Ezekieli 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezekieli 16 (Swahili) Ezekiel 16 (English)

Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Ezekieli 16:1

Again the word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, Ezekieli 16:2

Son of man, cause Jerusalem to know her abominations;

useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti. Ezekieli 16:3

and say, Thus says the Lord Yahweh to Jerusalem: Your birth and your birth is of the land of the Canaanite; the Amorite was your father, and your mother was a Hittite.

Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa. Ezekieli 16:4

As for your birth, in the day you were born your navel was not cut, neither were you washed in water to cleanse you; you weren't salted at all, nor swaddled at all.

Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa. Ezekieli 16:5

No eye pitied you, to do any of these things to you, to have compassion on you; but you were cast out in the open field, for that your person was abhorred, in the day that you were born.

Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai. Ezekieli 16:6

When I passed by you, and saw you weltering in your blood, I said to you, [Though you are] in your blood, live; yes, I said to you, [Though you are] in your blood, live.

Nalikufanya kuwa maelfu-elfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, huna nguo. Ezekieli 16:7

I caused you to multiply as that which grows in the field, and you increased and grew great, and you attained to excellent ornament; your breasts were fashioned, and your hair was grown; yet you were naked and bare.

Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nalikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu. Ezekieli 16:8

Now when I passed by you, and looked at you, behold, your time was the time of love; and I spread my skirt over you, and covered your nakedness: yes, I swore to you, and entered into a covenant with you, says the Lord Yahweh, and you became mine.

Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka mafuta; Ezekieli 16:9

Then washed I you with water; yes, I thoroughly washed away your blood from you, and I anointed you with oil.

nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri. Ezekieli 16:10

I clothed you also with embroidered work, and shod you with sealskin, and I girded you about with fine linen, and covered you with silk.

Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako. Ezekieli 16:11

I decked you with ornaments, and I put bracelets on your hands, and a chain on your neck.

Nikatia hazama puani mwako, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu ya kichwa chako. Ezekieli 16:12

I put a ring on your nose, and ear-rings in your ears, and a beautiful crown on your head.

Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme. Ezekieli 16:13

Thus was you decked with gold and silver; and your clothing was of fine linen, and silk, and embroidered work; you ate fine flour, and honey, and oil; and you were exceeding beautiful, and you did prosper to royal estate.

Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana MUNGU. Ezekieli 16:14

Your renown went forth among the nations for your beauty; for it was perfect, through my majesty which I had put on you, says the Lord Yahweh.

Lakini uliutumainia uzuri wako, ukafanya mambo ya kikahaba kwa sababu ya sifa zako, ukamwaga mambo yako ya kikahaba juu ya kila mtu aliyepita; ulikuwa wake. Ezekieli 16:15

But you did trust in your beauty, and played the prostitute because of your renown, and poured out your prostitution on everyone who passed by; his it was.

Ukatwaa baadhi ya mavazi yako, ukajifanyia mahali palipoinuka, palipopambwa kwa rangi mbalimbali, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake; mambo kama hayo hayatakuja wala hayatakuwako. Ezekieli 16:16

You took of your garments, and made for yourselves high places decked with various colors, and played the prostitute on them: [the like things] shall not come, neither shall it be [so].

Pia ulivitwaa vyombo vyako vya uzuri, vya dhahabu yangu na vya fedha yangu, nilivyokupa, ukajifanyia sanamu za wanaume, ukafanya mambo ya kikahaba pamoja nazo; Ezekieli 16:17

You also took your beautiful jewels of my gold and of my silver, which I had given you, and made for yourself images of men, and played the prostitute with them;

ukatwaa nguo zako za kazi ya taraza, ukawafunika, ukaweka mafuta yangu na uvumba wangu mbele yao. Ezekieli 16:18

and you took your embroidered garments, and covered them, and did set my oil and my incense before them.

Mkate wangu niliokupa, unga mzuri, na mafuta, na asali, nilivyokulisha, ukaviweka mbele yao viwe harufu ya kupendeza; na ndivyo vilivyokuwa; asema Bwana MUNGU. Ezekieli 16:19

My bread also which I gave you, fine flour, and oil, and honey, with which I fed you, you did even set it before them for a sweet savor; and [thus] it was, says the Lord Yahweh.

Pamoja na hayo uliwatwaa wana wako na binti zako, ulionizalia, ukawatoa sadaka kwao ili waliwe. Je! Mambo yako ya kikahaba ni kitu kidogo tu, Ezekieli 16:20

Moreover you have taken your sons and your daughters, whom you have borne to me, and these have you sacrificed to them to be devoured. Were your prostitution a small matter,

hata ukawaua watoto wangu, na kuwatoa kwa kuwapitisha motoni kwa hao? Ezekieli 16:21

that you have slain my children, and delivered them up, in causing them to pass through [the fire] to them?

