Hesabu 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 5 (Swahili) Numbers 5 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 5:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma maragoni, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya wafu; Hesabu 5:2

"Command the children of Israel that they put out of the camp every leper, and everyone who has an issue, and whoever is unclean by the dead.

mtawatoa nje wote, waume kwa wake, mtawaweka nje ya marago; ili wasiyatie unajisi marago yao, ambayo mimi naketi katikati yake. Hesabu 5:3

Both male and female shall you put out, outside of the camp shall you put them; that they not defile their camp, in the midst of which I dwell."

Wana wa Israeli wakafanya vivyo, wakawatoa na kuwaweka nje ya marago; kama Bwana alivyonena na Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. Hesabu 5:4

The children of Israel did so, and put them out outside of the camp; as Yahweh spoke to Moses, so did the children of Israel.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 5:5

Yahweh spoke to Moses, saying,

Uwaambie wana wa Israeli, Mtu mume au mke atakapofanya dhambi yo yote, ifanywayo na binadamu, kumwasi Bwana, na mtu huyo akawa na hatia; Hesabu 5:6

"Speak to the children of Israel: When a man or woman commits any sin that men commit, so as to trespass against Yahweh, and that soul is guilty;

ndipo watakapoungama dhambi yao waliyoifanya; naye atarudisha kwa hatia yake, kwa utimilifu wake, tena ataongeza juu yake sehemu ya tano, na kumpa huyo aliyemkosa. Hesabu 5:7

then he shall confess his sin which he has done, and he shall make restitution for his guilt in full, and add to it the fifth part of it, and give it to him in respect of whom he has been guilty.

Lakini kwamba mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye inampasa kurudishiwa kwa ajili ya hiyo hatia, kile kitakachorudishwa kwa Bwana kwa hiyo hatia kitakuwa cha kuhani, pamoja na kondoo mume wa upatanisho, ambaye kwa huyo utafanywa upatanisho kwa ajili yake. Hesabu 5:8

But if the man has no kinsman to whom restitution may be made for the guilt, the restitution for guilt which is made to Yahweh shall be the priest's; besides the ram of the atonement, by which atonement shall be made for him.

Tena kila sadaka ya kuinuliwa, ya vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, watakavyosongeza kwa kuhani, itakuwa ni yake. Hesabu 5:9

Every heave offering of all the holy things of the children of Israel, which they present to the priest, shall be his.

Tena vitu vilivyowekwa wakfu na mtu awaye yote, vitakuwa ni vya kuhani; kitu cho chote mtu atakachompa kuhani, kitakuwa chake. Hesabu 5:10

Every man's holy things shall be his: whatever any man gives the priest, it shall be his."

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 5:11

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na wana wa israeli, uwaambie, kama mke wa mtu ye yote akikengeuka, na kumkosa mumewe, Hesabu 5:12

"Speak to the children of Israel, and tell them: If any man's wife goes astray, and is unfaithful to him,

na mtu mume akalala naye kwa uasherati, na jambo hilo likamfichamania mumewe, likawa jambo lisilojulikana, na huyo mwanamke akawa najisi, wala hapana shahidi aliyeshuhudia juu yake, wala hakufumaniwa; Hesabu 5:13

and a man lies with her carnally, and it is hidden from the eyes of her husband, and is kept close, and she is defiled, and there is no witness against her, and she isn't taken in the act;

kisha mumewe akashikwa na roho ya wivu, akamwonea wivu mkewe, naye akawa najisi huyo mwanamke; au kama akiingiwa na roho ya wivu, akamwonea wivu mkewe, naye hakuwa na unajisi huyo mke; Hesabu 5:14

and the spirit of jealousy comes on him, and he is jealous of his wife, and she is defiled: or if the spirit of jealousy comes on him, and he is jealous of his wife, and she isn't defiled:

ndipo huyo mume atamchukua mkewe, aende naye kwa kuhani, naye ataleta sadaka yake kwa ajili yake, yaani, sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri; asitie mafuta juu yake, wala asitie ubani juu yake; maana, ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho ya kukumbukia uovu. Hesabu 5:15

then the man shall bring his wife to the priest, and shall bring her offering for her: the tenth part of an ephah of barley meal. He shall pour no oil on it, nor put frankincense on it, for it is a meal offering of jealousy, a meal offering of memorial, bringing iniquity to memory.

