Hesabu 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 13 (Swahili) Numbers 13 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, Hesabu 13:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao. Hesabu 13:2

Send you men, that they may spy out the land of Canaan, which I give to the children of Israel: of every tribe of their fathers shall you send a man, everyone a prince among them.

Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na Bwana; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli. Hesabu 13:3

Moses sent them from the wilderness of Paran according to the commandment of Yahweh: all of them men who were heads of the children of Israel.

Na majina yao ni haya; katika kabila ya Reubeni, Shamua mwana Zakuri. Hesabu 13:4

These were their names: Of the tribe of Reuben, Shammua the son of Zaccur.

Katika kabila ya Simeoni, Shafati mwana wa Hori. Hesabu 13:5

Of the tribe of Simeon, Shaphat the son of Hori.

Katika kabila ya Yuda, Kalebu mwana wa Yefune. Hesabu 13:6

Of the tribe of Judah, Caleb the son of Jephunneh.

Katika kabila ya Isakari, Igali mwana wa Yusufu. Hesabu 13:7

Of the tribe of Issachar, Igal the son of Joseph.

Katika kabila ya Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni Hesabu 13:8

Of the tribe of Ephraim, Hoshea the son of Nun.

Katika kabila ya Benyamini, Palti mwana wa Rafu. Hesabu 13:9

Of the tribe of Benjamin, Palti the son of Raphu.

Katika kabila ya Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi. Hesabu 13:10

Of the tribe of Zebulun, Gaddiel the son of Sodi.

Katika kabila ya Yusufu, yaani, katika kabila ya Manase, Gadi mwana wa Susi. Hesabu 13:11

Of the tribe of Joseph, [namely], of the tribe of Manasseh, Gaddi the son of Susi.

Katika kabila ya Dani, Amieli mwana wa Gemali. Hesabu 13:12

Of the tribe of Dan, Ammiel the son of Gemalli.

Katika kabila ya Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli. Hesabu 13:13

Of the tribe of Asher, Sethur the son of Michael.

Katika kabila ya Naftali, Nabi mwana wa Wofsi. Hesabu 13:14

Of the tribe of Naphtali, Nahbi the son of Vophsi.

Katika kabila ya Gadi, Geueli mwana wa Maki. Hesabu 13:15

Of the tribe of Gad, Geuel the son of Machi.

Hayo ndiyo majina ya hao watu waliotumwa na Musa waende kuipeleleza nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita jina lake Yoshua. Hesabu 13:16

These are the names of the men who Moses sent to spy out the land. Moses called Hoshea the son of Nun Joshua.

Musa akawapeleka ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, Pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani, Hesabu 13:17

Moses sent them to spy out the land of Canaan, and said to them, Go up this way by the South, and go up into the hill-country:

mkaitazame nchi ni ya namna gani; na watu wanaokaa ndani yake, kwamba ni hodari au dhaifu, kwamba ni wachache au wengi; Hesabu 13:18

and see the land, what it is; and the people who dwell therein, whether they are strong or weak, whether they are few or many;

na nchi wanayoikaa kwamba ni njema au mbaya; kwamba wanakaa katika matuo au katika ngome; Hesabu 13:19

and what the land is that they dwell in, whether it is good or bad; and what cities they are that they dwell in, whether in camps, or in strongholds;

nayo nchi ni ya namna gani, kwamba ni nchi ya unono au ya njaa, kwamba ina msitu au sivyo. Iweni na moyo mkuu, mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakati wa kuiva zabibu za kwanza. Hesabu 13:20

and what the land is, whether it is fat or lean, whether there is wood therein, or not. Be of good courage, and bring of the fruit of the land. Now the time was the time of the first-ripe grapes.

Basi wakapanda wakaipeleleza nchi toka jangwa la Sini hata Rehobu, mpaka kuingia Hamathi. Hesabu 13:21

So they went up, and spied out the land from the wilderness of Zin to Rehob, to the entrance of Hamath.

Wakapanda katika Negebu, wakafika Hebroni; na Ahimani, na Sheshai, na Talmai, wana wa Anaki, walikuwako huko. Nao Hebroni ulijengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri. Hesabu 13:22

They went up by the South, and came to Hebron; and Ahiman, Sheshai, and Talmai, the children of Anak, were there. (Now Hebron was built seven years before Zoan in Egypt.)

Wakafika bonde la Eshkoli, na huko wakakata tawi lenye kishada kimoja cha zabibu, wakalichukua kwa mti kati ya watu wawili; wakaleta makomamanga pia, na tini. Hesabu 13:23

They came to the valley of Eshcol, and cut down from there a branch with one cluster of grapes, and they bore it on a staff between two; [they brought] also of the pomegranates, and of the figs.

Bonde lile liliitwa bonde la Eshkoli kwa sababu ya hicho kishada walichokata huko wana wa Israeli. Hesabu 13:24

That place was called the valley of Eshcol, because of the cluster which the children of Israel cut down from there.

Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku arobaini. Hesabu 13:25

They returned from spying out the land at the end of forty days.

Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi. Hesabu 13:26

They went and came to Moses, and to Aaron, and to all the congregation of the children of Israel, to the wilderness of Paran, to Kadesh; and brought back word to them, and to all the congregation, and shown them the fruit of the land.

Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake. Hesabu 13:27

They told him, and said, We came to the land where you sent us; and surely it flows with milk and honey; and this is the fruit of it.

Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko. Hesabu 13:28

However the people who dwell in the land are strong, and the cities are fortified, [and] very great: and moreover we saw the children of Anak there.

Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani. Hesabu 13:29

Amalek dwells in the land of the South: and the Hittite, and the Jebusite, and the Amorite, dwell in the hill-country; and the Canaanite dwells by the sea, and along by the side of the Jordan.

Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Hesabu 13:30

Caleb stilled the people before Moses, and said, Let us go up at once, and possess it; for we are well able to overcome it.

Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Hesabu 13:31

But the men who went up with him said, We aren't able to go up against the people; for they are stronger than we.

Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Hesabu 13:32

They brought up an evil report of the land which they had spied out to the children of Israel, saying, The land, through which we have gone to spy it out, is a land that eats up the inhabitants of it; and all the people who we saw in it are men of great stature.

Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi. Hesabu 13:33

There we saw the Nephilim, the sons of Anak, who come of the Nephilim: and we were in our own sight as grasshoppers, and so we were in their sight.