2 Mambo ya Nyakati 29 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 29 (Swahili) 2nd Chronicles 29 (English)

Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na kenda; na jina la mamaye aliitwa Abiya binti Zekaria. 2 Mambo ya Nyakati 29:1

Hezekiah began to reign when he was twenty-five years old; and he reigned twenty-nine years in Jerusalem: and his mother's name was Abijah, the daughter of Zechariah.

Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Daudi babaye. 2 Mambo ya Nyakati 29:2

He did that which was right in the eyes of Yahweh, according to all that David his father had done.

Yeye, katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, katika mwezi wa kwanza, aliifungua milango ya nyumba ya Bwana, akaitengeneza. 2 Mambo ya Nyakati 29:3

He in the first year of his reign, in the first month, opened the doors of the house of Yahweh, and repaired them.

Akawaingiza makuhani na Walawi, akawakusanya uwandani upande wa mashariki, 2 Mambo ya Nyakati 29:4

He brought in the priests and the Levites, and gathered them together into the broad place on the east,

akawaambia, Nisikieni, enyi Walawi; jitakaseni nafsi zenu sasa, mkaitakase na nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zenu, mkautoe uchafu katika patakatifu. 2 Mambo ya Nyakati 29:5

and said to them, Hear me, you Levites; now sanctify yourselves, and sanctify the house of Yahweh, the God of your fathers, and carry forth the filthiness out of the holy place.

Kwa maana baba zetu wameasi, na kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wetu, wamemwacha, na kugeuzia mbali nyuso zao na makao ya Bwana, na kumpa maungo. 2 Mambo ya Nyakati 29:6

For our fathers have trespassed, and done that which was evil in the sight of Yahweh our God, and have forsaken him, and have turned away their faces from the habitation of Yahweh, and turned their backs.

Tena wameifunga milango ya ukumbi, na kuzizima taa, wala hawakufukiza uvumba, wala hawakumtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa katika patakatifu. 2 Mambo ya Nyakati 29:7

Also they have shut up the doors of the porch, and put out the lamps, and have not burned incense nor offered burnt offerings in the holy place to the God of Israel.

Kwa hiyo hasira ya Bwana imekuwa juu ya Yuda na Yerusalemu, naye amewatoa kuwa matetemeko, wawe ushangao, na mazomeo, kama mwonavyo kwa macho yenu. 2 Mambo ya Nyakati 29:8

Therefore the wrath of Yahweh was on Judah and Jerusalem, and he has delivered them to be tossed back and forth, to be an astonishment, and a hissing, as you see with your eyes.

Kwa kuwa, tazama, baba zetu wameangamia kwa upanga, na wana wetu, na binti zetu, na wake zetu wametekwa kwa ajili ya hayo. 2 Mambo ya Nyakati 29:9

For, behold, our fathers have fallen by the sword, and our sons and our daughters and our wives are in captivity for this.

Basi nia yangu ni kufanya agano na Bwana, Mungu wa Israeli, ili kwamba hasira yake kali itugeukie mbali. 2 Mambo ya Nyakati 29:10

Now it is in my heart to make a covenant with Yahweh, the God of Israel, that his fierce anger may turn away from us.

Basi wanangu, msijipurukushe sasa, kwa kuwa Bwana amewachagua ninyi msimame mbele yake, kumhudumia, nanyi mpate kuwa watumishi wake, mkafukize uvumba. 2 Mambo ya Nyakati 29:11

My sons, don't be negligent now; for Yahweh has chosen you to stand before him, to minister to him, and that you should be his ministers, and burn incense.

Ndipo wakaondoka Walawi, Mahathi mwana wa Amasai, na Yoeli mwana wa Azaria, wa wana wa Wakohathi; na wa wana wa Merari, Kishi mwana wa Abdi, na Azaria mwana wa Yehaleleli; na wa Wagershoni, Yoa mwana wa Zima na Edeni mwana wa Yoa; 2 Mambo ya Nyakati 29:12

Then the Levites arose, Mahath, the son of Amasai, and Joel the son of Azariah, of the sons of the Kohathites; and of the sons of Merari, Kish the son of Abdi, and Azariah the son of Jehallelel; and of the Gershonites, Joah the son of Zimmah, and Eden the son of Joah;

na wa wana wa Elisafani, Shimri na Yeueli; na wa wana wa Asafu, Zekaria na Matania; 2 Mambo ya Nyakati 29:13

and of the sons of Elizaphan, Shimri and Jeuel; and of the sons of Asaph, Zechariah and Mattaniah;

na wa wana wa Hemani, Yehueli na Shimei; na wa wana wa Yeduthuni, Shemaya na Uzieli. 2 Mambo ya Nyakati 29:14

and of the sons of Heman, Jehuel and Shimei; and of the sons of Jeduthun, Shemaiah and Uzziel.

Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa, wakaingia, kama alivyoamuru mfalme kwa maneno ya Bwana, ili waisafishe nyumba ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 29:15

They gathered their brothers, and sanctified themselves, and went in, according to the commandment of the king by the words of Yahweh, to cleanse the house of Yahweh.

Nao makuhani wakaingia nyumbani mwa Bwana, katika mahali pa ndani, ili waisafishe, wakatoa uchafu wote waliouona hekaluni mwa Bwana, wakautupa nje uani mwa nyumba ya Bwana. Walawi wakautwaa, ili wauchukue nje mpaka kijito cha Kidroni. 2 Mambo ya Nyakati 29:16

The priests went in to the inner part of the house of Yahweh, to cleanse it, and brought out all the uncleanness that they found in the temple of Yahweh into the court of the house of Yahweh. The Levites took it, to carry it out abroad to the brook Kidron.

Basi wakaanza kutakasa siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, hata siku ya nane ya mwezi wakafika katika ukumbi wa Bwana; wakaitakasa nyumba ya Bwana katika muda wa siku nane; wakamaliza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza. 2 Mambo ya Nyakati 29:17

Now they began on the first [day] of the first month to sanctify, and on the eighth day of the month came they to the porch of Yahweh; and they sanctified the house of Yahweh in eight days: and on the sixteenth day of the first month they made an end.

Wakaingia ndani kwa Hezekia mfalme, wakasema, Tumeisafisha nyumba yote ya Bwana, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, pamoja na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate ya wonyesho, pamoja na vyombo vyake vyote. 2 Mambo ya Nyakati 29:18

Then they went in to Hezekiah the king within [the palace], and said, We have cleansed all the house of Yahweh, and the altar of burnt offering, with all the vessels of it, and the table of show bread, with all the vessels of it.

Tena vyombo vyote alivyovitupa mfalme Ahazi alipotawala, hapo alipoasi, tumevitengeza na kuvitakasa; navyo, tazama, vipo mbele ya madhabahu ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 29:19

Moreover all the vessels, which king Ahaz in his reign did cast away when he trespassed, have we prepared and sanctified; and, behold, they are before the altar of Yahweh.

Ndipo Hezekia mfalme akaamka mapema, akakusanya wakuu wa mji, akapanda nyumbani kwa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 29:20

Then Hezekiah the king arose early, and gathered the princes of the city, and went up to the house of Yahweh.

Wakaleta ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba, na wana-kondoo saba, na mabeberu saba, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, na kwa ajili ya patakatifu, na kwa ajili ya Yuda. Akaamuru makuhani, wana wa Haruni, wawatoe madhabahuni pa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 29:21

They brought seven bulls, and seven rams, and seven lambs, and seven male goats, for a sin-offering for the kingdom and for the sanctuary and for Judah. He commanded the priests the sons of Aaron to offer them on the altar of Yahweh.

Basi wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu, wakainyunyiza madhabahuni; wakawachinja kondoo waume, na kuinyunyiza damu madhabahuni; wakawachinja na wana-kondoo, na kuinyunyiza damu madhabahuni. 2 Mambo ya Nyakati 29:22

So they killed the bulls, and the priests received the blood, and sprinkled it on the altar: and they killed the rams, and sprinkled the blood on the altar: they killed also the lambs, and sprinkled the blood on the altar.

Wakawaleta karibu mabeberu wa sadaka ya dhambi mbele ya mfalme na kusanyiko; wakawawekea mikono yao; 2 Mambo ya Nyakati 29:23

They brought near the male goats for the sin-offering before the king and the assembly; and they laid their hands on them:

na makuhani wakawachinja, wakaitoa damu yao kuwa sadaka ya dhambi madhabahuni, ili kuwafanyia Israeli wote upatanisho; maana mfalme aliamuru Israeli wote wafanyiwe sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya dhambi. 2 Mambo ya Nyakati 29:24

and the priests killed them, and they made a sin-offering with their blood on the altar, to make atonement for all Israel; for the king commanded [that] the burnt offering and the sin-offering [should be made] for all Israel.

Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa Bwana wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani Bwana aliamuru hivi kwa manabii wake. 2 Mambo ya Nyakati 29:25

He set the Levites in the house of Yahweh with cymbals, with psalteries, and with harps, according to the commandment of David, and of Gad the king's seer, and Nathan the prophet; for the commandment was of Yahweh by his prophets.

Wakasimama Walawi wenye vinanda vya Daudi, na makuhani wenye mapanda. 2 Mambo ya Nyakati 29:26

The Levites stood with the instruments of David, and the priests with the trumpets.

Hezekia akaamuru kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Na wakati ilipoanza sadaka hiyo ya kuteketezwa, ukaanza na huo wimbo wa Bwana, na mapanda, pamoja na vinanda vya Daudi mfalme wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 29:27

Hezekiah commanded to offer the burnt offering on the altar. When the burnt offering began, the song of Yahweh began also, and the trumpets, together with the instruments of David king of Israel.

Na kusanyiko lote wakaabudu, waimbaji wakaimba, wenye mapanda wakapiga; haya yote yakaendelea hata ilipomalizika sadaka ya kuteketezwa. 2 Mambo ya Nyakati 29:28

All the assembly worshiped, and the singers sang, and the trumpeters sounded; all this [continued] until the burnt offering was finished.

Hata walipokwisha kutoa sadaka, mfalme, na hao wote waliokuwapo naye, wakasujudia, wakaabudu. 2 Mambo ya Nyakati 29:29

When they had made an end of offering, the king and all who were present with him bowed themselves and worshiped.

Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie Bwana sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama vichwa, wakaabudu. 2 Mambo ya Nyakati 29:30

Moreover Hezekiah the king and the princes commanded the Levites to sing praises to Yahweh with the words of David, and of Asaph the seer. They sang praises with gladness, and they bowed their heads and worshiped.

Ndipo Hezekia akajibu, akasema, Sasa mmejifanya wakfu kwa Bwana, karibuni mkalete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa Bwana. Basi kusanyiko wakaleta dhabihu na matoleo ya shukrani; na wote wenye moyo wa ukarimu, wakaleta sadaka za kuteketezwa. 2 Mambo ya Nyakati 29:31

Then Hezekiah answered, Now you have consecrated yourselves to Yahweh; come near and bring sacrifices and thank-offerings into the house of Yahweh. The assembly brought in sacrifices and thank-offerings; and as many as were of a willing heart [brought] burnt offerings.

Na hesabu ya sadaka hizo za kuteketezwa walizozileta kusanyiko ikawa ng'ombe waume sabini, kondoo waume mia, na wana-kondoo mia mbili; hao wote walikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 29:32

The number of the burnt offerings which the assembly brought was seventy bulls, one hundred rams, and two hundred lambs: all these were for a burnt offering to Yahweh.

Na vitu vitakatifu vilikuwa ng'ombe mia sita, na kondoo elfu tatu. 2 Mambo ya Nyakati 29:33

The consecrated things were six hundred oxen and three thousand sheep.

Lakini makuhani walikuwa wachache, wasiweze kuchuna sadaka zote za kuteketezwa; basi ndugu zao Walawi wakawasaidia, hata ilipokwisha kazi, na hata makuhani walipojitakasa; kwa kuwa Walawi walikuwa wenye mioyo ya adili kwa kujitakasa kuliko makuhani. 2 Mambo ya Nyakati 29:34

But the priests were too few, so that they could not flay all the burnt offerings: therefore their brothers the Levites helped them, until the work was ended, and until the priests had sanctified themselves; for the Levites were more upright in heart to sanctify themselves than the priests.

Na tena sadaka za kuteketezwa nazo zilikuwa nyingi, pamoja na mafuta ya sadaka za amani, na sadaka za kinywaji kwa kila sadaka ya kuteketezwa. Hivyo ikatengezeka huduma ya nyumba ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 29:35

Also the burnt offerings were in abundance, with the fat of the peace-offerings, and with the drink-offerings for every burnt offering. So the service of the house of Yahweh was set in order.

Akafurahi Hezekia, na watu wote, kwa sababu ya hayo Mungu aliyowatengenezea watu; maana jambo hilo likawa kwa ghafula. 2 Mambo ya Nyakati 29:36

Hezekiah rejoiced, and all the people, because of that which God had prepared for the people: for the thing was done suddenly.