Ezekieli 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezekieli 9 (Swahili) Ezekiel 9 (English)

Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. Ezekieli 9:1

Then he cried in my ears with a loud voice, saying, Cause you them that have charge over the city to draw near, every man with his destroying weapon in his hand.

Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba. Ezekieli 9:2

Behold, six men came from the way of the upper gate, which lies toward the north, every man with his slaughter weapon in his hand; and one man in the midst of them clothed in linen, with a writer's inkhorn by his side. They went in, and stood beside the brazen altar.

Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Ezekieli 9:3

The glory of the God of Israel was gone up from the cherub, whereupon it was, to the threshold of the house: and he called to the man clothed in linen, who had the writer's inkhorn by his side.

Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Ezekieli 9:4

Yahweh said to him, Go through the midst of the city, through the midst of Jerusalem, and set a mark on the foreheads of the men that sigh and that cry over all the abominations that are done in the midst of it.

Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Ezekieli 9:5

To the others he said in my hearing, Go you through the city after him, and strike: don't let your eye spare, neither have you pity;

Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. Ezekieli 9:6

kill utterly the old man, the young man and the virgin, and little children and women; but don't come near any man on whom is the mark: and begin at my sanctuary. Then they began at the old men that were before the house.

Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji. Ezekieli 9:7

He said to them, Defile the house, and fill the courts with the slain: go you forth. They went forth, and struck in the city.

Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu? Ezekieli 9:8

It happened, while they were smiting, and I was left, that I fell on my face, and cried, and said, Ah Lord Yahweh! will you destroy all the residue of Israel in your pouring out of your wrath on Jerusalem?

Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, Bwana ameiacha nchi hii, naye Bwana haoni. Ezekieli 9:9

Then said he to me, The iniquity of the house of Israel and Judah is exceeding great, and the land is full of blood, and the city full of wrestling [of judgment]: for they say, Yahweh has forsaken the land, and Yahweh doesn't see.

Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao. Ezekieli 9:10

As for me also, my eye shall not spare, neither will I have pity, but I will bring their way on their head.

Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru. Ezekieli 9:11

Behold, the man clothed in linen, who had the inkhorn by his side, reported the matter, saying, I have done as you have commanded me.