Hesabu 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 18 (Swahili) Numbers 18 (English)

Bwana akamwambia Haruni, Wewe na wanao na nyumba ya baba zako pamoja nawe mtachukua uovu wa patakatifu; wewe na wanao pamoja nawe mtauchukua ukuhani wenu. Hesabu 18:1

Yahweh said to Aaron, You and your sons and your fathers' house with you shall bear the iniquity of the sanctuary; and you and your sons with you shall bear the iniquity of your priesthood.

Na ndugu zako nao, kabila ya Lawi, kabila ya baba yako, uwalete karibu pamoja nawe, ili waungwe nawe, na kukuhudumia; bali wewe na wanao pamoja nawe mtakuwa mbele ya hema ya ushahidi. Hesabu 18:2

Your brothers also, the tribe of Levi, the tribe of your father, bring you near with you, that they may be joined to you, and minister to you: but you and your sons with you shall be before the tent of the testimony.

Nao watashika ulinzi kwa amri yako, na ulinzi wa Hema yote; lakini wasikaribie vyombo vya patakatifu, wala madhabahu, wasife, wao pamoja na ninyi. Hesabu 18:3

They shall keep your charge, and the charge of all the Tent: only they shall not come near to the vessels of the sanctuary and to the altar, that they not die, neither they, nor you.

Nao wataungwa nawe, na kuushika ulinzi wa hema ya kukutania, kwa ajili ya utumishi wote wa hema; na mgeni asiwakaribie ninyi. Hesabu 18:4

They shall be joined to you, and keep the charge of the tent of meeting, for all the service of the Tent: and a stranger shall not come near to you.

Nanyi mtashika ulinzi wa patakatifu, na ulinzi wa madhabahu, isiwe ghadhabu juu ya wana wa Israeli tena. Hesabu 18:5

You shall keep the charge of the sanctuary, and the charge of the altar; that there be wrath no more on the children of Israel.

Nami, tazama, nimewatwaa ndugu zenu Walawi miongoni mwa wana wa Israeli; kwenu ninyi watu hao ni kipawa alichopewa Bwana, waufanye utumishi wa hema ya kukutania. Hesabu 18:6

I, behold, I have taken your brothers the Levites from among the children of Israel: to you they are a gift, given to Yahweh, to do the service of the tent of meeting.

Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa. Hesabu 18:7

You and your sons with you shall keep your priesthood for everything of the altar, and for that within the veil; and you shall serve: I give you the priesthood as a service of gift: and the stranger who comes near shall be put to death.

Kisha Bwana akamwambia Haruni, Tazama, nimekupa wewe ulinzi wa sadaka zangu za kuinuliwa, maana, vitu vyote vya hao wana wa Israeli vilivyowekwa wakfu; nimekupa wewe na wanao vitu hivyo kwa ajili ya kule kutiwa mafuta kwenu, kuwa haki yenu milele. Hesabu 18:8

Yahweh spoke to Aaron, I, behold, I have given you the charge of my heave-offerings, even all the holy things of the children of Israel; to you have I given them by reason of the anointing, and to your sons, as a portion forever.

Vitu hivi vitakuwa vyako katika vile vilivyo vitakatifu sana, visiteketezwe motoni; matoleo yao yote, maana, kila sadaka yao ya unga, na kila sadaka yao ya dhambi, na kila sadaka yao ya hatia watakayonitolea, vitakuwa vitakatifu sana kwa ajili yako wewe na kwa wanao. Hesabu 18:9

This shall be your of the most holy things, [reserved] from the fire: every offering of theirs, even every meal-offering of theirs, and every sin-offering of theirs, and every trespass-offering of theirs, which they shall render to me, shall be most holy for you and for your sons.

Utakula vitu hivyo kuwa ni vitu vitakatifu sana; kila mume atakula vitu hivyo; vitakuwa vitakatifu kwako wewe. Hesabu 18:10

As the most holy things shall you eat of it; every male shall eat of it: it shall be holy to you.

Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, sadaka za kutikiswa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula katika hizo. Hesabu 18:11

This is your: the heave-offering of their gift, even all the wave-offerings of the children of Israel; I have given them to you, and to your sons and to your daughters with you, as a portion forever; everyone who is clean in your house shall eat of it.

Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa Bwana, amekupa wewe hayo. Hesabu 18:12

All the best of the oil, and all the best of the vintage, and of the grain, the first fruits of them which they give to Yahweh, to you have I given them.

Matunda ya kwanza yaivayo katika yote yaliyo katika nchi yao, watakayomletea Bwana, yatakuwa yako, kila mtu aliye safi katika nyumba yako atakula katika vitu hivyo. Hesabu 18:13

The first-ripe fruits of all that is in their land, which they bring to Yahweh, shall be yours; everyone who is clean in your house shall eat of it.

Kila kitu kilichowekwa wakfu katika Israeli kitakuwa chako. Hesabu 18:14

Everything devoted in Israel shall be yours.

Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsongezea Bwana cha wanadamu na cha wanyama, ni chako; lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, huna budi utamkomboa, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utamkomboa. Hesabu 18:15

Everything that opens the womb, of all flesh which they offer to Yahweh, both of man and animal shall be yours: nevertheless the firstborn of man shall you surely redeem, and the firstborn of unclean animals shall you redeem.

Na hao watakaokombolewa katika wanyama hao, tangu aliyepata umri wa mwezi mmoja utamkomboa, kama utakavyohesabu kima chake, kwa fedha ya shekeli tano, kwa shekeli ya mahali patakatifu (nayo ni gera ishirini). Hesabu 18:16

Those who are to be redeemed of them from a month old shall you redeem, according to your estimation, for the money of five shekels, after the shekel of the sanctuary (the same is twenty gerahs).

Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwanza wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, hutawakomboa hao; maana, ni watakatifu hao; utanyunyiza damu yao katika madhabahu, na kuyateketeza mafuta yao kuwa sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto, iwe harufu ya kupendeza. Hesabu 18:17

But the firstborn of a cow, or the firstborn of a sheep, or the firstborn of a goat, you shall not redeem; they are holy: you shall sprinkle their blood on the altar, and shall burn their fat for an offering made by fire, for a sweet savor to Yahweh.

Tena nyama yao itakuwa ni yako wewe, kama kile kidari cha kutikiswa, na kama mguu wa nyuma wa upande wa kuume, itakuwa yako. Hesabu 18:18

The flesh of them shall be your, as the wave-breast and as the right thigh, it shall be yours.

Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa Bwana, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za Bwana kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe. Hesabu 18:19

All the heave-offerings of the holy things, which the children of Israel offer to Yahweh, have I given you, and your sons and your daughters with you, as a portion forever: it is a covenant of salt forever before Yahweh to you and to your seed with you.

Kisha Bwana akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli. Hesabu 18:20

Yahweh said to Aaron, You shall have no inheritance in their land, neither shall you have any portion among them: I am your portion and your inheritance among the children of Israel.

Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania. Hesabu 18:21

To the children of Levi, behold, I have given all the tithe in Israel for an inheritance, in return for their service which they serve, even the service of the tent of meeting.

Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa. Hesabu 18:22

Henceforth the children of Israel shall not come near the tent of meeting, lest they bear sin, and die.

Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi. Hesabu 18:23

But the Levites shall do the service of the tent of meeting, and they shall bear their iniquity: it shall be a statute forever throughout your generations; and among the children of Israel they shall have no inheritance.

Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote. Hesabu 18:24

For the tithe of the children of Israel, which they offer as a heave-offering to Yahweh, I have given to the Levites for an inheritance: therefore I have said to them, Among the children of Israel they shall have no inheritance.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 18:25

Yahweh spoke to Moses, saying,

Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka. Hesabu 18:26

Moreover you shall speak to the Levites, and tell them, When you take of the children of Israel the tithe which I have given you from them for your inheritance, then you shall offer up a heave-offering of it for Yahweh, a tithe of the tithe.

Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa kwenu, kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha kushindikia zabibu. Hesabu 18:27

Your heave-offering shall be reckoned to you, as though it were the grain of the threshing floor, and as the fullness of the winepress.

Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana. Hesabu 18:28

Thus you also shall offer a heave-offering to Yahweh of all your tithes, which you receive of the children of Israel; and of it you shall give Yahweh's heave-offering to Aaron the priest.

Katika vipawa vyenu vyote mtasongeza kila sadaka ya kuinuliwa ya Bwana, ya wema wake wote, hiyo sehemu yake iliyowekwa takatifu. Hesabu 18:29

Out of all your gifts you shall offer every heave-offering of Yahweh, of all the best of it, even the holy part of it out of it.

Kwa ajili ya hayo utawaambia, Mtakapoinua humo hayo yaliyo mema, ndipo yatahesabiwa kuwa ya Walawi, kama kuongea kwake sakafu ya kupuria nafaka, na kama maongeo ya kinu cha kushindikia zabibu. Hesabu 18:30

Therefore you shall tell them, When you heave the best of it from it, then it shall be reckoned to the Levites as the increase of the threshing floor, and as the increase of the wine-press.

Nanyi mtakula hayo kila mahali, ninyi na watu wa nyumbani mwenu; kwa kuwa ni thawabu yenu badala ya utumishi wenu katika hema ya kukutania. Hesabu 18:31

You shall eat it in every place, you and your households: for it is your reward in return for your service in the tent of meeting.

Nanyi hamtachukua dhambi kwa ajili yake, hapo mtakapokwisha kuinua humo hayo mema yake; lakini msivitie unajisi vile vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, ili msife. Hesabu 18:32

You shall bear no sin by reason of it, when you have heaved from it the best of it: and you shall not profane the holy things of the children of Israel, that you not die.