Hesabu 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 6 (Swahili) Numbers 6 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 6:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mtu mume au mtu mke atakapoweka nadhiri kubwa, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa Bwana; Hesabu 6:2

"Speak to the children of Israel, and tell them: When either man or woman shall make a special vow, the vow of a Nazirite, to separate himself to Yahweh,

atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka. Hesabu 6:3

he shall separate himself from wine and strong drink. He shall drink no vinegar of wine, or vinegar of fermented drink, neither shall he drink any juice of grapes, nor eat fresh grapes or dried.

Siku zote za kujitenga kwake asile kitu cho chote kilichoandaliwa kwa mzabibu, tangu kokwa hata maganda. Hesabu 6:4

All the days of his separation he shall eat nothing that is made of the grapevine, from the seeds even to the skins.

Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa Bwana, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu. Hesabu 6:5

"All the days of his vow of separation there shall no razor come on his head, until the days are fulfilled, in which he separates himself to Yahweh. He shall be holy. He shall let the locks of the hair of his head grow long.

Siku hizo zote ambazo alijiweka awe wa Bwana asikaribie maiti. Hesabu 6:6

"All the days that he separates himself to Yahweh he shall not go near a dead body.

Hatajitia unajisi kwa ajili ya baba yake, wala kwa ajili ya mamaye, wala kwa nduguye mume, wala kwa umbu lake, wakifa wao; kwa sababu ya huku kujiweka kwa Mungu ni juu ya kichwa chake. Hesabu 6:7

He shall not make himself unclean for his father, or for his mother, for his brother, or for his sister, when they die; because his separation to God is on his head.

Siku zote za kujitenga kwake, yeye ni mtakatifu kwa Bwana Hesabu 6:8

All the days of his separation he is holy to Yahweh.

Na kama mtu ye yote akifa ghafla karibu naye, akajitia unajisi kichwa cha kutengwa kwake, ndipo atakinyoa kichwa siku hiyo ya kutakaswa kwake, atakinyoa siku ya saba. Hesabu 6:9

"If any man dies very suddenly beside him, and he defiles the head of his separation; then he shall shave his head in the day of his cleansing. On the seventh day he shall shave it.

Tena siku ya nane ataleta hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, aende nao kwa kuhani, hata mlangoni pa hema ya kukutania; Hesabu 6:10

On the eighth day he shall bring two turtledoves or two young pigeons to the priest, to the door of the Tent of Meeting.

naye kuhani atasongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa sababu aliingia kosani kwa ajili ya mfu, naye atatakasa kichwa chake siku iyo hiyo. Hesabu 6:11

The priest shall offer one for a sin offering, and the other for a burnt offering, and make atonement for him, because he sinned by reason of the dead, and shall make his head holy that same day.

Kisha ataziweka kwa Bwana hizo siku za kujitenga kwake, naye ataleta mwana-kondoo mume wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya hatia; lakini hizo siku za kwanza hazitahesabiwa, kwa kuwa kule kujitenga kwake kulitiwa unajisi. Hesabu 6:12

He shall separate to Yahweh the days of his separation, and shall bring a male lamb a year old for a trespass offering; but the former days shall be void, because his separation was defiled.

Na sheria ya Mnadhiri ni hii, zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake; ataletwa mlangoni pa hema ya kukutania; Hesabu 6:13

"This is the law of the Nazirite: when the days of his separation are fulfilled, he shall be brought to the door of the Tent of Meeting,

naye atasongeza sadaka yake kwa Bwana, mwana-kondoo mmoja mume wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya kuteketezwa, na mwana-kondoo mmoja mke wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume mmoja mkamilifu kwa sadaka ya amani, Hesabu 6:14

and he shall offer his offering to Yahweh, one male lamb a year old without blemish for a burnt offering, and one ewe lamb a year old without blemish for a sin offering, and one ram without blemish for peace offerings,

na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, mikate ya unga mwembamba iliyokandwa kwa mafuta, na mikate ya kaki isiyochachwa, iliyotiwa mafuta, pamoja na sadaka zake za unga, na sadaka zake za kinywaji. Hesabu 6:15

and a basket of unleavened bread, cakes of fine flour mixed with oil, and unleavened wafers anointed with oil, and their meal offering, and their drink offerings.

Na kuhani atavisongeza mbele za Bwana, naye atasongeza sadaka yake ya dhambi, na sadaka yake ya kuteketezwa; Hesabu 6:16

The priest shall present them before Yahweh, and shall offer his sin offering, and his burnt offering.

naye atamsongeza huyo kondoo mume kuwa dhabihu ya sadaka za amani kwa Bwana, pamoja na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu; kisha kuhani atasongeza sadaka ya unga nayo, na sadaka yake ya kinywaji. Hesabu 6:17

He shall offer the ram for a sacrifice of peace offerings to Yahweh, with the basket of unleavened bread. The priest shall offer also its meal offering, and its drink offering.

Naye Mnadhiri atakinyoa kichwa cha kujitenga kwake, mlangoni pa hema ya kukutania, kisha atatwaa hizo nywele za kichwa cha kujitenga kwake, na kuzitia katika moto ulio chini ya dhabihu ya sadaka za amani. Hesabu 6:18

The Nazirite shall shave the head of his separation at the door of the Tent of Meeting, and shall take the hair of the head of his separation, and put it on the fire which is under the sacrifice of peace offerings.

Kisha kuhani atautwaa mkono wa huyo kondoo mume uliotokoswa, na mkate mmoja usio chachu atautwaa kikapuni, na mkate mmoja wa kaki, naye ataitia mikononi mwa yule Mnadhiri, baada ya kunyoa kichwa cha kujitenga kwake; Hesabu 6:19

The priest shall take the boiled shoulder of the ram, and one unleavened cake out of the basket, and one unleavened wafer, and shall put them on the hands of the Nazirite, after he has shaved the head of his separation;

naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana; kitu hicho ni kitakatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa, na paja la kuinuliwa; kisha baadaye Mnadhiri ana ruhusa kunywa divai. Hesabu 6:20

and the priest shall wave them for a wave offering before Yahweh. This is holy for the priest, together with the breast that is waved and the thigh that is offered. After that the Nazirite may drink wine.

Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea Bwana kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekayo ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuiandama sheria ya kujitenga kwake. Hesabu 6:21

"This is the law of the Nazirite who vows, and of his offering to Yahweh for his separation, besides that which he is able to get. According to his vow which he vows, so he must do after the law of his separation."

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 6:22

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia; Hesabu 6:23

"Speak to Aaron and to his sons, saying, 'This is how you shall bless the children of Israel.' You shall tell them,

Bwana akubarikie, na kukulinda; Hesabu 6:24

'Yahweh bless you, and keep you.

Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Hesabu 6:25

Yahweh make his face to shine on you, And be gracious to you.

Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani. Hesabu 6:26

Yahweh lift up his face toward you, And give you peace.'

Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia. Hesabu 6:27

"So they shall put my name on the children of Israel; and I will bless them."