Isaya 63 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 63 (Swahili) Isaiah 63 (English)

Ni nani huyu atokaye Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Isaya 63:1

Who is this who comes from Edom, with dyed garments from Bozrah? this who is glorious in his clothing, marching in the greatness of his strength? I who speak in righteousness, mighty to save.

Kwani mavazi yako kuwa mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu? Isaya 63:2

Why are you red in your clothing, and your garments like him who treads in the wine vat?

Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote. Isaya 63:3

I have trodden the winepress alone; and of the peoples there was no man with me: yes, I trod them in my anger, and trampled them in my wrath; and their lifeblood is sprinkled on my garments, and I have stained all my clothing.

Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu, Na mwaka wao niliowakomboa umewadia. Isaya 63:4

For the day of vengeance was in my heart, and the year of my redeemed is come.

Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza. Isaya 63:5

I looked, and there was none to help; and I wondered that there was none to uphold: therefore my own arm brought salvation to me; and my wrath, it upheld me.

Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nikaimwaga damu yao chini. Isaya 63:6

I trod down the peoples in my anger, and made them drunk in my wrath, and I poured out their lifeblood on the earth.

Nitautaja wema wa Bwana, sifa za Bwana kwa yote aliyotukirimia Bwana; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Isaya 63:7

I will make mention of the loving kindnesses of Yahweh, [and] the praises of Yahweh, according to all that Yahweh has bestowed on us, and the great goodness toward the house of Israel, which he has bestowed on them according to his mercies, and according to the multitude of his loving kindnesses.

Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao. Isaya 63:8

For he said, Surely, they are my people, children who will not deal falsely: so he was their Savior.

Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. Isaya 63:9

In all their affliction he was afflicted, and the angel of his presence saved them: in his love and in his pity he redeemed them; and he bore them, and carried them all the days of old.

Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao. Isaya 63:10

But they rebelled, and grieved his holy Spirit: therefore he was turned to be their enemy, [and] himself fought against them.

Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu? Isaya 63:11

Then he remembered the days of old, Moses [and] his people, [saying], Where is he who brought them up out of the sea with the shepherds of his flock? where is he who put his holy Spirit in the midst of them?

Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kuume wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele? Isaya 63:12

who caused his glorious arm to go at the right hand of Moses? who divided the waters before them, to make himself an everlasting name?

Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae? Isaya 63:13

who led them through the depths, as a horse in the wilderness, so that they didn't stumble?

Kama ng'ombe washukao bondeni, Roho ya Bwana akawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu. Isaya 63:14

As the cattle that go down into the valley, the Spirit of Yahweh caused them to rest; so did you lead your people, to make yourself a glorious name.

Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu. Isaya 63:15

Look down from heaven, and see from the habitation of your holiness and of your glory: where are your zeal and your mighty acts? the yearning of your heart and your compassion is restrained toward me.

Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako. Isaya 63:16

For you are our Father, though Abraham doesn't know us, and Israel does not acknowledge us: you, Yahweh, are our Father; our Redeemer from everlasting is your name.

Ee Bwana, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako. Isaya 63:17

O Yahweh, why do you make us to err from your ways, and harden our heart from your fear? Return for your servants' sake, the tribes of your inheritance.

Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako. Isaya 63:18

Your holy people possessed [it] but a little while: our adversaries have trodden down your sanctuary.

Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako. Isaya 63:19

We are become as they over whom you never bear rule, as those who were not called by your name.