2 Mambo ya Nyakati 30 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 30 (Swahili) 2nd Chronicles 30 (English)

Hezekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda pia; akawaandikia nyaraka Efraimu na Manase, waje nyumbani kwa Bwana Yerusalemu, ili wamfanyie pasaka Bwana, Mungu wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 30:1

Hezekiah sent to all Israel and Judah, and wrote letters also to Ephraim and Manasseh, that they should come to the house of Yahweh at Jerusalem, to keep the Passover to Yahweh, the God of Israel.

Kwa maana mfalme na wakuu wake, na kusanyiko lote katika Yerusalemu walifanya shauri kufanya pasaka mwezi wa pili. 2 Mambo ya Nyakati 30:2

For the king had taken counsel, and his princes, and all the assembly in Jerusalem, to keep the Passover in the second month.

Kwa sababu hawakuweza kuifanya wakati ule, kwa kuwa makuhani walikuwa hawajajitakasa wa kutosha, wala watu hawajakusanyika huko Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 30:3

For they could not keep it at that time, because the priests had not sanctified themselves in sufficient number, neither had the people gathered themselves together to Jerusalem.

Likawa neno jema machoni pa mfalme, na kusanyiko lote. 2 Mambo ya Nyakati 30:4

The thing was right in the eyes of the king and of all the assembly.

Basi wakafanya amri kupiga mbiu kati ya Israeli yote, toka Beer-sheba mpaka Dani, ya kwamba watu waje wamfanyie pasaka Bwana, Mungu wa Israeli, huko Yerusalemu; maana tangu siku nyingi hawakuifanya kama vile ilivyoandikwa. 2 Mambo ya Nyakati 30:5

So they established a decree to make proclamation throughout all Israel, from Beersheba even to Dan, that they should come to keep the Passover to Yahweh, the God of Israel, at Jerusalem: for they had not kept it in great numbers in such sort as it is written.

Wakaenda matarishi wenye nyaraka za mfalme na wakuu wake, kati ya Israeli yote na Yuda, na kwa amri ya mfalme, kusema, Enyi wana wa Israeli, mrudieni Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia waliosalia wenu waliookoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru. 2 Mambo ya Nyakati 30:6

So the posts went with the letters from the king and his princes throughout all Israel and Judah, and according to the commandment of the king, saying, You children of Israel, turn again to Yahweh, the God of Abraham, Isaac, and Israel, that he may return to the remnant that have escaped of you out of the hand of the kings of Assyria.

Wala msiwe kama baba zenu, na kama ndugu zenu, waliomwasi Bwana, Mungu wa baba zao, hata akawatoa kuwa ushangao, kama mwonavyo. 2 Mambo ya Nyakati 30:7

Don't be you like your fathers, and like your brothers, who trespassed against Yahweh, the God of their fathers, so that he gave them up to desolation, as you see.

Msiwe sasa wenye shingo ngumu kama baba zenu; lakini mjitoe kwa Bwana, mkaingie katika patakatifu pake, alipopatakasa milele, mkamtumikie Bwana, Mungu wenu, hasira yake kali iwageukie mbali. 2 Mambo ya Nyakati 30:8

Now don't you be stiff-necked, as your fathers were; but yield yourselves to Yahweh, and enter into his sanctuary, which he has sanctified forever, and serve Yahweh your God, that his fierce anger may turn away from you.

Kwa kuwa mkimrudia Bwana, ndugu zenu na watoto wenu watahurumiwa machoni pa hao waliowachukua mateka, nao watairudia nchi hii; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye mwenye neema, na mwenye rehema, wala hatawageuzia mbali uso wake, mkimrudia. 2 Mambo ya Nyakati 30:9

For if you turn again to Yahweh, your brothers and your children shall find compassion before those who led them captive, and shall come again into this land: for Yahweh your God is gracious and merciful, and will not turn away his face from you, if you return to him.

Basi matarishi wakapita mji kwa mji kati ya nchi ya Efraimu na Manase, hata kufika Zabuloni; lakini waliwacheka-cheka, na kuwadhihaki. 2 Mambo ya Nyakati 30:10

So the posts passed from city to city through the country of Ephraim and Manasseh, even to Zebulun: but they ridiculed them, and mocked them.

Ila watu wengine wa Asheri, na wa Manase, na wa Zabuloni walijinyenyekeza, wakaja Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 30:11

Nevertheless certain men of Asher and Manasseh and of Zebulun humbled themselves, and came to Jerusalem.

Tena katika Yuda mkono wa Mungu ulikuwa ukiwapa moyo mmoja, waitimize amri ya mfalme na wakuu kwa neno la Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 30:12

Also on Judah came the hand of God to give them one heart, to do the commandment of the king and of the princes by the word of Yahweh.

Basi wakakusanyika Yerusalemu watu wengi ili kuifanya sikukuu ya mikate isiyochachwa katika mwezi wa pili, kusanyiko kuu sana. 2 Mambo ya Nyakati 30:13

There assembled at Jerusalem much people to keep the feast of unleavened bread in the second month, a very great assembly.

