2 Mambo ya Nyakati 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 2 (Swahili) 2nd Chronicles 2 (English)

Basi Sulemani alikusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana, na kuujengea ufalme wake nyumba. 2 Mambo ya Nyakati 2:1

Now Solomon purposed to build a house for the name of Yahweh, and a house for his kingdom.

Sulemani akahesabu watu sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na watu themanini elfu wawe wachongaji milimani, na elfu tatu na mia sita wawe wasimamizi wao. 2 Mambo ya Nyakati 2:2

Solomon counted out seventy thousand men to bear burdens, and eighty thousand men who were stone cutters in the mountains, and three thousand and six hundred to oversee them.

Sulemani akatuma watu kwa Hiramu mfalme wa Tiro,akisema ,kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, na kumletea mierezi , ajijengee nyumba ya kukaa ,unitendee na mimi. 2 Mambo ya Nyakati 2:3

Solomon sent to Huram the king of Tyre, saying, As you dealt with David my father, and sent him cedars to build him a house in which to dwell, [even so deal with me].

Angalia, najenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za Bwana, Mungu wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 2:4

Behold, I am about to build a house for the name of Yahweh my God, to dedicate it to him, and to burn before him incense of sweet spices, and for the continual show bread, and for the burnt offerings morning and evening, on the Sabbaths, and on the new moons, and on the set feasts of Yahweh our God. This is [an ordinance] forever to Israel.

Nayo nyumba nitakayoijenga ni kubwa; kwa sababu Mungu wetu ndiye mkuu juu ya miungu yote. 2 Mambo ya Nyakati 2:5

The house which I build is great; for great is our God above all gods.

Lakini ni nani awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya kufukizia fukizo mbele zake? 2 Mambo ya Nyakati 2:6

But who is able to build him a house, seeing heaven and the heaven of heavens can't contain him? who am I then, that I should build him a house, save only to burn incense before him?

Unipelekee basi mtu mstadi wa kazi ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya urujuani, na nyekundu, na samawi, mwenye kujua kuchora machoro, pamoja na wastadi walioko Yuda na Yerusalemu pamoja nami, aliowaweka baba yangu Daudi. 2 Mambo ya Nyakati 2:7

Now therefore send me a man skillful to work in gold, and in silver, and in brass, and in iron, and in purple, and crimson, and blue, and who knows how to engrave [all manner of] engravings, [to be] with the skillful men who are with me in Judah and in Jerusalem, whom David my father did provide.

Niletee tena mierezi, na miberoshi, na miti ya msandali kutoka Lebanoni; maana najua ya kwamba watumishi wako hujua sana kuchonga miti Lebanoni; na tazama, watumishi wangu watakuwa pamoja na watumishi wako, 2 Mambo ya Nyakati 2:8

Send me also cedar trees, fir trees, and algum trees, out of Lebanon; for I know that your servants know how to cut timber in Lebanon: and, behold, my servants shall be with your servants,

ili wanitengenezee miti kwa wingi; kwani nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa ajabu. 2 Mambo ya Nyakati 2:9

even to prepare me timber in abundance; for the house which I am about to build shall be great and wonderful.

Na tazama, nitawapa watumishi wako, wachongaji wakatao miti, kori ishirini elfu za ngano iliyopondwa , na kori ishirini elfu za shayiri , na bathi ishirini elfu za mvinyo,na bathi ishirini elfu za mafuta. 2 Mambo ya Nyakati 2:10

Behold, I will give to your servants, the cutters who cut timber, twenty thousand measures of beaten wheat, and twenty thousand measures of barley, and twenty thousand baths of wine, and twenty thousand baths of oil.

Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akajibu kwa waraka, aliompelekea Sulemani, Ni kwa sababu Bwana awapenda watu wake, amekufanya uwe mfalme juu yao. 2 Mambo ya Nyakati 2:11

Then Huram the king of Tyre answered in writing, which he sent to Solomon, Because Yahweh loves his people, he has made you king over them.

Hiramu akasema tena, Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, aliyezifanya mbingu na nchi, ambaye amempa mfalme Daudi mwana wa hekima, mwenye busara na akili, ili amjengee Bwana nyumba, na nyumba kwa ufalme wake. 2 Mambo ya Nyakati 2:12

Huram said moreover, Blessed be Yahweh, the God of Israel, that made heaven and earth, who has given to David the king a wise son, endowed with discretion and understanding, that should build a house for Yahweh, and a house for his kingdom.

Na sasa nimemtuma mtu mstadi, mwenye akili, yaani, Hiramu baba yangu. 2 Mambo ya Nyakati 2:13

Now I have sent a skillful man, endowed with understanding, of Huram my father's,

mwana wa mwanamke wa binti za Dani, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, ajuaye sana kazi ya dhahabu, na ya fedha, ya shaba, ya chuma, ya mawe, na ya mti, ya urujuani, ya samawi, na ya kitani safi, na ya nyekundu; tena mstadi wa kuchora machoro yo yote, na wa kufikiri fikira yo yote; apate kuagiziwa kazi pamoja na watu wako wastadi, tena na wastadi wa bwana wangu Daudi baba yako. 2 Mambo ya Nyakati 2:14

the son of a woman of the daughters of Dan; and his father was a man of Tyre, skillful to work in gold, and in silver, in brass, in iron, in stone, and in timber, in purple, in blue, and in fine linen, and in crimson, also to engrave any manner of engraving, and to devise any device; that there may be [a place] appointed to him with your skillful men, and with the skillful men of my lord David your father.

Basi sasa hiyo ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, aliyonena bwana wangu, na wapelekewe watumishi wake; 2 Mambo ya Nyakati 2:15

Now therefore the wheat and the barley, the oil and the wine, which my lord has spoken of, let him send to his servants:

nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaichukua Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 2:16

and we will cut wood out of Lebanon, as much as you shall need; and we will bring it to you in floats by sea to Joppa; and you shall carry it up to Jerusalem.

Ndipo Sulemani akawahesabu wageni wote waliokuwamo katika nchi ya Israeli, sawasawa na hesabu aliyowahesabu Daudi baba yake; wakatokea mia hamsini na tatu elfu, na mia sita. 2 Mambo ya Nyakati 2:17

Solomon numbered all the foreigners who were in the land of Israel, after the numbering with which David his father had numbered them; and they were found one hundred fifty-three thousand six hundred.

Akaweka katika hao sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na themanini elfu wawe wachongaji milimani, na wasimamizi elfu tatu na mia sita, ili wawatie watu kazini. 2 Mambo ya Nyakati 2:18

He set seventy thousand of them to bear burdens, and eighty thousand who were stone cutters in the mountains, and three thousand six hundred overseers to set the people at work.