2 Mambo ya Nyakati 25 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 25 (Swahili) 2nd Chronicles 25 (English)

Amazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na kenda; na jina la mamaye aliitwa Yehoadani wa Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 25:1

Amaziah was twenty-five years old when he began to reign; and he reigned twenty-nine years in Jerusalem: and his mother's name was Jehoaddan, of Jerusalem.

Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, lakini si kwa moyo mkamilifu. 2 Mambo ya Nyakati 25:2

He did that which was right in the eyes of Yahweh, but not with a perfect heart.

Basi ikawa, alipopata nguvu katika ufalme wake, akawaua watumishi wale waliomwua mfalme babaye. 2 Mambo ya Nyakati 25:3

Now it happened, when the kingdom was established to him, that he killed his servants who had killed the king his father.

Lakini watoto wao hakuwaua, ila alifanya sawasawa na hayo yaliyoandikwa katika torati, katika kitabu cha Musa, kama Bwana alivyoamuru, akisema, Mababa wasife kwa makosa ya wana, wala wana wasife kwa makosa ya mababa; lakini kila mtu atakufa kwa dhambi yake mwenyewe. 2 Mambo ya Nyakati 25:4

But he didn't put their children to death, but did according to that which is written in the law in the book of Moses, as Yahweh commanded, saying, The fathers shall not die for the children, neither shall the children die for the fathers; but every man shall die for his own sin.

Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka sawasawa na nyumba za baba zao chini ya maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule mia tatu elfu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao. 2 Mambo ya Nyakati 25:5

Moreover Amaziah gathered Judah together, and ordered them according to their fathers' houses, under captains of thousands and captains of hundreds, even all Judah and Benjamin: and he numbered them from twenty years old and upward, and found them three hundred thousand chosen men, able to go forth to war, who could handle spear and shield.

Akaajiri pia watu mashujaa mia elfu wa Israeli kwa talanta mia za fedha. 2 Mambo ya Nyakati 25:6

He hired also one hundred thousand mighty men of valor out of Israel for one hundred talents of silver.

Lakini mtu wa Mungu akamjia, akasema, Ee mfalme, usiwaache jeshi la Israeli waende nawe; kwa kuwa Bwana hayupo pamoja na Israeli, yaani, wana wote wa Efraimu. 2 Mambo ya Nyakati 25:7

But there came a man of God to him, saying, O king, don't let the army of Israel go with you; for Yahweh is not with Israel, [to wit], with all the children of Ephraim.

Lakini ukitaka kwenda, haya, jitie nguvu upigane; Mungu atakuangusha mbele ya adui; maana Mungu anazo nguvu za kusaidia, na kuangusha. 2 Mambo ya Nyakati 25:8

But if you will go, do [valiantly], be strong for the battle: God will cast you down before the enemy; for God has power to help, and to cast down.

Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Bwana aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo. 2 Mambo ya Nyakati 25:9

Amaziah said to the man of God, But what shall we do for the hundred talents which I have given to the army of Israel? The man of God answered, Yahweh is able to give you much more than this.

Ndipo Amazia akawafarakisha jeshi lililomjia kutoka Efraimu, ili warudi kwao; kwa hiyo ikawaka sana hasira yao juu ya Yuda, nao wakarudi kwao wenye hasira kali. 2 Mambo ya Nyakati 25:10

Then Amaziah separated them, [to wit], the army that had come to him out of Ephraim, to go home again: therefore their anger was greatly kindled against Judah, and they returned home in fierce anger.

Amazia akapiga moyo konde, akawaongoza watu wake, akaenda mpaka Bonde la Chumvi, akawapiga katika wana wa Seiri watu elfu kumi. 2 Mambo ya Nyakati 25:11

Amaziah took courage, and led forth his people, and went to the Valley of Salt, and struck of the children of Seir ten thousand.

Na elfu kumi wengine, ambao wana wa Yuda waliwachukua wali hai, wakawaleta juu ya jabali, wakawaangusha toka juu ya jabali, hata wakavunjika-vunjika wote. 2 Mambo ya Nyakati 25:12

[other] ten thousand did the children of Judah carry away alive, and brought them to the top of the rock, and cast them down from the top of the rock, so that they all were broken in pieces.

Lakini wale watu wa jeshi, aliowarudisha Amazia, wasiende naye vitani, hao wakaiteka miji ya Yuda, tangu Samaria mpaka Beth-horoni, wakawapiga watu elfu tatu, wakachukua nyara nyingi. 2 Mambo ya Nyakati 25:13

But the men of the army whom Amaziah sent back, that they should not go with him to battle, fell on the cities of Judah, from Samaria even to Beth Horon, and struck of them three thousand, and took much spoil.

