2 Mambo ya Nyakati 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 16 (Swahili) 2nd Chronicles 16 (English)

Katika mwaka wa thelathini na sita wa kutawala kwake Asa, Baasha mfalme wa Israeli akapanda juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu ye yote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 16:1

In the six and thirtieth year of the reign of Asa, Baasha king of Israel went up against Judah, and built Ramah, that he might not allow anyone to go out or come in to Asa king of Judah.

Ndipo Asa akatoa fedha na dhahabu katika hazina za nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, akampelekea Ben-hadadi mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema, 2 Mambo ya Nyakati 16:2

Then Asa brought out silver and gold out of the treasures of the house of Yahweh and of the king's house, and sent to Ben Hadad king of Syria, who lived at Damascus, saying,

Kwangu na kwako na liwe agano kama lilivyokuwa kwa baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea fedha na dhahabu; basi, uvunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili aniondokee mimi. 2 Mambo ya Nyakati 16:3

[There is] a league between me and you, as [there was] between my father and your father: behold, I have sent you silver and gold; go, break your league with Baasha king of Israel, that he may depart from me.

Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawapeleka maakida wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli; wakapiga Iyoni, na Dani, na Abel-maimu, na miji ya hazina yote ya Naftali. 2 Mambo ya Nyakati 16:4

Ben Hadad listened to king Asa, and sent the captains of his armies against the cities of Israel; and they struck Ijon, and Dan, and Abel Maim, and all the store-cities of Naphtali.

Ikawa Baasha aliposikia habari hiyo, akaacha kuujenga Rama, akaikomesha kazi yake. 2 Mambo ya Nyakati 16:5

It happened, when Baasha heard of it, that he left off building Ramah, and let his work cease.

Ndipo mfalme Asa akawatwaa Yuda wote; nao wakayachukua mawe ya Rama, na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye akajenga kwa vitu hivyo Geba na Mispa. 2 Mambo ya Nyakati 16:6

Then Asa the king took all Judah; and they carried away the stones of Ramah, and the timber of it, with which Baasha had built; and he built therewith Geba and Mizpah.

Wakati ule Hanani mwonaji akamwendea Asa mfalme wa Yuda, akamwambia, Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala hukumtegemea Bwana, Mungu wako, kwa hiyo limeokoka jeshi la mfalme wa Shamu mkononi mwako. 2 Mambo ya Nyakati 16:7

At that time Hanani the seer came to Asa king of Judah, and said to him, Because you have relied on the king of Syria, and have not relied on Yahweh your God, therefore is the host of the king of Syria escaped out of your hand.

Je! Hao Wakushi na Walubi hawakuwa jeshi kubwa mno, wenye magari na wapanda farasi wengi sana? Lakini, kwa kuwa ulimtegemea Bwana, aliwatia mkononi mwako. 2 Mambo ya Nyakati 16:8

Weren't the Ethiopians and the Lubim a huge host, with chariots and horsemen exceeding many? yet, because you did rely on Yahweh, he delivered them into your hand.

Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita. 2 Mambo ya Nyakati 16:9

For the eyes of Yahweh run back and forth throughout the whole earth, to show himself strong in the behalf of them whose heart is perfect toward him. Herein you have done foolishly; for from henceforth you shall have wars.

Ndipo Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia nyumbani mwa mkatale; maana amemghadhibikia kwa sababu ya neno hilo. Na Asa akawaonea baadhi ya watu wakati ule ule. 2 Mambo ya Nyakati 16:10

Then Asa was angry with the seer, and put him in the prison-house; for he was in a rage with him because of this thing. Asa oppressed some of the people at the same time.

Na tazama, mambo yake Asa, ya kwanza na ya mwisho, angalia, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 16:11

Behold, the acts of Asa, first and last, behold, they are written in the book of the kings of Judah and Israel.

Akashikwa Asa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta Bwana katika ugonjwa wake, bali waganga. 2 Mambo ya Nyakati 16:12

In the thirty-ninth year of his reign Asa was diseased in his feet; his disease was exceeding great: yet in his disease he didn't seek Yahweh, but to the physicians.

Asa akalala na babaze, akafa katika mwaka wa arobaini na mmoja wa kumiliki kwake. 2 Mambo ya Nyakati 16:13

Asa slept with his fathers, and died in the one and fortieth year of his reign.

Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakamfukizia mafukizo makuu sana.

2 Mambo ya Nyakati 16:14

They buried him in his own tombs, which he had hewn out for himself in the city of David, and laid him in the bed which was filled with sweet odors and various kinds [of spices] prepared by the perfumers' are: and they made a very great burning for him.