Ezekieli 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezekieli 6 (Swahili) Ezekiel 6 (English)

Neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 6:1

The word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, uelekeze uso wako uitazame milima ya Israeli, ukaitabirie, Ezekieli 6:2

Son of man, set your face toward the mountains of Israel, and prophesy to them,

ukisema, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi milima na vilima, na vijito na mabonde; Tazama, mimi, naam, mimi, nitaleta upanga juu yenu, nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, Ezekieli 6:3

and say, You mountains of Israel, hear the word of the Lord Yahweh: Thus says the Lord Yahweh to the mountains and to the hills, to the watercourses and to the valleys: Behold, I, even I, will bring a sword on you, and I will destroy your high places.

Na madhabahu zenu zitakuwa ukiwa, na sanamu zenu za jua zitavunjika; nami nitawatupa wana wenu waliouawa mbele ya vinyago vyenu. Ezekieli 6:4

Your altars shall become desolate, and your sun-images shall be broken; and I will cast down your slain men before your idols.

Nami nitaiweka mizoga ya wana wa Israeli mbele ya vinyago vyao; nami nitaitawanya mifupa yenu pande zote za madhabahu zenu. Ezekieli 6:5

I will lay the dead bodies of the children of Israel before their idols; and I will scatter your bones round about your altars.

Kila mahali mkaapo miji itaharibika, na mahali palipoinuka patakuwa ukiwa; ili madhabahu zenu ziharibiwe, na kufanywa ukiwa, na vinyago vyenu vivunjwe, na kukoma, na sanamu zenu za jua zikatwe, na kuangushwa, na kazi zenu zifutwe kabisa. Ezekieli 6:6

In all your dwelling-places the cities shall be laid waste, and the high places shall be desolate; that your altars may be laid waste and made desolate, and your idols may be broken and cease, and your sun-images may be hewn down, and your works may be abolished.

Na hao waliouawa wataanguka katikati yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ezekieli 6:7

The slain shall fall in the midst of you, and you shall know that I am Yahweh.

Lakini nitasaza mabaki; maana mtakuwa na baadhi ya watu watakaoukimbia upanga kati ya mataifa, mtakapokuwa mmetawanyika katika nchi za watu. Ezekieli 6:8

Yet will I leave a remnant, in that you shall have some that escape the sword among the nations, when you shall be scattered through the countries.

Na hao wa kwenu watakaookoka watanikumbuka kati ya mataifa, watakakochukuliwa mateka, jinsi nilivyoiponda mioyo yao ya kikahaba, iliyoniacha, na macho yao, yaendayo kufanya uasherati na vinyago vyao; nao watajichukia nafsi zao machoni pao wenyewe, kwa sababu ya mabaya yao yote, waliyoyatenda kwa machukizo yao yote. Ezekieli 6:9

Those of you that escape shall remember me among the nations where they shall be carried captive, how that I have been broken with their lewd heart, which has departed from me, and with they eyes, which play the prostitute after their idols: and they shall loathe themselves in their own sight for the evils which they have committed in all their abominations.

Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; sikusema bure kama nitawatenda mabaya hayo. Ezekieli 6:10

They shall know that I am Yahweh: I have not said in vain that I would do this evil to them.

Bwana MUNGU asema hivi; Piga kwa mkono wako, ipige nchi kwa mguu wako, ukaseme, Ole! Kwa sababu ya machukizo maovu yote ya nyumba ya Israeli; maana wataanguka kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni. Ezekieli 6:11

Thus says the Lord Yahweh: Smite with your hand, and stamp with your foot, and say, Alas! because of all the evil abominations of the house of Israel; for they shall fall by the sword, by the famine, and by the pestilence.

Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni; na yeye aliye karibu atakufa kwa upanga; na yeye atakayesalia, na kuhusuriwa katika mji, atakufa kwa njaa, hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu juu yao. Ezekieli 6:12

He who is far off shall die of the pestilence; and he who is near shall fall by the sword; and he who remains and is besieged shall die by the famine: thus will I accomplish my wrath on them.

Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, watu wa kwao waliouawa watakapokuwa kati ya vinyago vyao, pande zote za madhabahu zao, juu ya kila kilima kirefu, juu ya vilele vya milima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi, na chini ya kila mwaloni mnene, pale pale walipovifukizia uvumba mzuri vinyago vyao vyote. Ezekieli 6:13

You shall know that I am Yahweh, when their slain men shall be among their idols round about their altars, on every high hill, on all the tops of the mountains, and under every green tree, and under every thick oak, the places where they offered sweet savor to all their idols.

Nami nitanyosha mkono wangu juu yao, na kuifanya nchi kuwa maganjo, tena ukiwa mbaya kuliko jangwa upande wa Dibla, katika makao yao yote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ezekieli 6:14

I will stretch out my hand on them, and make the land desolate and waste, from the wilderness toward Diblah, throughout all their habitations: and they shall know that I am Yahweh.