Na katika machukizo yako yote, na mambo yako ya kikahaba, hukuzikumbuka siku za ujana wako, ulipokuwa uchi, huna nguo, ukawa ukigaagaa katika damu yako. Ezekieli 16:22

In all your abominations and your prostitution you have not remembered the days of your youth, when you were naked and bare, and was weltering in your blood.

Tena, imekuwa baada ya uovu wako wote, (ole wako! ole wako! Asema Bwana MUNGU,) Ezekieli 16:23

It is happen after all your wickedness, (woe, woe to you! says the Lord Yahweh),

ulijijengea mahali palipoinuka, ukajifanyia mahali palipoinuka katika kila njia kuu. Ezekieli 16:24

that you have built to you a vaulted place, and have made you a lofty place in every street.

Umejenga mahali pako palipoinuka penye kichwa cha kila njia, ukaufanya uzuri wako kuwa chukizo, ukatanua miguu yako kwa kila mtu aliyepita karibu, ukaongeza mambo yako ya kikahaba. Ezekieli 16:25

You have built your lofty place at the head of every way, and have made your beauty an abomination, and have opened your feet to everyone who passed by, and multiplied your prostitution.

Tena umezini na Wamisri, jirani zako, wakuu wa mwili; ukaongeza mambo yako ya kikahaba, ili kunikasirisha. Ezekieli 16:26

You have also committed sexual immorality with the Egyptians, your neighbors, great of flesh; and have multiplied your prostitution, to provoke me to anger.

Basi, tazama, kwa ajili ya hayo nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nimelipunguza posho lako, na kukutoa kwa mapenzi yao wanaokuchukia, binti za Wafilisti, walioyaonea haya mambo yako ya uasherati. Ezekieli 16:27

See therefore, I have stretched out my hand over you, and have diminished your ordinary [food], and delivered you to the will of those who hate you, the daughters of the Philistines, who are ashamed of your lewd way.

Pia umefanya mambo ya kikahaba pamoja na Waashuri, kwa sababu ulikuwa huwezi kushibishwa; naam, umefanya mambo ya kikahaba pamoja nao, wala hujashiba bado. Ezekieli 16:28

You have played the prostitute also with the Assyrians, because you were insatiable; yes, you have played the prostitute with them, and yet you weren't satisfied.

Pamoja na hayo umeongeza mambo yako ya kikahaba katika nchi ya Kanaani, mpaka Ukaldayo, wala hujashibishwa kwa hayo. Ezekieli 16:29

You have moreover multiplied your prostitution to the land of merchants, to Chaldea; and yet you weren't satisfied with this.

Jinsi moyo wako ulivyokuwa dhaifu, asema Bwana MUNGU, ikiwa unafanya mambo hayo yote, kazi ya mwanamke mzinzi, Ezekieli 16:30

How weak is your heart, says the Lord Yahweh, seeing you do all these things, the work of an impudent prostitute;

apendaye kutawala watu; kwa kuwa wajijengea mahali pako pakuu penye kichwa cha kila njia, na kufanya mahali pako palipoinuka katika kila njia kuu; lakini hukuwa kama kahaba, kwa maana ulidharau kupokea ujira. Ezekieli 16:31

in that you build your vaulted place at the head of every way, and make your lofty place in every street, and have not been as a prostitute, in that you scorn pay.

Mke wa mtu, aziniye! Akaribishaye wageni badala ya mumewe! Ezekieli 16:32

A wife who commits adultery! who takes strangers instead of her husband!

Watu huwapa makahaba wote zawadi, bali wewe unawapa wapenzi wako wote zawadi zako, na kuwapa rushwa ili waje kwako pande zote, kwa ajili ya mambo yako ya kikahaba. Ezekieli 16:33

They give gifts to all prostitutes; but you give your gifts to all your lovers, and bribe them, that they may come to you on every side for your prostitution.

Tena, katika mambo yako ya kikahaba, wewe na wanawake wengine ni mbalimbali, kwa kuwa hapana akufuataye katika mambo yako ya kikahaba; tena kwa kuwa unatoa ujira, wala hupewi ujira; basi, njia yako na njia yao ni mbalimbali. Ezekieli 16:34

You are different from [other] women in your prostitution, in that none follows you to play the prostitute; and whereas you give hire, and no hire is given to you, therefore you are different.

