2 Mambo ya Nyakati 31 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 31 (Swahili) 2nd Chronicles 31 (English)

Basi hayo yote yalipokwisha, wakatoka Israeli wote waliokuwako waende miji ya Yuda, wakazivunja-vunja nguzo, wakayakata-kata maashera, wakabomoa mahali pa juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, katika Efraimu pia na Manase, hata walipokwisha kuviharibu vyote. Ndipo wana wa Israeli wote wakarudi, kila mtu kwa milki yake, mijini kwao. 2 Mambo ya Nyakati 31:1

Now when all this was finished, all Israel who were present went out to the cities of Judah, and broke in pieces the pillars, and hewed down the Asherim, and broke down the high places and the altars out of all Judah and Benjamin, in Ephraim also and Manasseh, until they had destroyed them all. Then all the children of Israel returned, every man to his possession, into their own cities.

Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa matuo ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 31:2

Hezekiah appointed the divisions of the priests and the Levites after their divisions, every man according to his service, both the priests and the Levites, for burnt offerings and for peace-offerings, to minister, and to give thanks, and to praise in the gates of the camp of Yahweh.

Tena akaweka sehemu ya mfalme ya mali zake kwa sadaka za kuteketezwa, yaani, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa za sabato, na za mwezi mpya, na sikukuu, kama ilivyoandikwa katika torati ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 31:3

[He appointed] also the king's portion of his substance for the burnt-offerings, [to wit], for the morning and evening burnt offerings, and the burnt offerings for the Sabbaths, and for the new moons, and for the set feasts, as it is written in the law of Yahweh.

Tena akawaamuru watu waliokaa Yerusalemu, watoe sehemu ya makuhani na Walawi, ili hao wajibidiishe katika torati ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 31:4

Moreover he commanded the people who lived in Jerusalem to give the portion of the priests and the Levites, that they might give themselves to the law of Yahweh.

Mara ilipotangaa amri, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, na divai, na mafuta, na asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta nyingi. 2 Mambo ya Nyakati 31:5

As soon as the commandment came abroad, the children of Israel gave in abundance the first fruits of grain, new wine, and oil, and honey, and of all the increase of the field; and the tithe of all things brought they in abundantly.

Nao wana wa Israeli na Yuda, waliokaa mijini mwa Yuda, wakaleta pia zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyowekewa Bwana, Mungu wao, wakaviweka chungu chungu. 2 Mambo ya Nyakati 31:6

The children of Israel and Judah, who lived in the cities of Judah, they also brought in the tithe of oxen and sheep, and the tithe of dedicated things which were consecrated to Yahweh their God, and laid them by heaps.

Katika mwezi wa tatu wakaanza kuweka misingi ya hizo chungu, wakazimaliza katika mwezi wa saba. 2 Mambo ya Nyakati 31:7

In the third month they began to lay the foundation of the heaps, and finished them in the seventh month.

Hata walipokuja Hezekia na wakuu, na kuziona zile chungu, wakamhimidi Bwana, na watu wake Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 31:8

When Hezekiah and the princes came and saw the heaps, they blessed Yahweh, and his people Israel.

Ndipo Hezekia akaulizana na makuhani na Walawi katika habari ya hizo chungu. 2 Mambo ya Nyakati 31:9

Then Hezekiah questioned the priests and the Levites concerning the heaps.

Azaria kuhani mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa Bwana, tumekula na kushiba, na kusaza tele; kwa kuwa Bwana amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa. 2 Mambo ya Nyakati 31:10

Azariah the chief priest, of the house of Zadok, answered him and said, Since [the people] began to bring the offerings into the house of Yahweh, we have eaten and had enough, and have left plenty: for Yahweh has blessed his people; and that which is left is this great store.

Ndipo Hezekia akaamuru kutengeneza vyumba nyumbani mwa Bwana; wakavitengeneza. 2 Mambo ya Nyakati 31:11

Then Hezekiah commanded to prepare chambers in the house of Yahweh; and they prepared them.

Wakayaingiza matoleo na zaka na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu; na juu yake Konania Mlawi alikuwa mkuu, na wa pili ni Shimei nduguye. 2 Mambo ya Nyakati 31:12

They brought in the offerings and the tithes and the dedicated things faithfully: and over them Conaniah the Levite was ruler, and Shimei his brother was second.