Wakainuka, wakaziondoa madhabahu zilizokuwamo Yerusalemu, nazo madhabahu za kufukizia wakaziondoa, wakazitupa katika kijito Kidroni. 2 Mambo ya Nyakati 30:14

They arose and took away the altars that were in Jerusalem, and all the altars for incense took they away, and cast them into the brook Kidron.

Kisha wakaichinja pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, nao makuhani na Walawi wakatahayarika, wakajitakasa, wakaleta sadaka za kuteketezwa nyumbani mwa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 30:15

Then they killed the Passover on the fourteenth [day] of the second month: and the priests and the Levites were ashamed, and sanctified themselves, and brought burnt offerings into the house of Yahweh.

Wakasimama mahali pao kwa taratibu yao, sawasawa na torati ya Musa, mtu wa Mungu; nao makuhani wakainyunyiza damu, waliyoipokea mikononi mwa Walawi. 2 Mambo ya Nyakati 30:16

They stood in their place after their order, according to the law of Moses the man of God: the priests sprinkled the blood [which they received] of the hand of the Levites.

Kwa maana kulikuwa na wengi katika kusanyiko ambao hawajajitakasa; kwa hiyo Walawi wakamchinjia pasaka, kila mtu asiyekuwa safi, ili kuwatakasa kwa Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 30:17

For there were many in the assembly who had not sanctified themselves: therefore the Levites had the charge of killing the Passovers for everyone who was not clean, to sanctify them to Yahweh.

Kwani wingi wa watu, naam, wengi wa Efraimu, na wa Manase, na wa Isakari, na wa Zabuloni, hawakujisafisha, lakini wakala pasaka, ila si kama ilivyoandikwa. Naye Hezekia alikuwa amewaombea, akisema, Bwana mwema na amsamehe kila mtu, 2 Mambo ya Nyakati 30:18

For a multitude of the people, even many of Ephraim and Manasseh, Issachar and Zebulun, had not cleansed themselves, yet did they eat the Passover otherwise than it is written. For Hezekiah had prayed for them, saying, The good Yahweh pardon everyone

aukazaye moyo wake kumtafuta Mungu, Bwana, Mungu wa babaze, hata ikiwa si kwa utakaso wa patakatifu. 2 Mambo ya Nyakati 30:19

who sets his heart to seek God, Yahweh, the God of his fathers, though not [cleansed] according to the purification of the sanctuary.

Bwana akamsikia Hezekia, akawaponya watu. 2 Mambo ya Nyakati 30:20

Yahweh listened to Hezekiah, and healed the people.

Nao wana wa Israeli waliohudhuria Yerusalemu wakafanya sikukuu ya mikate isiyochachwa siku saba kwa furaha kubwa; Walawi na makuhani wakamsifu Bwana siku kwa siku, wakimwimbia Bwana kwa vinanda vyenye sauti kuu. 2 Mambo ya Nyakati 30:21

The children of Israel who were present at Jerusalem kept the feast of unleavened bread seven days with great gladness; and the Levites and the priests praised Yahweh day by day, [singing] with loud instruments to Yahweh.

Hezekia akawafurahisha mioyo Walawi wote waliokuwa wastadi wa kumtumikia Bwana. Basi muda wa siku saba wakala sikukuu, wakitoa dhabihu za sadaka za amani, na kumtolea shukrani Bwana, Mungu wa baba zao. 2 Mambo ya Nyakati 30:22

Hezekiah spoke comfortably to all the Levites who had good understanding [in the service] of Yahweh. So they ate throughout the feast for the seven days, offering sacrifices of peace-offerings, and making confession to Yahweh, the God of their fathers.

Na kusanyiko lote wakafanya shauri kufanya sikukuu siku saba nyingine; wakafanya sikukuu siku saba nyingine kwa furaha. 2 Mambo ya Nyakati 30:23

The whole assembly took counsel to keep other seven days; and they kept [other] seven days with gladness.

Maana Hezekia, mfalme wa Yuda, aliwatolea kusanyiko matoleo ya ng'ombe elfu, na kondoo elfu saba; na wakuu wakawatolea kusanyiko ng'ombe elfu, na kondoo elfu kumi; tena wakajitakasa makuhani wengi sana. 2 Mambo ya Nyakati 30:24

For Hezekiah king of Judah did give to the assembly for offerings one thousand bulls and seven thousand sheep; and the princes gave to the assembly a thousand bulls and ten thousand sheep: and a great number of priests sanctified themselves.

Na kusanyiko lote la Yuda, pamoja na makuhani na Walawi, na kusanyiko lote waliotoka Israeli, na wageni waliotoka katika nchi ya Israeli, nao waliokaa Yuda, wakafurahi. 2 Mambo ya Nyakati 30:25

All the assembly of Judah, with the priests and the Levites, and all the assembly who came out of Israel, and the foreigners who came out of the land of Israel, and who lived in Judah, rejoiced.

Ikawa furaha kuu katika Yerusalemu; kwa sababu tangu siku za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, hayajakuwako mambo kama hayo huko Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 30:26

So there was great joy in Jerusalem; for since the time of Solomon the son of David king of Israel there was not the like in Jerusalem.

Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni. 2 Mambo ya Nyakati 30:27

Then the priests the Levites arose and blessed the people: and their voice was heard, and their prayer came up to his holy habitation, even to heaven.