Kwa sababu hiyo, Ewe kahaba, lisikie neno la Bwana; Ezekieli 16:35

Therefore, prostitute, hear the word of Yahweh:

Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu uchafu wako umemwagwa, na uchi wako umefunuliwa, kwa njia ya uzinzi wako pamoja na wapenzi wako; na kwa sababu ya vinyago vyote vya machukizo yako; na kwa sababu ya damu ya watoto wako, uliyowapa; Ezekieli 16:36

Thus says the Lord Yahweh, Because your filthiness was poured out, and your nakedness uncovered through your prostitution with your lovers; and because of all the idols of your abominations, and for the blood of your children, that you gave to them;

basi, tazama, nitawakusanya wapenzi wako wote ambao umejifurahisha pamoja nao, nao wote uliowapenda, pamoja na watu wote uliowachukia; naam, nitawakusanya juu yako pande zote, na kuwafunulia uchi wako, wapate kuuona uchi wako wote. Ezekieli 16:37

therefore see, I will gather all your lovers, with whom you have taken pleasure, and all those who you have loved, with all those who you have hated; I will even gather them against you on every side, and will uncover your nakedness to them, that they may see all your nakedness.

Nami nitakuhukumu, kama wahukumiwavyo wake walioolewa wazinio, na kumwaga damu, nami nitakupatiliza damu ya ghadhabu na wivu. Ezekieli 16:38

I will judge you, as women who break wedlock and shed blood are judged; and I will bring on you the blood of wrath and jealousy.

Tena nitakutia katika mikono yao, nao watapaangusha mahali pako pakuu, na kupabomoa mahali pako palipoinuka, nao watakuvua nguo zako, na kutwaa vyombo vyako vya uzuri, nao watakuacha uchi, huna nguo. Ezekieli 16:39

I will also give you into their hand, and they shall throw down your vaulted place, and break down your lofty places; and they shall strip you of your clothes, and take your beautiful jewels; and they shall leave you naked and bare.

Tena wataleta mkutano wa watu juu yako, nao watakupiga kwa mawe, na kukuchoma kwa panga zao. Ezekieli 16:40

They shall also bring up a company against you, and they shall stone you with stones, and thrust you through with their swords.

Nao watazipiga moto nyumba zako, na kutekeleza hukumu juu yako mbele ya wanawake wengi, nami nitakulazimisha kuacha mambo ya kikahaba, wala hutatoa ujira tena. Ezekieli 16:41

They shall burn your houses with fire, and execute judgments on you in the sight of many women; and I will cause you to cease from playing the prostitute, and you shall also give no hire any more.

Hivyo ndivyo nitakavyoshibisha ghadhabu yangu juu yako, na wivu wangu utanitoka, nami nitatulia wala sitaona hasira tena. Ezekieli 16:42

So will I cause my wrath toward you to rest, and my jealousy shall depart from you, and I will be quiet, and will be no more angry.

Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako, bali umenikasirisha kwa mambo hayo yote; basi, tazama, mimi nami nitaleta njia yako juu ya kichwa chako, asema Bwana MUNGU; wala hutafanya uasherati zaidi ya machukizo yako yote. Ezekieli 16:43

Because you have not remembered the days of your youth, but have raged against me in all these things; therefore, behold, I also will bring your way on your head, says the Lord Yahweh: and you shall not commit this lewdness with all your abominations.

Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake. Ezekieli 16:44

Behold, everyone who uses proverbs shall use [this] proverb against you, saying, As is the mother, so is her daughter.

Wewe u binti ya mama yako, amchukiaye mume wake na watoto wake; nawe u umbu la maumbu yako, waliowachukia waume zao na watoto wao; mama yako alikuwa Mhiti, na baba yako Mwamori. Ezekieli 16:45

You are the daughter of your mother, who loathes her husband and her children; and you are the sister of your sisters, who loathed their husbands and their children: your mother was a Hittite, and your father an Amorite.

Na umbu lako mkubwa ni Samaria, akaaye mkono wako wa kushoto, yeye na binti zake; na umbu lako mdogo, akaaye mkono wako wa kuume, ni Sodoma na binti zake. Ezekieli 16:46

Your elder sister is Samaria, who dwells at your left hand, she and her daughters; and your younger sister, who dwells at your right hand, is Sodom and her daughters.

Lakini hukuenda katika njia zao, wala hukutenda sawasawa na machukizo yao; lakini kana kwamba hilo ni jambo dogo sana, ulikuwa umeharibika kuliko wao katika njia zako zote. Ezekieli 16:47

Yet have you not walked in their ways, nor done after their abominations; but, as [if that were] a very little [thing], you were more corrupt than they in all your ways.

Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, Sodoma, umbu lako, yeye na binti zake, hawakutenda kama wewe ulivyotenda, wewe na binti zako. Ezekieli 16:48

As I live, says the Lord Yahweh, Sodom your sister has not done, she nor her daughters, as you have done, you and your daughters.

