2 Mambo ya Nyakati 33 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 33 (Swahili) 2nd Chronicles 33 (English)

Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka hamsini na mitano. 2 Mambo ya Nyakati 33:1

Manasseh was twelve years old when he began to reign; and he reigned fifty-five years in Jerusalem.

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo yote ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 33:2

He did that which was evil in the sight of Yahweh, after the abominations of the nations whom Yahweh cast out before the children of Israel.

Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopabomoa Hezekia babaye; akazisimamisha madhabahu za mabaali, akafanya na sanamu za maashera, akaabudu jeshi lote la mbinguni, na kulitumikia. 2 Mambo ya Nyakati 33:3

For he built again the high places which Hezekiah his father had broken down; and he reared up altars for the Baals, and made Asheroth, and worshiped all the host of the sky, and served them.

Akajenga madhabahu katika nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu litakuwako jina langu milele. 2 Mambo ya Nyakati 33:4

He built altars in the house of Yahweh, of which Yahweh said, In Jerusalem shall my name be forever.

Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika nyua mbili za nyumba ya Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 33:5

He built altars for all the host of the sky in the two courts of the house of Yahweh.

Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. 2 Mambo ya Nyakati 33:6

He also made his children to pass through the fire in the valley of the son of Hinnom; and he practiced sorcery, and used enchantments, and practiced sorcery, and dealt with those who had familiar spirits, and with wizards: he worked much evil in the sight of Yahweh, to provoke him to anger.

Akaiweka sanamu ya kuchonga aliyoifanya, katika nyumba ya Mungu ambayo Mungu alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele; 2 Mambo ya Nyakati 33:7

He set the engraved image of the idol, which he had made, in the house of God, of which God said to David and to Solomon his son, In this house, and in Jerusalem, which I have chosen out of all the tribes of Israel, will I put my name forever:

wala sitawaondoshea miguu tena Israeli katika nchi niliyowaagizia baba zenu; wakiangalia tu kutenda yote niliyowaamuru, yaani, torati yote, na sheria, na maagizo, niliyowaamuru kwa mkono wa Musa. 2 Mambo ya Nyakati 33:8

neither will I any more remove the foot of Israel from off the land which I have appointed for your fathers, if only they will observe to do all that I have commanded them, even all the law and the statutes and the ordinances [given] by Moses.

Basi Manase akawakosesha Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, hata wakazidi kufanya mabaya kuliko mataifa, aliowaharibu Bwana mbele ya wana wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 33:9

Manasseh seduced Judah and the inhabitants of Jerusalem, so that they did evil more than did the nations whom Yahweh destroyed before the children of Israel.

Naye Bwana akasema na Manase, na watu wake; wala wasiangalie. 2 Mambo ya Nyakati 33:10

Yahweh spoke to Manasseh, and to his people; but they gave no heed.

Kwa hiyo Bwana akaleta juu yao maakida wa jeshi la mfalme wa Ashuru, waliomkamata Manase kwa minyororo, wakamfunga kwa pingu, wakamchukua mpaka Babeli. 2 Mambo ya Nyakati 33:11

Therefore Yahweh brought on them the captains of the host of the king of Assyria, who took Manasseh in chains, and bound him with fetters, and carried him to Babylon.

Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi Bwana, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. 2 Mambo ya Nyakati 33:12

When he was in distress, he begged Yahweh his God, and humbled himself greatly before the God of his fathers.

Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba Bwana ndiye Mungu. 2 Mambo ya Nyakati 33:13

He prayed to him; and he was entreated of him, and heard his supplication, and brought him again to Jerusalem into his kingdom. Then Manasseh knew that Yahweh he was God.

Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya lango la samaki; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka maakida mashujaa katika miji yote ya Yuda yenye maboma. 2 Mambo ya Nyakati 33:14

Now after this he built an outer wall to the city of David, on the west side of Gihon, in the valley, even to the entrance at the fish gate; and he compassed Ophel about [with it], and raised it up to a very great height: and he put valiant captains in all the fortified cities of Judah.

Akaiondoa miungu migeni, na hiyo sanamu nyumbani mwa Bwana, na madhabahu zote alizozijenga katika mlima wa nyumba ya Bwana, na Yerusalemu, akazitupa nje ya mji. 2 Mambo ya Nyakati 33:15

He took away the foreign gods, and the idol out of the house of Yahweh, and all the altars that he had built in the mountain of the house of Yahweh, and in Jerusalem, and cast them out of the city.

Akaijenga madhabahu ya Bwana, akatoa juu yake dhabihu za sadaka za amani, na za shukrani, akawaamuru Yuda wamtumikie Bwana, Mungu wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 33:16

He built up the altar of Yahweh, and offered thereon sacrifices of peace-offerings and of thanksgiving, and commanded Judah to serve Yahweh, the God of Israel.

Lakini watu wakaendelea kutoa dhabihu katika mahali pa juu, ila wakamtolea Bwana, Mungu wao tu. 2 Mambo ya Nyakati 33:17

Nevertheless the people sacrificed still in the high places, but only to Yahweh their God.

Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji walionena naye kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa kati ya mambo ya wafalme wa Israeli. 2 Mambo ya Nyakati 33:18

Now the rest of the acts of Manasseh, and his prayer to his God, and the words of the seers who spoke to him in the name of Yahweh, the God of Israel, behold, they are written among the acts of the kings of Israel.

Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika tarehe ya Hozai. 2 Mambo ya Nyakati 33:19

His prayer also, and how [God] was entreated of him, and all his sin and his trespass, and the places in which he built high places, and set up the Asherim and the engraved images, before he humbled himself: behold, they are written in the history of Hozai.

Basi Manase akalala na babaze, wakamzika nyumbani mwake; na Amoni mwanawe akatawala mahali pake. 2 Mambo ya Nyakati 33:20

So Manasseh slept with his fathers, and they buried him in his own house: and Amon his son reigned in his place.

Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka miwili. 2 Mambo ya Nyakati 33:21

Amon was twenty-two years old when he began to reign; and he reigned two years in Jerusalem.

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kama alivyofanya Manase babaye; Amoni akazitolea dhabihu sanamu zote alizozifanya Manase babaye, akazitumikia. 2 Mambo ya Nyakati 33:22

He did that which was evil in the sight of Yahweh, as did Manasseh his father; and Amon sacrificed to all the engraved images which Manasseh his father had made, and served them.

Wala hakujinyenyekeza mbele za Bwana, kama Manase babaye alivyojinyenyekeza; lakini huyo Amoni akaongeza makosa juu ya makosa. 2 Mambo ya Nyakati 33:23

He didn't humble himself before Yahweh, as Manasseh his father had humbled himself; but this same Amon trespassed more and more.

Wakamfanyia fitina watumishi wake, wakamwua katika nyumba yake mwenyewe. 2 Mambo ya Nyakati 33:24

His servants conspired against him, and put him to death in his own house.

Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliomfanyia fitina mfalme Amoni; watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme badala yake. 2 Mambo ya Nyakati 33:25

But the people of the land killed all those who had conspired against king Amon; and the people of the land made Josiah his son king in his place.