2 Mambo ya Nyakati Mlango 13 2nd Chronicles

2 Mambo ya Nyakati 13:1

Katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu, akaanza Abiya kutawala juu ya Yuda.

2 Mambo ya Nyakati 13:2

Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka binti Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.

2 Mambo ya Nyakati 13:3

Abiya akapanga vita mwenye jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule mia nne elfu; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake mwenye watu wateule mia nane elfu, waliokuwa waume mashujaa.

2 Mambo ya Nyakati 13:4

Basi Abiya akasimama juu ya kilima cha Semaraimu, kilichoko milimani mwa Efraimu, akasema, Nisikieni, enyi Yeroboamu na Israeli wote;

2 Mambo ya Nyakati 13:5

je! Haikuwapasa kujua ya kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi?

2 Mambo ya Nyakati 13:6

Lakini Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumwa wa Sulemani mwana wa Daudi, akainuka, akamfanyia fitina bwana wake.

2 Mambo ya Nyakati 13:7

Wakamkusanyikia watu mabaradhuli, wasiofaa kitu, waliojitia nguvu juu ya Rehoboamu mwana wa Sulemani, Rehoboamu alipokuwa kijana na wa moyo mwororo, asiweze kuwazuia.

2 Mambo ya Nyakati 13:8

Hata sasa mwajidhania kuwa mtauzuia ufalme wa Bwana mikononi mwa wana wa Daudi; nanyi mmekuwa jamii kubwa, na kwenu mna ndama za dhahabu alizowafanyia Yeroboamu kuwa miungu.

2 Mambo ya Nyakati 13:9

Je! Hamkuwafukuza makuhani wa Bwana, wana wa Haruni, na Walawi; mkajifanyia makuhani kama wafanyavyo watu wa nchi nyingine? Hata ye yote ajaye kujifanya wakfu na ndama, na kondoo waume saba, aweza kuwa kuhani wa hiyo isiyo miungu.

2 Mambo ya Nyakati 13:10

Lakini sisi, Bwana ndiye Mungu wetu, wala sisi hatukumwacha; tena tunao makuhani wanaomtumikia Bwana, wana wa Haruni, na Walawi, kwa kazi yao;

2 Mambo ya Nyakati 13:11

nao humtolea Bwana kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi twayalinda malinzi ya Bwana, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha.

2 Mambo ya Nyakati 13:12

Na tazama, Mungu yu pamoja nasi atutangulie, na makuhani wake wenye mapanda, ili wapige sauti ya kugutusha juu yenu. Enyi wana wa Israeli, msipigane na Bwana, Mungu wa baba zenu; kwani hamtafanikiwa.

2 Mambo ya Nyakati 13:13

Lakini Yeroboamu aliwazungushia waviziao kwa nyuma; basi wao wakawa mbele ya Yuda, na wale waviziao nyuma yao.

2 Mambo ya Nyakati 13:14

Na Yuda walipotazama nyuma, angalia, vita vikawa mbele na nyuma; wakamlilia Bwana, na makuhani wakapiga mapanda.

2 Mambo ya Nyakati 13:15

Ndipo wakapiga kelele watu wa Yuda; ikawa, watu na Yuda walipopiga kelele, Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.

2 Mambo ya Nyakati 13:16

Wana wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda; naye Mungu akawaua mikononi mwao.

2 Mambo ya Nyakati 13:17

Abiya na watu wake wakawapiga mapigo makuu; hata wakaanguka wameuawa wa Israeli mia tano elfu, watu wateule.

2 Mambo ya Nyakati 13:18

Ndivyo walivyotiishwa wana wa Israeli wakati ule, wakashinda wana wa Yuda, kwa kuwa walimtegemea Bwana, Mungu wa baba zao.

2 Mambo ya Nyakati 13:19

Abiya akamfuata Yeroboamu, akamnyang'anya miji, Betheli na miji yake, na Yeshana na miji yake, na Efroni na miji yake.

2 Mambo ya Nyakati 13:20

Wala Yeroboamu hakupata nguvu tena siku za Abiya; kisha Bwana akampiga, akafa.

2 Mambo ya Nyakati 13:21

Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana ishirini na wawili, na binti kumi na sita.

2 Mambo ya Nyakati 13:22

Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.