Tazama, uovu wa umbu lako, Sodoma, ulikuwa huu; kiburi, na kushiba chakula, na kufanikiwa, hayo yalikuwa ndani yake na binti zake; tena hakuutia nguvu mkono wa maskini na mhitaji. Ezekieli 16:49

Behold, this was the iniquity of your sister Sodom: pride, fullness of bread, and prosperous ease was in her and in her daughters; neither did she strengthen the hand of the poor and needy.

Nao walijivuna, wakafanya machukizo mbele zangu; kwa sababu hiyo naliwaondoa hapo nilipoyaona. Ezekieli 16:50

They were haughty, and committed abomination before me: therefore I took them away as I saw [good].

Samaria naye hakutenda nusu ya dhambi zako; bali wewe umeyaongeza machukizo yako zaidi ya hao, nawe umewapa haki maumbu yako kwa machukizo yako yote uliyoyatenda. Ezekieli 16:51

Neither has Samaria committed half of your sins; but you have multiplied your abominations more than they, and have justified your sisters by all your abominations which you have done.

Wewe nawe, ichukue aibu yako mwenyewe, kwa kuwa umetoa hukumu juu ya maumbu yako; kwa dhambi zako ulizozitenda, zilizochukiza kuliko hao, wao wana haki kuliko wewe; naam, ufedheheke wewe nawe, ukaichukue aibu yako, kwa kuwa umewapa haki maumbu yako. Ezekieli 16:52

You also, bear you your own shame, in that you have given judgment for your sisters; through your sins that you have committed more abominable than they, they are more righteous that you: yes, be also confounded, and bear your shame, in that you have justified your sisters.

Nami nitawarudisha watu wao waliofungwa; wafungwa wa Sodoma na binti zake, na wafungwa wa Samaria na binti zake na wafungwa wako waliofungwa kati yao; Ezekieli 16:53

I will turn again their captivity, the captivity of Sodom and her daughters, and the captivity of Samaria and her daughters, and the captivity of your captives in the midst of them;

upate kuichukua aibu yako mwenyewe, na kutahayari, kwa sababu ya mambo yote uliyoyatenda, kwa kuwa umekuwa faraja kwao. Ezekieli 16:54

that you may bear your own shame, and may be ashamed because of all that you have done, in that you are a comfort to them.

Na maumbu yako, Sodoma na binti zake, watairudia hali yao ya kwanza, na Samaria na binti zake watairudia hali yao ya kwanza, na wewe na binti zako mtairudia hali yenu ya kwanza. Ezekieli 16:55

Your sisters, Sodom and her daughters, shall return to their former estate; and Samaria and her daughters shall return to their former estate; and you and your daughters shall return to your former estate.

Kwa maana umbu lako, Sodoma, hakutajwa kwa kinywa chako katika siku ya kiburi chako; Ezekieli 16:56

For your sister Sodom was not mentioned by your mouth in the day of your pride,

kabla uovu wako haujafunuliwa bado, kama vile wakati ule walipokutukana binti za Shamu, na wale wote waliomzunguka, binti za Wafilisti wanaokudharau pande zote. Ezekieli 16:57

before your wickedness was uncovered, as at the time of the reproach of the daughters of Syria, and of all who are round about her, the daughters of the Philistines, who do despite to you round about.

Umeuchukua uasherati wako, na machukizo yako, asema Bwana. Ezekieli 16:58

You have borne your lewdness and your abominations, says Yahweh.

Maana Bwana MUNGU asema hivi; Nitakutenda vile vile kama ulivyotenda, uliyekidharau kiapo kwa kulivunja agano. Ezekieli 16:59

For thus says the Lord Yahweh: I will also deal with you as you have done, who have despised the oath in breaking the covenant.

Walakini nitalikumbuka agano langu nililolifanya pamoja nawe, katika siku za ujana wako, nami nitaweka imara agano la milele pamoja nawe. Ezekieli 16:60

Nevertheless I will remember my covenant with you in the days of your youth, and I will establish to you an everlasting covenant.

Hapo ndipo utakapozikumbuka njia zako, na kutahayarika, hapo utakapowakaribisha maumbu yako, walio wakubwa wako na wadogo wako; nami nitakupa hao wawe binti zako, lakini si kwa agano lako. Ezekieli 16:61

Then shall you remember your ways, and be ashamed, when you shall receive your sisters, your elder [sisters] and your younger; and I will give them to you for daughters, but not by your covenant.

Nami nitaweka imara agano langu nawe; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; Ezekieli 16:62

I will establish my covenant with you; and you shall know that I am Yahweh;

upate kukumbuka, na kufadhaika, usifumbue kinywa chako tena, kwa sababu ya aibu yako; hapo nitakapokusamehe yote uliyoyatenda, asema Bwana MUNGU. Ezekieli 16:63

that you may remember, and be confounded, and never open your mouth any more, because of your shame, when I have forgiven you all that you have done, says the Lord Yahweh.