Hesabu Mlango 33 Numbers

Hesabu 33:1

Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni.

Hesabu 33:2

Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya Bwana; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa.

Hesabu 33:3

Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote,

Hesabu 33:4

hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, Bwana aliokuwa amewapiga kati yao; Bwana akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo.

Hesabu 33:5

Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapanga katika Sukothi.

Hesabu 33:6

Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapanga Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika.

Hesabu 33:7

Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapanga mbele ya Migdoli.

Hesabu 33:8

Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapanga Mara.

Hesabu 33:9

Wakasafiri kutoka Mara, wakafikilia Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapanga hapo.

Hesabu 33:10

Wakasafiri kutoka Elimu wakapanga karibu na Bahari ya Shamu.

Hesabu 33:11

Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapanga katika nyika ya Sini.

Hesabu 33:12

Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka.

Hesabu 33:13

Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi.

Hesabu 33:14

Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa.

Hesabu 33:15

Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapanga katika nyika ya Sinai.

Hesabu 33:16

Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapanga Kibroth-hataava.

Hesabu 33:17

Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapanga Haserothi.

Hesabu 33:18

Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga Rithma.

Hesabu 33:19

Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi.

Hesabu 33:20

Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapanga Libna.

Hesabu 33:21

Wakasafiri kutoka Libna, wakapanga Risa.

Hesabu 33:22

Wakasafiri kutoka Risa, wakapanga Keheletha.

Hesabu 33:23

Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapanga katika mlima wa Sheferi

Hesabu 33:24

Wakasafiri kutoka huo mlima wa Sheferi, wakapanga Harada.

Hesabu 33:25

Wakasafiri kutoka Harada, wakapanga Makelothi.

Hesabu 33:26

Wakasafiri kutoka Makelothi, wakapanga Tahathi.

Hesabu 33:27

Wakasafiri kutoka Tahathi wakapanga Tera.

Hesabu 33:28

Wakasafiri kutoka Tera, wakapanga Mithka.

Hesabu 33:29

Wakasafiri kutoka Mithka, wakapanga Hashmona.

Hesabu 33:30

Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapanga Moserothi.

Hesabu 33:31

Wakasafiri kutoka Moserothi, wakapanga Bene-yakani.

Hesabu 33:32

Wakasafiri kutoka Bene-yakani, wakapanga Hor-hagidgadi.

Hesabu 33:33

Wakasafiri kutoka Hor-hagidgadi, wakapanga Yotbatha.

Hesabu 33:34

Wakasafiri kutoka Yotbatha, wakapanga Abrona.

Hesabu 33:35

Wakasafiri kutoka Abrona, wakapanga Esion-geberi.

Hesabu 33:36

Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapanga katika nyika ya Sini (ni Kadeshi).

Hesabu 33:37

Wakasafiri kutoka Kadeshi wakapanga katika mlima wa Hori, katika mpaka wa nchi ya Edomu,

Hesabu 33:38

Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya Bwana, akafa hapo, katika mwaka wa arobaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi.

Hesabu 33:39

Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia na ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori.

Hesabu 33:40

Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli.

Hesabu 33:41

Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapanga Salmona.

Hesabu 33:42

Wakasafiri kutoka Salmona, wakapanga Punoni.

Hesabu 33:43

Wakasafiri kutoka Punoni, wakapanga Obothi.

Hesabu 33:44

Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika mpaka wa Moabu.

Hesabu 33:45

Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapanga Dibon-gadi.

Hesabu 33:46

Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapanga Almon-diblathaimu.

Hesabu 33:47

Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapanga katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo.

Hesabu 33:48

Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapanga katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko.

Hesabu 33:49

Wakapanga karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikilia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu.

Hesabu 33:50

Kisha Bwana akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia,

Hesabu 33:51

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani,

Hesabu 33:52

ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja-vunja mahali pao pote palipoinuka;

Hesabu 33:53

nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki.

Hesabu 33:54

Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali po pote kura itakapomwangukia mtu ye yote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo.

Hesabu 33:55

Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.

Hesabu 33:56

Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi.