2 Mambo ya Nyakati Mlango 11 2nd Chronicles

2 Mambo ya Nyakati 11:1

Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, watu wateule mia na themanini elfu waliokuwa hodari, watu wa vita, ili wapigane juu ya Israeli, ili wamrudishie Rehoboamu huo ufalme.

2 Mambo ya Nyakati 11:2

Lakini neno la Bwana likamjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema,

2 Mambo ya Nyakati 11:3

Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, uwaambie na Israeli wote waliomo Yuda na Benyamini, ukisema,

2 Mambo ya Nyakati 11:4

Bwana asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakayasikiliza maneno ya Bwana, wakarudi katika kumwendea Yeroboamu.

2 Mambo ya Nyakati 11:5

Naye Rehoboamu akakaa Yerusalemu, akajenga miji yenye ngome katika Yuda.

2 Mambo ya Nyakati 11:6

Akajenga na Bethlehemu, na Etamu, na Tekoa,

2 Mambo ya Nyakati 11:7

na Bethsuri, na Soko, na Adulamu,

2 Mambo ya Nyakati 11:8

na Gathi, na Maresha, na Zifu,

2 Mambo ya Nyakati 11:9

na Adoraimu, na Lakishi, na Azeka,

2 Mambo ya Nyakati 11:10

na Sora, na Aiyaloni, na Hebroni, iliyoko katika Yuda na Benyamini, miji yenye maboma.

2 Mambo ya Nyakati 11:11

Akazifanya imara hizo ngome, akaweka majemadari humo, na akiba ya vyakula, na mafuta, na mvinyo.

2 Mambo ya Nyakati 11:12

Na ndani ya miji yote mmoja mmoja aliweka ngao na mikuki, akaifanya kuwa na nguvu nyingi mno. Yuda na Benyamini ikawa milki yake.

2 Mambo ya Nyakati 11:13

Wakamwendea makuhani na Walawi waliokuwa katika Israeli yote, kutoka mpaka wao wote.

2 Mambo ya Nyakati 11:14

Kwani Walawi wakaacha malisho yao, na milki yao, wakaja Yuda na Yerusalemu; kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwatupa, ili wasimfanyie Bwana ukuhani;

2 Mambo ya Nyakati 11:15

naye akajiwekea makuhani wa mahali pa juu, na wa wale majini, na wa zile ndama alizozifanya.

2 Mambo ya Nyakati 11:16

Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu Bwana, Mungu wa baba zao.

2 Mambo ya Nyakati 11:17

Hivyo wakaufanya imara kwa miaka mitatu ufalme wa Yuda, na kumtia nguvu Rehoboamu mwana wa Sulemani; kwa maana muda wa miaka mitatu wakaiendea njia ya Daudi na Sulemani.

2 Mambo ya Nyakati 11:18

Rehoboamu akaoa mke, Mahalathi binti Yerimothi mwana wa Daudi, na wa Abihaili binti Eliabu, mwana wa Yese;

2 Mambo ya Nyakati 11:19

akamzalia wana, Yeushi, na Shemaria, na Zahamu.

2 Mambo ya Nyakati 11:20

Kisha baada yake akamwoa Maaka, binti Absalomu; na yeye akamzalia Abiya, na Atai, na Ziza, na Shelomithi.

2 Mambo ya Nyakati 11:21

Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu kuliko wakeze wote na masuria yake; (maana alioa wake kumi na wanane, na masuria sitini, akazaa wana ishirini na wanane na binti sitini).

2 Mambo ya Nyakati 11:22

Rehoboamu akamsimamisha Abiya, mwana wa Maaka, kuwa mkuu, mtawala kati ya nduguze, kwa kuwa aliazimia kumtawaza awe mfalme.

2 Mambo ya Nyakati 11:23

Akafanya kwa akili, akawatawanya wanawe wote kati ya nchi zote za Yuda na Benyamini, katika kila mji wenye boma; akawapa vyakula tele. Akawatafutia wake wengi.