Hesabu Mlango 2 Numbers

Hesabu 2:1

Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

Hesabu 2:2

Wana wa Israeli watapanga kila mtu penye beramu yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakakopanga kwa kuizunguka pande zote.

Hesabu 2:3

Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa beramu ya marago ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.

Hesabu 2:4

Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa sabini na nne elfu na mia sita.

Hesabu 2:5

Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Isakari; na mkuu wa wana wa Isakari atakuwa Nethaneli mwana wa Suari;

Hesabu 2:6

na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na nne elfu na mia nne;

Hesabu 2:7

na kabila ya Zabuloni; na mkuu wa wana wa Zabuloni atakuwa Eliabu mwana wa Heloni;

Hesabu 2:8

na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na saba elfu na mia nne.

Hesabu 2:9

Hao wote waliohesabiwa katika marago ya Yuda walikuwa mia na themanini na sita elfu na mia nne, kwa majeshi yao. Hao ndio watakaosafiri mbele.

Hesabu 2:10

Upande wa kusini kutakuwa na beramu ya marago ya Reubeni kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Reubeni atakuwa Elisuri mwana wa Shedeuri.

Hesabu 2:11

Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na sita elfu na mia tano.

Hesabu 2:12

Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Simeoni; na mkuu wa wana wa Simeoni atakuwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai;

Hesabu 2:13

na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na kenda elfu na mia tatu;

Hesabu 2:14

na kabila ya Gadi; na mkuu wa wana wa Gadi atakuwa Eliasafu mwana wa Deueli;

Hesabu 2:15

na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita na hamsini.

Hesabu 2:16

Wote waliohesabiwa katika marago ya Reubeni walikuwa mia na hamsini na moja elfu na mia nne na hamsini, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaosafiri mahali pa pili.

Hesabu 2:17

Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na marago ya Walawi katikati ya marago yote; kama wapangavyo marago, watasafiri vivyo, kila mtu mahali pake, penye beramu zao.

Hesabu 2:18

Upande wa magharibi kutakuwa na beramu ya marago ya Efraimu kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Efraimu atakuwa Elishama mwana wa Amihudi.

Hesabu 2:19

Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini elfu na mia tano.

Hesabu 2:20

Na karibu naye itakuwa kabila ya Manase; na mkuu wa wana wa Manase atakuwa Gamalieli mwana wa Pedasuri;

Hesabu 2:21

na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa thelathini na mbili elfu na mia mbili;

Hesabu 2:22

tena kabila ya Benyamini; na mkuu wa wana wa Benyamini atakuwa Abidani mwana wa Gideoni;

Hesabu 2:23

na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa thelathini na tano elfu na mia nne.

Hesabu 2:24

Wote waliohesabiwa katika marago ya Efraimu walikuwa mia na nane elfu na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaosafiri katika mahali pa tatu.

Hesabu 2:25

Upande wa kaskazini kutakuwa na beramu ya marago ya Dani kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Dani atakuwa Ahiezeri mwana wa Amishadai.

Hesabu 2:26

Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na mbili elfu na mia saba.

Hesabu 2:27

Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Asheri; na mkuu wa wana wa Asheri atakuwa Pagieli mwana wa Okrani;

Hesabu 2:28

na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na moja elfu na mia tano;

Hesabu 2:29

kisha kabila ya Naftali; na mkuu wa wana wa Naftali atakuwa Ahira mwana wa Enani;

Hesabu 2:30

na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na tatu elfu na mia nne.

Hesabu 2:31

Wote waliohesabiwa katika marago ya Dani walikuwa mia na hamsini na saba elfu na mia sita. Hao ndio watakaosafiri mwisho kwa kuandama beramu zao.

Hesabu 2:32

Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa nyumba za baba zao; wote waliohesabiwa katika marago kwa majeshi yao, walikuwa mia sita na tatu elfu na mia tano na hamsini.

Hesabu 2:33

Lakini Walawi hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli; kama Bwana alivyomwagiza Musa.

Hesabu 2:34

Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote Bwana aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyopanga penye beramu zao, na ndivyo walivyosafiri, kila mtu kwa jamaa zao, kwa nyumba za baba zao.