Hesabu 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 4 (Swahili) Numbers 4 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, Hesabu 4:1

Yahweh spoke to Moses and to Aaron, saying,

Katika wana wa Lawi uitenge hesabu ya wana wa Kohathi, kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao, Hesabu 4:2

"Take a census of the sons of Kohath from among the sons of Levi, by their families, by their fathers' houses,

tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi hata umri wa miaka hamsini, wote waingiao katika utumishi huo, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania. Hesabu 4:3

from thirty years old and upward even until fifty years old, all who enter into the service, to do the work in the Tent of Meeting.

Huu ndio utumishi wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania, katika vile vyombo vitakatifu sana; Hesabu 4:4

This is the service of the sons of Kohath in the Tent of Meeting, the most holy things.

hapo watakapong'oa safari, Haruni ataingia ndani, na wanawe, nao watalishusha pazia la sitara, na kulifunika sanduku la ushahidi kwa hilo pazia; Hesabu 4:5

When the camp moves forward, Aaron shall go in, and his sons, and they shall take down the veil of the screen, and cover the ark of the Testimony with it,

kisha atatia juu yake ngozi za pomboo za kulifunikia, na kutandika juu yake nguo ya rangi ya samawi tupu, kisha watatia hiyo miti yake. Hesabu 4:6

and shall put a covering of sealskin on it, and shall spread over it a cloth all of blue, and shall put in its poles.

Tena juu ya meza ya mikate ya wonyesho watatandika nguo ya rangi ya samawi, na kuweka juu yake sahani, na miiko, na mabakuli, na vikombe vya kumiminia; na hiyo mikate ya daima itakuwa juu yake; Hesabu 4:7

On the table of show bread they shall spread a blue cloth, and put on it the dishes, the spoons, the bowls, and the cups with which to pour out; and the continual bread shall be on it.

nao watatandika juu yake nguo ya rangi nyekundu, na kuifunika kwa ngozi za pomboo za kuifunikia, na kuitia ile miti yake. Hesabu 4:8

They shall spread on them a scarlet cloth, and cover the same with a covering of sealskin, and shall put in its poles.

Kisha watatwaa nguo ya rangi ya samawi, na kukifunika kinara cha taa ya nuru, na taa zake, na makasi yake, na sahani zake za kutilia makaa, na vyombo vyake vyote vya mafuta, watumiavyo kwa kazi yake; Hesabu 4:9

They shall take a blue cloth, and cover the lampstand of the light, and its lamps, and its snuffers, and its snuff dishes, and all its oil vessels, with which they minister to it.

nao watakitia, na vyombo vyake vyote, ndani ya ngozi ya pomboo, na kukitia juu ya miti ya kukichukulia Hesabu 4:10

They shall put it and all its vessels within a covering of sealskin, and shall put it on the frame.

Tena watatandika nguo ya rangi ya samawi juu ya madhabahu ya dhahabu, na kuifunika kwa ngozi za pomboo, na kuitia ile miti yake; Hesabu 4:11

On the golden altar they shall spread a blue cloth, and cover it with a covering of sealskin, and shall put in its poles.

kisha watavitwaa vile vyombo vyote vya utumishi wavitumiavyo katika mahali patakatifu, na kuvitia katika nguo ya rangi ya samawi, na kuvifunika kwa ngozi za pomboo, na kuvitia juu ya miti ya kuvichukulia. Hesabu 4:12

They shall take all the vessels of ministry, with which they minister in the sanctuary, and put them in a blue cloth, and cover them with a covering of sealskin, and shall put them on the frame.

Nao watayaondoa hayo majivu madhabahuni; na kutandika nguo ya rangi ya zambarau juu yake; Hesabu 4:13

They shall take away the ashes from the altar, and spread a purple cloth on it.

nao wataweka vyombo vyake vyote juu yake ambavyo wavitumia katika madhabahu, vyetezo, na nyuma, na miiko, na mabakuli, vyombo vyote vya hiyo madhabahu; nao watatandika juu yake ngozi za pomboo, na kutia miti yake mahali pake. Hesabu 4:14

They shall put on it all its vessels, with which they minister about it, the fire pans, the flesh hooks, the shovels, and the basins; all the vessels of the altar; and they shall spread on it a covering of sealskin, and put in its poles.

Na Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong'oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife. Vyombo vile ni mzigo wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania. Hesabu 4:15

"When Aaron and his sons have finished covering the sanctuary, and all the furniture of the sanctuary, as the camp moves forward; after that, the sons of Kohath shall come to carry it: but they shall not touch the sanctuary, lest they die. These things are the burden of the sons of Kohath in the Tent of Meeting.

Na ulinzi wake Eleazari mwana wa Haruni kuhani utakuwa ni kuyaangalia mafuta kwa nuru, na uvumba mzuri, na sadaka ya unga ya daima, na mafuta ya kupaka, tena ulinzi wa hiyo maskani yote, na wa vitu vyote vilivyo ndani yake, mahali patakatifu, na vyombo vyake. Hesabu 4:16

"The charge of Eleazar the son of Aaron the priest shall be the oil for the light, the sweet incense, the continual meal offering, and the anointing oil, the charge of all the tabernacle, and of all that is in it, the sanctuary, and its furnishings."

Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, Hesabu 4:17

Yahweh spoke to Moses and to Aaron, saying,

Msiitenge kabisa kabila ya jamaa za Wakohathi katika hao Walawi; Hesabu 4:18

"Don't cut off the tribe of the families of the Kohathites from among the Levites;

lakini wafanyieni neno hili, ili kwamba wawe hai, wasife, hapo watakapovikaribia vile vitu vilivyo vitakatifu sana; Haruni na wanawe wataingia ndani, na kuwawekea kila mtu utumishi wake, na kila mtu mzigo wake; Hesabu 4:19

but thus do to them, that they may live, and not die, when they approach to the most holy things: Aaron and his sons shall go in, and appoint them everyone to his service and to his burden;

lakini wasiingie wao kupaona mahali pale patakatifu, hata kwa dakika moja, ili wasife. Hesabu 4:20

but they shall not go in to see the sanctuary even for a moment, lest they die."

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 4:21

Yahweh spoke to Moses, saying,

Fanya jumla ya wana wa Gershoni nao, kwa nyumba za baba zao, na jamaa zao; Hesabu 4:22

"Take a census of the sons of Gershon also, by their fathers' houses, by their families;

tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini utawahesabu; wote watakaoingia kutumika, ili kufanya kazi katika hema ya kukutania. Hesabu 4:23

from thirty years old and upward until fifty years old shall you number them; all who enter in to wait on the service, to do the work in the Tent of Meeting.

Huu ni utumishi wa jamaa za Wagershoni, katika kutumika na katika kuchukua mizigo; Hesabu 4:24

This is the service of the families of the Gershonites, in serving and in bearing burdens:

wao watayachukua mapazia ya maskani, na hema ya kukutania, hizo nguo za kufunikia, na zile ngozi za pomboo za kufunikia zilizo juu yake, na pazia la mlango wa hema ya kukutania; Hesabu 4:25

they shall carry the curtains of the tabernacle, and the Tent of Meeting, its covering, and the covering of sealskin that is above on it, and the screen for the door of the Tent of Meeting,

na kuta za nguo za ua, na sitara ya ile nafasi ya kuingilia ya lango la ua, ulio karibu na maskani na madhabahu, kuzunguka pande zote, na kamba zake, na vyombo vyote vya utumishi wao, na yote yatakayotendeka kwavyo, watatumika katika hayo. Hesabu 4:26

and the hangings of the court, and the screen for the door of the gate of the court, which is by the tabernacle and around the altar, and their cords, and all the instruments of their service, and whatever shall be done with them. Therein shall they serve.

Utumishi wote wa wana wa Wagershoni, katika mzigo wao wote, na utumishi wao wote, utakuwa kwa amri ya Haruni na wanawe; nanyi mtawaagizia mzigo wao wote kuulinda. Hesabu 4:27

At the commandment of Aaron and his sons shall be all the service of the sons of the Gershonites, in all their burden, and in all their service; and you shall appoint to them in charge all their burden.

Huu ni utumishi wa jamaa za wana wa Wagershoni katika hema kukutania; na ulinzi utakuwa chini ya mkono wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani. Hesabu 4:28

This is the service of the families of the sons of the Gershonites in the Tent of Meeting: and their charge shall be under the hand of Ithamar the son of Aaron the priest.

Katika habari ya wana wa Merari, utawahesabu kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao; Hesabu 4:29

"As for the sons of Merari, you shall number them by their families, by their fathers' houses;

tangu aliyepata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, utawahesabu, kila atakayeingia katika huo utumishi, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania. Hesabu 4:30

from thirty years old and upward even to fifty years old shall you number them, everyone who enters on the service, to do the work of the Tent of Meeting.

Na mausia ya mzigo wao ni haya, kwa utumishi wao wote katika hema ya kukutania; mbao za maskani, na mataruma yake, na nguzo zake, na matako yake; Hesabu 4:31

This is the charge of their burden, according to all their service in the Tent of Meeting: the tabernacle's boards, its bars, its pillars, its sockets,

na viguzo vya ua vya kuuzunguka pande zote, na matako yake, na vigingi vyake, na kamba zake, na vyombo vyake vyote, pamoja na utumishi wake wote; nanyi mtawaagizia kila mtu kwa jina lake vile vyombo vya mzigo wao watakaoulinda. Hesabu 4:32

and the pillars of the court around it, and their sockets, and their pins, and their cords, with all their instruments, and with all their service: and by name you shall appoint the instruments of the charge of their burden.

Huu ni utumishi wa jamaa za wana wa Merari, kwa utumishi wao wote, katika hema ya kukutania, chini ya mkono wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani. Hesabu 4:33

This is the service of the families of the sons of Merari, according to all their service, in the Tent of Meeting, under the hand of Ithamar the son of Aaron the priest."

Basi Musa na Haruni na hao wakuu wa mkutano wakawahesabu wana wa Kohathi kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao, Hesabu 4:34

Moses and Aaron and the princes of the congregation numbered the sons of the Kohathites by their families, and by their fathers' houses,

tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, kila mtu aliyeingia katika utumishi kwa kazi katika hema ya kukutania, Hesabu 4:35

from thirty years old and upward even to fifty years old, everyone who entered into the service, for work in the Tent of Meeting.

na waliohesabiwa kwao kwa jamaa zao, walikuwa elfu mbili na mia saba hamsini. Hesabu 4:36

Those who were numbered of them by their families were two thousand seven hundred fifty.

Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za Wakohathi, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya Bwana kwa mkono wa Musa. Hesabu 4:37

These are those who were numbered of the families of the Kohathites, all who served in the Tent of Meeting, whom Moses and Aaron numbered according to the commandment of Yahweh by Moses.

Na hao waliohesabiwa katika wana wa Gershoni, kwa jamaa zao na nyumba zao baba zao, Hesabu 4:38

Those who were numbered of the sons of Gershon, their families, and by their fathers' houses,

tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, kila mtu aliyeingia katika utumishi, kwa kazi katika hema ya kukutania, Hesabu 4:39

from thirty years old and upward even to fifty years old, everyone who entered into the service, for work in the Tent of Meeting,

hata wale waliohesabiwa kwao, kwa jamaa zao na nyumba za baba zao, walikuwa elfu mbili na mia sita na thelathini. Hesabu 4:40

even those who were numbered of them, by their families, by their fathers' houses, were two thousand six hundred thirty.

Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Gershoni, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya Bwana. Hesabu 4:41

These are those who were numbered of the families of the sons of Gershon, all who served in the Tent of Meeting, whom Moses and Aaron numbered according to the commandment of Yahweh.

Na hao waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Merari, kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao, Hesabu 4:42

Those who were numbered of the families of the sons of Merari, by their families, by their fathers' houses,

tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, kila mtu aliyeingia katika utumishi kwa kazi katika hema ya kukutania, Hesabu 4:43

from thirty years old and upward even to fifty years old, everyone who entered into the service, for work in the Tent of Meeting,

wale waliohesabiwa kwao, kwa jamaa zao, walikuwa elfu tatu na mia mbili. Hesabu 4:44

even those who were numbered of them by their families, were three thousand two hundred.

Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Merari, ambao Musa na; Haruni waliwahesabu kwa amri ya Bwana, kwa mkono wa Musa. Hesabu 4:45

These are those who were numbered of the families of the sons of Merari, whom Moses and Aaron numbered according to the commandment of Yahweh by Moses.

Wote waliohesabiwa katika Walawi, ambao Musa na Haruni na hao wakuu wa Israeli waliwahesabu, kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao, Hesabu 4:46

All those who were numbered of the Levites, whom Moses and Aaron and the princes of Israel numbered, by their families, and by their fathers' houses,

tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, kila aliyeingia kufanya kazi ya utumishi, na kazi ya kuchukua mizigo katika hema ya kukutania, Hesabu 4:47

from thirty years old and upward even to fifty years old, everyone who entered in to do the work of service, and the work of bearing burdens in the Tent of Meeting,

hao waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu nane na mia tano themanini. Hesabu 4:48

even those who were numbered of them, were eight thousand five hundred eighty.

Kwa amri ya Bwana, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama Bwana alivyomwagiza Musa.

Hesabu 4:49

According to the commandment of Yahweh they were numbered by Moses, everyone according to his service, and according to his burden. Thus were they numbered by him, as Yahweh commanded Moses.