaye akafanya chakula kitamu namna ile aliyopenda babaye. Mwanzo 27:14

He went, and got them, and brought them to his mother. His mother made savory food, such as his father loved.

Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwanawe mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. Mwanzo 27:15

Rebekah took the good clothes of Esau, her elder son, which were with her in the house, and put them on Jacob, her younger son.

Na ngozi za wana-mbuzi akamvika mikononi, na katika ulaini wa shingo yake. Mwanzo 27:16

She put the skins of the kids of the goats on his hands, and on the smooth of his neck.

Naye akampa Yakobo mwanawe mikononi mwake hicho chakula kitamu, na mkate alioufanya. Mwanzo 27:17

She gave the savory food and the bread, which she had prepared, into the hand of her son Jacob.

Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu? Mwanzo 27:18

He came to his father, and said, "My father?" He said, "Here I am. Who are you, my son?"

Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Ondoka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki. Mwanzo 27:19

Jacob said to his father, "I am Esau your firstborn. I have done what you asked me to do. Please arise, sit and eat of my venison, that your soul may bless me."

Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu Bwana, Mungu wako, amenifanikisha. Mwanzo 27:20

Isaac said to his son, "How is it that you have found it so quickly, my son?" He said, "Because Yahweh your God gave me success."

Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo. Mwanzo 27:21

Isaac said to Jacob, "Please come near, that I may feel you, my son, whether you are really my son Esau or not."

Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau. Mwanzo 27:22

Jacob went near to Isaac his father. He felt him, and said, "The voice is Jacob's voice, but the hands are the hands of Esau."

Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika; basi akambariki. Mwanzo 27:23

He didn't recognize him, because his hands were hairy, like his brother, Esau's hands. So he blessed him.

Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi. Mwanzo 27:24

He said, "Are you really my son Esau?" He said, "I am."

Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa. Mwanzo 27:25

He said, "Bring it near to me, and I will eat of my son's venison, that my soul may bless you." He brought it near to him, and he ate. He brought him wine, and he drank.

Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. Mwanzo 27:26

His father Isaac said to him, "Come near now, and kiss me, my son."

Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana. Mwanzo 27:27

He came near, and kissed him. He smelled the smell of his clothing, and blessed him, and said, "Behold, the smell of my son Is as the smell of a field which Yahweh has blessed.

Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mwanzo 27:28

God give you of the dew of the sky, of the fatness of the earth, and plenty of grain and new wine.

Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe. Mwanzo 27:29

Let peoples serve you, Nations bow down to you. Be lord over your brothers, Let your mother's sons bow down to you. Cursed be everyone who curses you, Blessed be everyone who blesses you."

Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake. Mwanzo 27:30

It happened, as soon as Isaac had made an end of blessing Jacob, and Jacob had just gone out from the presence of Isaac his father, that Esau his brother came in from his hunting.

Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki. Mwanzo 27:31

He also made savory food, and brought it to his father. He said to his father, "Let my father arise, and eat of his son's venison, that your soul may bless me."

Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza. Mwanzo 27:32

Isaac his father said to him, "Who are you?" He said, "I am your son, your firstborn, Esau."

Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa. Mwanzo 27:33

Isaac trembled violently, and said, "Who, then, is he who has taken venison, and brought it me, and I have eaten of all before you came, and have blessed him? Yes, he will be blessed."

Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu. Mwanzo 27:34

When Esau heard the words of his father, he cried with an exceeding great and bitter cry, and said to his father, "Bless me, even me also, my father."

Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako. Mwanzo 27:35

He said, "Your brother came with deceit, and has taken away your blessing."

Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka? Mwanzo 27:36

He said, "Isn't he rightly named Jacob? For he has supplanted me these two times. He took away my birthright. See, now he has taken away my blessing." He said, "Haven't you reserved a blessing for me?"

Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu? Mwanzo 27:37

Isaac answered Esau, "Behold, I have made him your lord, and all his brothers have I given to him for servants. With grain and new wine have I sustained him. What then will I do for you, my son?"

Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia. Mwanzo 27:38

Esau said to his father, "Have you but one blessing, my father? Bless me, even me also, my father." Esau lifted up his voice, and wept.

Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,Angalia,penye manono ya nchi patakuwa makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu. Mwanzo 27:39

Isaac his father answered him, "Behold, of the fatness of the earth will be your dwelling, and of the dew of the sky from above.

Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako. Mwanzo 27:40

By your sword will you live, and you will serve your brother. It will happen, when you will break loose, That you shall shake his yoke from off your neck."

Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo. Mwanzo 27:41

Esau hated Jacob because of the blessing with which his father blessed him. Esau said in his heart, "The days of mourning for my father are at hand. Then I will kill my brother Jacob."

Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akapeleka mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zako Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua. Mwanzo 27:42

The words of Esau, her elder son, were told to Rebekah. She sent and called Jacob her younger son, and said to him, "Behold, your brother Esau comforts himself about you by planning to kill you.

Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani; Mwanzo 27:43

Now therefore, my son, obey my voice. Arise, flee to Laban, my brother, in Haran.

ukae kwake siku chache, hata ghadhabu ya ndugu yako igeuke; Mwanzo 27:44

Stay with him a few days, until your brother's fury turns away;

hata ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapopeleka watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja? Mwanzo 27:45

until your brother's anger turn away from you, and he forgets what you have done to him. Then I will send, and get you from there. Why should I be bereaved of you both in one day?"

Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidia nini?

Mwanzo 27:46

Rebekah said to Isaac, "I am weary of my life because of the daughters of Heth. If Jacob takes a wife of the daughters of Heth, such as these, of the daughters of the land, what good will my life do me?"