Hesabu BSB

Hesabu 34

Numbers Chapter 34

1
Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
Then the LORD said to Moses,
2
Waagize wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi ya Kanaani, (hii ndiyo nchi itakayowaangukia kuwa urithi, maana, hiyo nchi ya Kanaani kama mipaka yake ilivyo,)
“Command the Israelites and say to them: When you enter the land of Canaan, it will be allotted to you as an inheritance with these boundaries:
3
ndipo upande wenu wa kusini utakuwa tangu bara ya Sini kupita kando ya Edomu, na mpaka wenu wa kusini utakuwa tangu mwisho wa Bahari ya Chumvi kuelekea mashariki;
Your southern border will extend from the Wilderness of Zin along the border of Edom. On the east, your southern border will run from the end of the Salt Sea,
4
kisha mpaka wenu utageuka kwenda upande wa kusini wa kukwelea kwake Akrabimu, kisha kupita kwendelea Sini; na kutokea kwake kutakuwa kuelekea upande wa kusini wa Kadesh-barnea; kisha utaendelea mpaka Hasar-adari, na kufikilia Azmoni;
cross south of the Ascent of Akrabbim, continue to Zin, and go south of Kadesh-barnea. Then it will go on to Hazar-addar and proceed to Azmon,
5
kisha mpaka utageuka kutoka Azmoni kwendelea kijito cha Misri, na kutokea kwake kutakuwa hapo baharini.
where it will turn from Azmon, join the Brook of Egypt, and end at the Sea.
6
Kisha mpaka wenu wa upande wa magharibi mtakuwa na bahari kubwa na mpaka wake; hii ndiyo mpaka wenu upande wa magharibi.
Your western border will be the coastline of the Great Sea; this will be your boundary on the west.
7
Kisha mpaka wenu wa upande wa kaskazini utakuwa ni huu; kutoka bahari kubwa mtajiandikia mlima wa Hori;
Your northern border will run from the Great Sea directly to Mount Hor,
8
na kutoka mlima wa Hori mtaandika mpaka kuingilia kwake Hamathi; na kutokea kwake mpaka kutakuwa hapo Sedada;
and from Mount Hor to Lebo-hamath, then extend to Zedad,
9
tena mpaka utatokea hata Zifroni, na kutokea kwake kutakuwa hapo Hasarenani; huo ndio mpaka wenu wa upande wa kaskazini.
continue to Ziphron, and end at Hazar-enan. This will be your boundary on the north.
10
Kisha mtaandika mpaka wenu wa upande wa mashariki kutoka Hasarenani hata Shefamu;
And your eastern border will run straight from Hazar-enan to Shepham,
11
kisha mpaka utatelemka kutoka Shefamu mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mpaka utatelemka na kufikilia upande wa bahari ya Kinerethi upande wa mashariki;
then go down from Shepham to Riblah on the east side of Ain and continue along the slopes east of the Sea of Chinnereth.
12
kisha mpaka utatelemkia Yordani, na kutokea kwake kutakuwa hapo katika Bahari ya Chumvi; hii ndiyo nchi yenu kama mipaka yake ilivyo kuizunguka pande zote.
Then the border will go down along the Jordan and end at the Salt Sea. This will be your land, defined by its borders on all sides.”
13
Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo Bwana ameagiza wapewe watu wa zile kabila kenda, na nusu ya kabila;
So Moses commanded the Israelites, “Apportion this land by lot as an inheritance. The LORD has commanded that it be given to the nine and a half tribes.
14
kwa kuwa kabila ya wana wa Reubeni kwa nyumba za baba zao, na kabila ya wana wa Gadi kwa nyumba za baba zao, wamekwisha pata, na hiyo nusu ya kabila ya Manase wamekwisha pata urithi wao;
For the tribes of the Reubenites and Gadites, along with the half-tribe of Manasseh, have already received their inheritance.
15
hizo kabila mbili na nusu ya kabila wamekwisha pata urithi wao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo Yeriko, upande wa mashariki, kuelekea maawio ya jua.
These two and a half tribes have received their inheritance across the Jordan from Jericho, toward the sunrise.”
16
Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
Then the LORD said to Moses,
17
Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia nchi iwe urithi wenu; Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni.
“These are the names of the men who are to assign the land as an inheritance for you: Eleazar the priest and Joshua son of Nun.
18
Kisha mtamtwaa mkuu mmoja wa kila kabila, ili waigawanye nchi iwe urithi wenu.
Appoint one leader from each tribe to distribute the land.
19
Na majina ya watu hao ni haya; katika kabila ya Yuda, ni Kalebu mwana wa Yefune.
These are their names: Caleb son of Jephunneh from the tribe of Judah;
20
Na katika kabila ya wana wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
Shemuel son of Ammihud from the tribe of Simeon;
21
Katika kabila ya Benyamini, ni Elidadi mwana wa Kisloni.
Elidad son of Chislon from the tribe of Benjamin;
22
Na katika kabila ya wana wa Dani, mkuu, Buki mwana wa Yogli.
Bukki son of Jogli, a leader from the tribe of Dan;
23
Katika wana wa Yusufu; katika kabila ya wana wa Manase, mkuu, Hanieli mwana wa Efodi;
Hanniel son of Ephod, a leader from the tribe of Manasseh son of Joseph;
24
na katika kabila ya wana wa Efraimu, mkuu, Kemueli mwana wa Shiftani.
Kemuel son of Shiphtan, a leader from the tribe of Ephraim;
25
Na katika kabila ya wana wa Zabuloni, mkuu, Elisafani mwana wa Parnaki.
Eli-zaphan son of Parnach, a leader from the tribe of Zebulun;
26
Na katika kabila ya wana wa Isakari, mkuu, Paltieli mwana wa Azani.
Paltiel son of Azzan, a leader from the tribe of Issachar;
27
Na katika kabila ya wana wa Asheri, mkuu, Ahihudi mwana wa Shelomi.
Ahihud son of Shelomi, a leader from the tribe of Asher;
28
Na katika kabila ya wana wa Naftali, mkuu, Pedaheli mwana wa Amihudi.
and Pedahel son of Ammihud, a leader from the tribe of Naphtali.”
29
Hao ndio Bwana aliowaagiza wawagawanyie urithi wana wa Israeli katika nchi ya Kanaani.
These are the ones whom the LORD commanded to apportion the inheritance to the Israelites in the land of Canaan.

Chagua Sura