Basi kuhani atamleta mwanamke akaribie, na kumweka mbele za Bwana; Hesabu 5:16

The priest shall bring her near, and set her before Yahweh;

kisha kuhani atatwaa maji matakatifu katika chombo cha udongo; kisha kuhani atatwaa katika vumbi lililo pale chini ya maskani, na kulitia katika hayo maji; Hesabu 5:17

and the priest shall take holy water in an earthen vessel; and of the dust that is on the floor of the tabernacle the priest shall take, and put it into the water.

kisha kuhani atamweka mwanamke mbele za Bwana, naye atazifungua nywele za kichwani mwa huyo mwanamke, kisha atampa hiyo sadaka ya unga ya ukumbusho mikononi mwake, ambayo ni sadaka ya unga ya wivu, naye kuhani atakuwa na hayo maji ya uchungu yaletayo laana mkononi mwake; Hesabu 5:18

The priest shall set the woman before Yahweh, and let the hair of the woman's head go loose, and put the meal offering of memorial in her hands, which is the meal offering of jealousy. The priest shall have in his hand the water of bitterness that brings a curse.

tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena kwamba hukukengeuka kuandama uchafu, uli chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana yasikudhuru; Hesabu 5:19

The priest shall cause her to swear, and shall tell the woman, 'If no man has lain with you, and if you haven't gone aside to uncleanness, being under your husband, be free from this water of bitterness that brings a curse.

lakini kwamba umekengeuka uli chini ya mumeo, na kwamba u hali ya unajisi, na mtu mume amelala nawe, asiyekuwa mumeo; Hesabu 5:20

But if you have gone astray, being under your husband, and if you are defiled, and some man has lain with you besides your husband:'

hapo ndipo kuhani atamwapisha mwanamke kwa kiapo cha kuapiza, kisha kuhani atamwambia huyo mwanamke maneno haya, Bwana na akufanye wewe uwe laana na kiapo kati ya watu wako, hapo Bwana akufanyapo paja lako kupooza, na tumbo lako kuvimba; Hesabu 5:21

then the priest shall cause the woman to swear with the oath of cursing, and the priest shall tell the woman, 'Yahweh make you a curse and an oath among your people, when Yahweh allows your thigh to fall away, and your body to swell;

na maji yaletayo laana yatakuingia matumboni mwako, na kukuvimbisha tumbo, na kukupoozesha paja lako; na mwanamke ataitika, Amina, Amina. Hesabu 5:22

and this water that brings a curse will go into your bowels, and make your body swell, and your thigh fall away.' The woman shall say, 'Amen, Amen.'

Kisha kuhani ataziandika laana hizo ndani ya kitabu, na kuzifuta katika maji ya uchungu; Hesabu 5:23

"The priest shall write these curses in a book, and he shall blot them out into the water of bitterness.

kisha atamnywesha mwanamke hayo maji ya uchungu yaletayo laana; nayo maji yaletayo laana yataingia ndani yake, nayo yatageuka kuwa uchungu. Hesabu 5:24

He shall make the woman drink the water of bitterness that causes the curse; and the water that causes the curse shall enter into her and become bitter.

Kisha kuhani ataitwaa hiyo sadaka ya unga ya wivu, kwa kuiondoa mkononi mwa huyo mwanamke, naye ataitikisa sadaka ya unga mbele ya Bwana, na kuisongeza pale madhabahuni; Hesabu 5:25

The priest shall take the meal offering of jealousy out of the woman's hand, and shall wave the meal offering before Yahweh, and bring it to the altar.

kisha kuhani atatwaa konzi moja ya sadaka ya unga, kuwa ni ukumbusho wake, na kuuteketeza madhabahuni, baadaye atamnywesha mwanamke hayo maji. Hesabu 5:26

The priest shall take a handful of the meal offering, as the memorial of it, and burn it on the altar, and afterward shall make the woman drink the water.

Kisha hapo atakapokwisha kumnywesha maji, ndipo itakapokuwa, kama amekuwa hali ya unajisi na kumkosa mumewe, hayo maji yaletayo laana yatamwingia ndani yake, nayo yatakuwa uchungu, na tumbo lake litavimba, na paja lake litapooza; na huyo mwanamke atakuwa laana kati ya watu wake. Hesabu 5:27

When he has made her drink the water, then it shall happen, if she is defiled, and has committed a trespass against her husband, that the water that causes the curse will enter into her and become bitter, and her body will swell, and her thigh will fall away: and the woman will be a curse among her people.

Na kama mwanamke hakuwa na unajisi lakini yu safi; ndipo ataachiliwa, naye atazaa wana. Hesabu 5:28

If the woman isn't defiled, but is clean; then she shall be free, and shall conceive seed.

Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi; Hesabu 5:29

"This is the law of jealousy, when a wife, being under her husband, goes astray, and is defiled;

au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume, naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za Bwana, na kuhani atatenda juu yake sheria hii yote. Hesabu 5:30

or when the spirit of jealousy comes on a man, and he is jealous of his wife; then he shall set the woman before Yahweh, and the priest shall execute on her all this law.

Na huyo mume atakuwa hana uovu, na mwanamke atauchukua uovu wake. Hesabu 5:31

The man shall be free from iniquity, and that woman shall bear her iniquity."