Na Yehieli, na Azaria, na Nahathi, na Asaheli, na Yerimothi, na Yozabadi, na Elieli, na Ismakia, na Mahathi, na Benaya, walikuwa wasimamizi chini ya mkono wa Konania na Shimei nduguye, kwa amri ya Hezekia mfalme, na Azaria mkuu wa nyumba ya Mungu. 2 Mambo ya Nyakati 31:13

Jehiel, and Azaziah, and Nahath, and Asahel, and Jerimoth, and Jozabad, and Eliel, and Ismachiah, and Mahath, and Benaiah, were overseers under the hand of Conaniah and Shimei his brother, by the appointment of Hezekiah the king, and Azariah the ruler of the house of God.

Na Kore, mwana wa Imna, Mlawi, bawabu wa mlango wa mashariki, alizisimamia sadaka za hiari za Mungu; ili kugawa matoleo ya Bwana, navyo vitu vilivyokuwa vitakatifu sana. 2 Mambo ya Nyakati 31:14

Kore the son of Imnah the Levite, the porter at the east [gate], was over the freewill-offerings of God, to distribute the offerings of Yahweh, and the most holy things.

Na chini yake walikuwa Edeni, na Minyamini, na Yeshua, na Shemaya, na Amaria, na Shekania, mijini mwa makuhani, kwa walivyoaminiwa, ili kuwagawia ndugu zao kwa zamu, wakuu na wadogo sawasawa; 2 Mambo ya Nyakati 31:15

Under him were Eden, and Miniamin, and Jeshua, and Shemaiah, Amariah, and Shecaniah, in the cities of the priests, in their office of trust, to give to their brothers by divisions, as well to the great as to the small:

zaidi ya wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wanaume, wenye miaka mitatu na zaidi, kila mmoja aliyeingia nyumbani mwa Bwana, kama ilivyopasa kazi ya kila siku, kwa huduma zao katika malinzi yao, kwa kadiri ya zamu zao; 2 Mambo ya Nyakati 31:16

besides those who were reckoned by genealogy of males, from three years old and upward, even everyone who entered into the house of Yahweh, as the duty of every day required, for their service in their offices according to their divisions;

na wale waliohesabiwa kwa nasaba ya makuhani kufuata nyumba za baba zao, na Walawi, wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, katika malinzi yao, kwa kadiri ya zamu zao; 2 Mambo ya Nyakati 31:17

and those who were reckoned by genealogy of the priests by their fathers' houses, and the Levites from twenty years old and upward, in their offices by their divisions;

na wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wadogo wao wote, wake zao, na wana wao, na binti zao, katika kusanyiko lote; kwani kwa vile walivyoaminiwa, wakajitakasa katika utakatifu; 2 Mambo ya Nyakati 31:18

and those who were reckoned by genealogy of all their little ones, their wives, and their sons, and their daughters, through all the congregation: for in their office of trust they sanctified themselves in holiness.

tena kwa ajili ya wana wa Haruni makuhani, waliokuwamo mashambani mwa malisho ya miji yao, mji kwa mji, kulikuwa na watu waliotajwa majina yao, ili kuwagawia sehemu wanaume wote miongoni mwa makuhani, na wote waliohesabiwa kwa nasaba miongoni mwa Walawi. 2 Mambo ya Nyakati 31:19

Also for the sons of Aaron the priests, who were in the fields of the suburbs of their cities, in every city, there were men who were mentioned by name, to give portions to all the males among the priests, and to all who were reckoned by genealogy among the Levites.

Na hivyo ndivyo alivyofanya Hezekia katika Yuda yote; akatenda yaliyo mema, na ya adili, na uaminifu, mbele za Bwana, Mungu wake. 2 Mambo ya Nyakati 31:20

Thus did Hezekiah throughout all Judah; and he worked that which was good and right and faithful before Yahweh his God.

Na katika kila kazi aliyoanza kwa utumishi wa nyumba ya Mungu, na kwa torati, na kwa amri, ili kumtafuta Mungu wake, aliifanya kwa moyo wake wote, akafanikiwa. 2 Mambo ya Nyakati 31:21

In every work that he began in the service of the house of God, and in the law, and in the commandments, to seek his God, he did it with all his heart, and prospered.