Basi ikawa, Amazia alipokwisha rudi kutoka kuwaua Waedomi, alileta miungu ya wana wa Seiri, akaisimamisha kuwa miungu yake, akajiinama mbele yao, akaifukizia uvumba. 2 Mambo ya Nyakati 25:14

Now it happened, after that Amaziah was come from the slaughter of the Edomites, that he brought the gods of the children of Seir, and set them up to be his gods, and bowed down himself before them, and burned incense to them.

Kwa hiyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Amazia, akampelekea nabii, aliyemwambia, Mbona umeitafuta miungu ya watu, isiyowaokoa watu wao mkononi mwako? 2 Mambo ya Nyakati 25:15

Therefore the anger of Yahweh was kindled against Amaziah, and he sent to him a prophet, who said to him, Why have you sought after the gods of the people, which have not delivered their own people out of your hand?

Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu. 2 Mambo ya Nyakati 25:16

It happened, as he talked with him, that [the king] said to him, Have we made you of the king's counsel? Stop! Why should you be struck down? Then the prophet stopped, and said, I know that God has determined to destroy you, because you have done this, and have not listened to my counsel.

Ndipo mfalme Amazia akafanya shauri, akatuma wajumbe kwa Yehoashi, mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu,mfalme wa Israeli,kusema,njoo,tutazamane uso kwa uso. 2 Mambo ya Nyakati 25:17

Then Amaziah king of Judah took advice, and sent to Joash, the son of Jehoahaz the son of Jehu, king of Israel, saying, Come, let us look one another in the face.

Na Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amazia mfalme wa Yuda, kusema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ukatuma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita hayawani aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti. 2 Mambo ya Nyakati 25:18

Joash king of Israel sent to Amaziah king of Judah, saying, The thistle that was in Lebanon sent to the cedar that was in Lebanon, saying, Give your daughter to my son as wife: and there passed by a wild animal that was in Lebanon, and trod down the thistle.

Wasema, Tazama, umewapiga Edomu; na moyo wako wakutukuza ujisifu; kaa nyumbani mwako basi; mbona unataka kujitia bure katika madhara, hata uanguke, wewe na Yuda pamoja nawe? 2 Mambo ya Nyakati 25:19

You say, Behold, you have struck Edom; and your heart lifts you up to boast: abide now at home; why should you meddle to [your] hurt, that you should fall, even you, and Judah with you?

Lakini Amazia hakutaka kusikia, kwa maana hayo yalitoka kwa Mungu, ili awatie mikononi mwao, kwa kuwa wameitafuta miungu ya Edomu. 2 Mambo ya Nyakati 25:20

But Amaziah would not hear; for it was of God, that he might deliver them into the hand [of their enemies], because they had sought after the gods of Edom.

Basi Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea; wakatazamana uso kwa uso, yeye na Amazia mfalme wa Yuda huko Beth-shemeshi, ulio wa Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 25:21

So Joash king of Israel went up; and he and Amaziah king of Judah looked one another in the face at Beth-shemesh, which belongs to Judah.

Yuda wakashindwa mbele ya Israeli; wakakimbia kila mtu hemani kwake. 2 Mambo ya Nyakati 25:22

Judah was put to the worse before Israel; and they fled every man to his tent.

Yehoashi mfalme wa Israeli akamtwaa Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-shemeshi,akamchukua mpaka Yerusalemu ,akauvunja ukuta wa Yerusalemu , toka lango la Efraimu mpaka lango la pembeni ,mikono mia nne. 2 Mambo ya Nyakati 25:23

Joash king of Israel took Amaziah king of Judah, the son of Joash the son of Jehoahaz, at Beth-shemesh, and brought him to Jerusalem, and broke down the wall of Jerusalem from the gate of Ephraim to the corner gate, four hundred cubits.

Akaitwaa dhahabu yote, na fedha, na vyombo vyote vilivyoonekana nyumbani mwa Mungu kwa Obed-edomu, na hazina za nyumba ya mfalme, tena watu kuwa amana, akarudi Samaria. 2 Mambo ya Nyakati 25:24

[He took] all the gold and silver, and all the vessels that were found in the house of God with Obed-edom, and the treasures of the king's house, the hostages also, and returned to Samaria.

Naye Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, akaishi baada ya kufa kwake Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli, miaka kumi na mitano. 2 Mambo ya Nyakati 25:25

Amaziah the son of Joash king of Judah lived after the death of Joash son of Jehoahaz king of Israel fifteen years.

Na mambo yote ya Amazia yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, tazama, je! Hayakuandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli? 2 Mambo ya Nyakati 25:26

Now the rest of the acts of Amaziah, first and last, behold, aren't they written in the book of the kings of Judah and Israel?

Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata Bwana, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko. 2 Mambo ya Nyakati 25:27

Now from the time that Amaziah did turn away from following Yahweh they made a conspiracy against him in Jerusalem; and he fled to Lachish: but they sent after him to Lachish, and killed him there.

Wakamleta juu ya farasi; wakamzika pamoja na babaze katika mji wa Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 25:28

They brought him on horses, and buried him with his fathers in the city of Judah.